Dola.. Dola... Dola taasisi za serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dola.. Dola... Dola taasisi za serikali

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mfamaji, Sep 22, 2010.

 1. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wakuu baada ya Bw. Kinana yule kinara wa kusimamia kampeni za chama fisadi CCM kuibuka na risiti feki inayoonyesha USD 15,000/= ????? walizolipia ndege ya mama aliyemua kumpigia mumewe kampeni arudi ikulu akaendelee kula bata , taasisi nyingi tu za serikali zimeachana na fedha halali ya Tanzania hata baada ya tamko la serikali kuhusu matumizi ya dola.

  AICC ni taasisi ya serikali. Ukienda kukodisha ukumbi wanakuambia dola , chakula..dola , computer,....dola maji ya kunywa ..dola , kalamu... dola. Dola ..dola.. dola ..hadi kupaki gari. Sasa sisi watanzania dola tunatoa wapi? Bora hao wageni wangelipa hizo dola lakini mbongo unamchaji dola ili iwe nini. Utashangaa hata pango la nyumba na ofisi wanacharge dola . Serikali hii vipi bana inaweka sheria inazivunja yenyewe ? Nyambaf.. Halafu eti kiongozi hicho kituo ni MCCM damu, na Mneki .

  Doctor Slaa come , and come faster to redeem this collapsing nation.
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hayo ndo matunda ya kuwa na viongozi wasio makini, hawataki hata kujifunza kutoka nchi jirani. Wanaachilia mambo tu yaende kienyeji-kienyeji na hilo unalozungumzia ndo sababu mojawapo inayosababisha mbomoko wa shililingi yetu kiasi kwamba hata Seriklai yenyeewe haiitaki pesa yake sasa tushangae nini shilingi kuporomoka?

  Nadhani ili kutunusuru na mbomoko na mporomoko wa shilingi ni vema tukaifuta na kuanza matumizi ya dola na dola nayo ikashabomoka ndipo tuchapishe shilingi mpya. Hili limefanikiwa Zimbabwe; hata Somalia dola haina thamani kwa kuwa ndo pesa inayotumika kama sarafu halali vivyo hivyo Sudan Kusini rafiki yangu mmoja wa huko aliniambia kuwa wao mshahara wao wanpokea katika US dola na si pesa ya Sudan.
   
Loading...