DAWATI LA HATUDANGANYIKI limepokea taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vyake kuwa kuwa mara tu baada ya mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CHADEMA, siku ya Jumamosi tarehe 28 Agosti 2010 wakuu wa Idara ya intelejensia walikutana na timu ya Kampeni ya CCM kwa ajili ya kutoa mlisho nyuma, na kupanga mikakati ya kuikabili CHADEMA, na yafuatayo yalijiri:-
a)Idara ililazimika kutolea ufafanuzi sababu zilizopelekea shauri wake wa kutaka matangazo ya TBC ya mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CHADEMA kurejeshwa mara moja baada ya kukatizwa. Walieleza kuwa ilitokana na maelfu ya wananchi waliohudhuruia mkutano huo kuwa wa kwanza kugundua kukatishwa kwa matangazo hayo na kuamua wenyewe, bila ya kushawishiwa na kiongozi yeyote kuchukua hatua kali sana dhidi ya TBC. Viongozi wa CHADEMA walistukia tuu mkutano ukitaka kuvurugika kwa wananchi kudai vikali kurejeshwa kwa matangazo hayo. Ilielezwa kuwa kuvurugika kwa mkutano ikwa sababu ya kukatishwa kwa matangazo ya chombo cha umaa kama TBC iimeelezwa kuwa ingekuwa ni aibu kubwa kwa Serikali na TBC.
b)Idara ilitoa taarifa kuwa licha ya umati wa watu waliohudhuria kutofikia ule wa mkutano wa uzinduzi wa CCM, lakini kwa kuwa umati huo kila mtu alijinyanyua kutoka atokako na kuja Jangwani kwa ajili ya CHADEMA tofauti na maandalizi makubwa ya usafiri, fedha, burudani za kila aina, viburudisho n.k yaliyofanywa na CCM kuwafikisha watu kwa maelfu Jangwani. Hizo ni dalili mabaya na ni tishio kubwa kwa CCM. Na ikaamuliwa kuwa iandaliwe mikakati ya kuwakatisha tamma wananchi wenye mapenzi na CHADEMA.
Mkakati :- Ilamuliwa kuwa upandikizwe mgogoro baina ya viongozi wa CHADEMA na mgombea wake Dr W. Slaa; na kuwachonganisha na wapiga debe wao akina Marando, Shibuda, Mpendazoe n.k kwa nia ya kuwakatisha tamaa wenye mapenzi na CHADEMA na wote wanaotarajia kuwapigia kura wagombea wa CHADEMA.
Iliamualiwa kwa kuwa wananchi wanampenda sana Dr W Slaa, zisambazwe habari kuwa aelewani na Mwenyekiti wake Ndg Freeman Mbowe kwa sababu Dr Slaa sio kutoka kabila la wachagga. I
likubaliwa kuwa taarifa hizo zianze kusambazwa wiki inayoanzia Jumatatu ya tarehe 30 Agosti 2010. Na tathmini ifanyike kujua mafanikio yake wakati zinatungwa mbinu mpya.
Iliamuliwa kuwa magazeti ya New Habari Corporation ikiwemo Mtanzania, Rai n.k yaanze kutumika kwa kazi hiyo wakati waandishi zaidi wa kufanya kzai hiyo wakitafutwa.
Ili wananchi wenye mapenzi mema na CHADEMA waweze kusadiki taarifa zitakazosambazwa ilikubaliwa kuwa magazeti yatakayotumika yaanze kwanza kwa kipindi kifupi kuandika habari njema kuhusu CHADEMA na wagombea wake; na baada ya mashabiki wake kuyaamini magazeti na vyombo hivyo vya habari ndipo kazi ya kuisamabaratisha CHADEMA ianze rasmi.
Ili kutekeleza mipango hiyo waandishi wa gazeti la Mtanzania walipatiwa maelekezo ya kurekebisha kichwa cha habari na maudhui ya habari za uzinduzi wa CHADEMA zilizochapishwa tarehe 29/8/2010, kwa lengo hilo.
Vyombo vya habari vya Serikali ya ikiwemo magazeti ya Daily News na Habari Leo na TBC na redio za TBC vilielekezwa kuanza mara moja kazi ya kuipamba CHADEMA kama chama na watu wa fujo mbele ya jamii makakati amabo unadaiwa kufanikiwa sana kuisambaratisha CUF mwaka 2005, wakati Mkuu wa chombo kimoja cha dola alipodai siku moja kabla ya upigaji kura wamekamata shehena ya majambia yenye rangi za bendera za CUF
c)Pingamzi la CHADEMA dhidi ya Jakaya Kikwete mkutano ulikubaliana kuwa kuaniza sasa idara ihakikishe kuwa inamgeuzia kibao Dr Slaa na kusambaza habari kwa wafanyakazi na umma kuwa DR Slaa anapinga wafanyakazi kuongezwa mishahara ndio maana CHADEMA inamuwekea pingamizi mgombe wa CCM Jakaya Kikwete kwa kitendo cha kuwaongezea mishahara watumishi wa umma katika kipindi hiki cha kampeni.
Dawati litaendelea kuwahabarisha!!!!!!![/QUOTE
Hao mashushu watamdanganya nani? Kila mfanyakazi alisikia mwenyewe kwa masikio yake mgombea Urais wa CCM Jakaya Kikwete akitamka kuwa "Serikaliyake haina uwezo wa kuongeza mishahara ya watumishi wa Serikali hata punje hata wakigoma kwa miaka minane"
Wafanyakazi pia wanatambua kuwa ni kwa kutoteteleka kwa TUCTA chini ya Mgaya, na kauli za mgombea Urais wa CHADEMA kutamka wazi wazi katika mikutano yake ya kutafuta wadhamin, kuwa "nazihitaji kura za wafanyakazi alizokataa mgombea wa CCM", na akachapisha fulana za kuwahamasisha wafanyakazi kutoa kura zao kwake ndio vilivyoitia adabu CCM na mgombea wao Mhe Jakaya Kikwete, kiasi cha kufikia hatua ya kuwapigia magoti wafanyakazi aliowabwatukia Mei 2010. Wafanyakazi wanatambua ni kutokana na kufikishwa hatua hiyo ndio maana mgombea Uraisa wa CCM Dk Jakaya Kikwete akakubali kutoa nyongeza ya mshahara ya kima cha chini kutoka Shs 104,000/= hadi Shs 235,000/= kwa mwezi katika mwezi Julai 2009.
Wafanyakazi wanatambua kabisa kama Mgaya na Dr Slaa wangekuwa waoga kwa vitisho alivyokuwa akitoa vya mgombea wa CCM Mhe Jakaya Kikwete, nyongeza hiyo isingepatikana asilani.
Kwa kuwa Serikali ya Jakaya Kikwete ilitoa nyongeza za mishahara na marupurupu kwa viongozi waandamizi wa Serikali wakiwemo wabunge, mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, majaji, wakuu wa vyombo vya dola na pia kulipa malimbikizo ya mishahara kulingana na ongezeko hilo kutokea tarehe maombi yao yailpowasilishwa Serikalini hadi tarehe ya kuanza kulipwa.
Wafanyakazi wanatambua kuwa bado wanaidai Serikali ya Jakaya Kikwete malimbikizo ya nyongeza ya mshahara kama ilivyofanyika kwa viongozi waaanamizi wa Serikali waliotajwa hapo juu. Hivyo basi kwa kuwa madai ya nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma yaliwasilishwa Serikalini na TUCTA kutokea mwaka 2006, mwaka mmoja baada ya wafanyakzi kumchagua Mhe Jakaya Kikwete kwa kishindo kushika wadhifa wa Urais mwaka 2005.
Wafanyakzi wanatambua kwa kuwa sasa imedhihirika wazi kuwa nyongeza hiyo ilikuwa ni haki yao. Ni wazi kuwa wanaidai Serikali waliyoichagua kwa kishindo mwaka 2005 ya Mhe Jakaya Kikwete malimbikizo ya mishahara kama yaliyotolewa kwa viongozi waandamizi wa Serikali. Malimbikizo hayao ni kama ifuatavyo, kima cha zamani Shs 104,000/=. Kima kipya kilichofikiwa baada ya TUCTA na CHADEMA kushikamana katika madai hayo katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 201o, Shs 235,000/=. Hivyo basi ongezeko hiklo ni Shs 235,000 -104,000= Shs 131,000/= kwa mwezi; zidisha kwa miezi 48 kutokea Juni 2006 TUCTA ilipowasilisha madai Serikalini hadi hadi Julai 2010, hatimaye Serikali ilipokuja kukubali kutoa nyongeza hiyo. Shs 131,000/= X miezi 48= Shs 6,288,000/=.
Kama wafanyakzi wa Tanzania wangekuwa wanatendewa haki namna hii na viongozi wanaowachagua kwa kishindo hivi kweli pangekuwa na mfanyakzi anayeshnda kununua kiwanja cha kujenga nyumba bora; kumlipi mtoto wake ada ya sekondari, kujijengea nyumba bora; kununua bati n.k.
Ni kutokana na viongozi tunaowachagua kwa kishindo kujikumbuka wenyewe ndio maana ni wao tu ndio wana magari mazuri, watoto wao wanasoma shule nzuri na hata nje ya nchi, wanajenga nyumba kama mahekaru n.k.
Wakati umefika wa kuamka na kuacha kudanganyika, acha kusikiliza blah blah wafanyakzi kahuna anytukumbka kwa kuwa wabunge tunaopeleka Dodoma waote wanatola kambi moja, tupeleke kutoka kambi ingine ili wakosoane badala ya kwenda kulindana ndio watakukumbuka kutupa haki zetu
Hivyo wafanyakazi wa kima cha chini walistahili kulipwa malimbikizo ya mishahara waliyostahili ya Shs 6,419,000/=. Hii ni haki yao na si ombi kwa kuwa katika kipindi kutokea kuwasilishwa kwa maombi ya nyongeza ya mshahara na TUCTA yaano mwaka 2006, Serikali hii hii iliyokaa kimya ilitoa nyongeza za mishahara kwa viongozi waandamizi wa Serikali.