We utakuwa mzanzibara. Nasubiri muungano ufe tukutimueKUEPUKANA NA KUFUATWA FUATWA NA NZI ONDOA CHAKULA ULICHOBEBA UBAVUNI.
Wazanzibar mmewanyonya vyakutosha na kuwadhulumu kwakiwango kisichoelezeka. Wanataka sasa nchi yao yenye mamlaka kamili nyie mwalalamikia udouble standard wao. Wenye double standard ni sisi watanganyika/serikali isiyotaka kuwaacha wazanzibar na taifa lao.
Kwanini tunaendelea kuwanyonya na kuiharibu Zanzibar yao huku twajifanya eti wao ndio wananufaika? Mnaogopa nini kuwapa taifa lao? Au mnaogopa nchi kuongozwa na sheria za dini ndio maana gharama kubwa yatumika kuulinda muungano/ukoloni kwa wazanzibar?
Mkuu mimi nazungumzia maslahi ya nchi, sio u-CHADEMA wala u-CCM. Hilo la external influence liko wazi kabisa wala halihitaji speculations! Soma taarifa ya Siri ya CIA juu ya Mapinduzi ya Zanzibar, 1964 in context ndio utaelewa namaanisha nini hapa!Hapa ndugu unaimba wimbo moyo wako unapenda kabisa. Hapa nawe umekuwa mwanaCCM kwakuwa inaulinda muungano ambao upo kwa ajili ya kupambana na uislamu kama maelezo yako yanavyojieleza.
Wewe ni CHADEMA damu lakini hapa unaiunga mkono CCM kisa CIA inaisapoti ili kuhakikisha muungano haufi ili kupambana na uislamu usijefanya zanzibar dola ya kidini huoni wewe pia ni double agent mkuu!!? Hapa unajifanya kuibebesha CCM majukumu/responsibility kuwa ndio inajua pekee inachokifanya na kumbe nawe ndio ngoma unapenda CCM iendelee kucheza.
Huu ndio unafiki ambao mimi ninauchukia kwasababu nyie chadema hata serikali tatu mwazitaka kwa makusudio ya kisiasa tu lakini hampo tayari muungano kuvunjwa. Nyie mwataka kuja endeleza utawala wa ki imla kama aliokuwa akiuendesha Nyerere.
KUEPUKANA NA KUFUATWA FUATWA NA NZI ONDOA CHAKULA ULICHOBEBA UBAVUNI. Wazanzibar mmewanyonya vyakutosha na kuwadhulumu kwakiwango kisichoelezeka. Wanataka sasa nchi yao yenye mamlaka kamili nyie mwalalamikia udouble standard wao. Wenye double standard ni sisi watanganyika/serikali isiyotaka kuwaacha wazanzibar na taifa lao. Kwanini tunaendelea kuwanyonya na kuiharibu zanzibar yao huku twajifanya eti wao ndio wananufaika? Mnaogopa nini kuwapa taifa lao? Au mnaogopa nchi kuongozwa na sheria za dini ndio maana gharama kubwa yatumika kuulinda muungano/ukoloni kwa wazanzibar?
Sijazungumzia suala "Takwimu" zilizotolewa kwenye Tume ya Warioba bali ni kauli ya "Zanzibar Sio Nchi" ilipotolewa na Jaji Agustino Ramadhan hatukuona pilikapilika za Kubadili Katiba ya Zanzibar, 1984 ili Zanzibar iwe "nchi" lakini PM Pinda, mtoto wa Mkulima aliponyanyua tu mdomo, unajua kilichotokea!mbona unataka ku-divert mada kwa makusudi?
Wanafiki ni viumbe wabaya sana!
Linapokuja suala la Muungano basi utawaona wako sera za CCM! Na kujifanya watu wa karibu saaana na CCM!
Likija suala la Uongozi wa nchi wanavaa yale yale magwanda yao ya CDM!
Hivi huu unafiki utaisha lini!?
Kwa hiyo wewe fikra zako zinaishia hapo kwenye mafuta au ndio muendelezo wa kejeli kwa wazanzibar? Zanzibar ni taifa lenye kila utajiri na zanzibar ni taifa ambalo kwa hadhi yake halikupaswa kuwa ombaomba kwa Watanganyika. Leo hii Zanzibar ndio inategemea eti iwezeshwe na watanganyika ili kuendesha nchi wakati Zanzibar inautajiri wa kuweza kuindesha serikali bila kuwa ombaomba. Maliasili zinabebwa kinyemela kutoka Zanzibar na kuja kuinufaisha Tanganyika kisha Twasema Zanzibar inategemea Tanganyika.
Sasa mimi nashindwa kuwaelewa maccm,hivi kwanin. Huwa mnapinga serikali tatu kwenye rasimu ya katiba kama kweli mnauchungu nazenji mlitakiwa kulipigania hili lipite
Cc boko halam,biggshow,Buchanan
What the hell is double standard nyinyi??acheni unafiki wenu...!!
Watu mmekaa kushingilia jambo moja kila siku kwa maslahi yenu huku mmeweka pamba maskion ndio nin sasa??
Kama wao wazanzibar wenyewe wanataka taifa lao iweje nyinyi muendelee kuwawekea ngumu na kuwatolea kauli za kejeli?
What is double standard wakati watu wameweka nia yao mbele na inaonekana?
Mkuu mimi nazungumzia maslahi ya nchi, sio u-CHADEMA wala u-CCM. Hilo la external influence liko wazi kabisa wala halihitaji speculations! Soma taarifa ya Siri ya CIA juu ya Mapinduzi ya Zanzibar, 1964 in context ndio utaelewa namaanisha nini hapa!
Kwa taarifa yako hata Constitutional Review Commission (CRC) ya akina Warioba walilijadili hili kwa kirefu sana!
Ukweli ndo huo, wewe baki na "CHADEMA/CCM Politics," dunia inaendeshwa kwa underground movements kwa kiasi kikubwa!
Sio unafiki, watu hatuangalii "personalities" tunaangalia masuala! Ukweli ni ukweli tu hata kama utasemwa na Shetani!
Nini Pinda kwa upande wa Zanzibar hata JK akisema Zanzibar siyo nchi watamjia juu,kwa sababu kwani
yeye ni nani kwenye nchi ya Zanzibar?? Tatizo ni unafiki wa watanganyika kujifanya tunang'anga'na na
Zanzibar na kuendelea kuendesha Tanganyika kwa mgongo wa Tanzania'
Kwa nini tuiachie Zanzibar wajukuu wa sultani! Mnadhani Watanganyika wajinga waache ndugu zao warejeshwe kwenye utumwa?
Sasa mimi nashindwa kuwaelewa maccm,hivi kwanin. Huwa mnapinga serikali tatu kwenye rasimu ya katiba kama kweli mnauchungu nazenji mlitakiwa kulipigania hili lipite
Cc boko halam,biggshow,Buchanan
Angalia sana mkuu, ukisema ukweli sana juu ya hili utaitwa mwana Chadema. Imefika mahali watu hawataki tena kufikirisha ubongo wao bali kurukia mambo ya itikadi za vyama tu.
We utakuwa mzanzibara. Nasubiri muungano ufe tukutimue
Hata Zanzibar inaing'ang'ania Tanzania, ndio maana wanaishi popote katika nchi hii bila kuulizwa na mtu yeyote! Wanaongoza Wizara na Idara zisizo za Muungano bila hofu yoyote! Pia tumesikia kauli mbalimbali za Wazanzibari wenyewe wakiombea Muungano wa Serikali 2 uendelee! Hata wale wasioupenda kabisa Muungano still bado wanataka Muungano wa "Nkataba!"
Hawa Wazenj wanakuwa kama wanawake akitaka umpende zaidi atatishia kurudi kwao, huku akibaki pale pale!
Kwa hiyo asikudanganye mtu, hakuna wanaoung'ang'ania Muungano kama Wazanzibari!
Mkuu kwanza nakuomba upunguze kunipiga Ban kwakumsalandia bwana mdogo Lema na unawaacha wanaomtukana Jk. Nimeyasema haya kwakuwa wahenga wana msemo wao wasemao UMUONAPO ZUMBE HAPOHAPO MSALIMIE. Tukirudi kwenye mnakasha nikubaliane na wewe kuhusu hili la influence ya nje katika politics zetu na bila shaka ni kila nchi yeyote duniani haikosi hali hiyo. Lakini Unapowasema wazanzibar ati ni double standard kwenye kauli zao kuhusu masuala ya muungano ni vyema na wewe pia ukajipima ni msafi kiasi gani. Kumbuka unapomnyooshea kidole kimoja mwenzako vyengine vinne vinakuzodoa mwenyewe. Uzuri tunafahamiana humu ndani kwa maandiko yetu ndio maana nakuambia wenye undumilakuwili sio wazanzibar tu bali sisi watanganyika ni zaidi ya hapo. Therefore if we wish to solve the problem then we should remove our hypocratical ideas and deed. Lazima tukisema flani ni mzinzi ni vyema tujitathmini sisi ni wasafi kiasi gani. Arrasso!?