Nimesikiliza mahojiano kati ya Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi Na mwandishi wa Habari ,katika mazungumzo hayo Mbatia kasema.
1. Watu wakiendelea kumsakama Kwa kumuita msaliti,atamwaga siri zote za UKAWA Na nani alikuwa anasaidia UKAWA.
2. Analalamika kuwa UKAWA ulisababisha Idadi ya Wabunge kutoka NCCR Mageuzi kuporomoka kutoka watano mpaka mmoja,Na pia hata ile nafasi moja ya Mbunge wa Afrika Mashariki wakaipoteza.
3. Analalamika pia hata Makao Makuu ya UKAWA hayakuwa NCCR.
Baada ya kumsikiliza Mbatia nimejiuliza maswali mengi
1. Kwa nini Mh Mbatia analalamika leo kuhusu UKAWA?
2. Mbatia anahofia nini kueleza nia ovu ya UKAWA Kama kweli analitakia heri taifa hili?
3. Je Mbeya ni Jimbo la Mbatia? Na je, ni jimboni kwa mbunge wa NCCR au? Kama sivyo je, kauli iliyotolewa kwamba kila mbunge afanye shughuli za siasa jimboni kwake haikumhusu Mbatia?
4. Kama ina mhusu imekuwaje kwenda kutoa hamasa Mbeya? Je, tayari Kampein zimeshaanza kwa vyama vyote na Mbatia kaona kwa kuanza kueleza sera za chama chake ni Mbeya?
Kama Mbatia ana mapenzi Na nchi yake, anahofia nini kueleza hayo mabaya ya UKAWA?
In God we Trust