Inaitwa "Chroma Keying". Ni technology ambayo humtoa mtu kutoka background moja na kumuweka kwenye nyingine. Kinachofanyika ni kwamba wanaweka pazia/shuka nyuma ya mtu (kama wanavyofanya kwenye passport size). Tofauti na passport size ambapo huwa ni kichwa tu, lenyewe ni mwili wote. Sharti ni huwa usivae nguo zenye rangi sawa na pazia.
Baada ya hapo wanarekodi video(bado pazia likiwa nyuma). Mfano wanaweza kurekodi unajibizana na mtu(kama wanavyofanya kwa twins) ingawa kiukweli unaongea peke yako. Katika kurekodi, yake majibizano yanakuwa yamepangwa kiasi kwamba unaacha nafasi kidogo kila unapomaliza kuongea(nitaelezea hili kwanini). Wakishamaliza, wanaenda kwenye computer. Huko ndio utundu.
Kwenye computer, ile video wanaedit hivi: kama pazia la nyuma lilikuwa la kijani, basi wanatoa/wanafuta ukijani wote kwenye picha au kama pazia lilikuwa ni la blue basi wanatoa/wanafuta ubluu wote, na ndio maana huwa unaambiwa usivae nguo yenya rangi sawa na pazia kwa sababu na wewe nguo zako zitatolewa/zitafutwa.
Ikishafanyika hivyo inamaana anabaki mtu na nyuma panabaki empty/transparent. Hapo, watachukua icho kipande halafu wataenda kukipachika kwenye sehemu ambapo majibizano inabidi yafanyike. Mtu yule yule atabadilisha nguo na kurekodiwa(maybe sebuleni) akifanya majibizano ila safari hii anatoa majibu ya yale majibizano ya kwanza na hakuna pazia nyuma hivyo kama kuna viti, tv, na meza vitaonekana na yule wa kwanza kwa vile nyuma hamna kitu yaani transparent, basi akipachikwa pale naye viti, tv na meza vya yule wa pili vitaonekana. Mfano:-
yule wa kwanza:"We ulikuwa wapi?"
huyu wa pili:"Nilienda town mara moja kaka"
unakumbuku yule wa kwanza nyuma kulitolewa kukabaki hamna kitu, akabaki mtu tu? Sasa wanamchukua huyo mtu na kumbandika kwenye video ya pili na kama ni majibizano basi watawekwa wanatazamana. Kama unakumbuka nilisema yule wa kwanza anaongea lakini anaacha muda kidogo kila anapomaliza sentensi. Pale anapoacha muda ndio anatoa nafasi kwa huyu wa pili kutoa jibu. Kwa wale walio advance wanaweza wakafanya zaidi na kuweka hata muingiliano na mpaka wote wawili kugusana!
Hiyo ndio inaitwa CHROMA KEYING. Kwenye Adobe AfterEffects plugin ya Keylight inaweza ikafanya hii. Kutokana na rangi ya shuka iliyotumika wengine huita green screening na wengine blue screening lakini huwa wanasahau kwamba rangi tofauti hutumika na hivyo kuepuka majina mengi mengi huitwa Chroma Keying.
Rangi ya shuka hutegemea vitu. Mfano, kama kipande kinahitaji rangi ya kijani, hawawezi kufanya green screening kwa sababu watatoa ukijani wote(unakumbuka?) hivyo watafanya blue screening na sio green screening. Pia, wenzetu wazungu wengine macho yao iris (sehemu ya ndani ya jicho) ina rangi ya blue hivyo wakifanya blue screening na kutoa ubluu wataharibu muonekano wa macho so watafanya green screening na sio blue screening. I hope nimesaidia kidogo. Ahsante.
GIVENALITY.