Mhe Rais, Waziri wa Fedha na Gavana wa BOT mbona kuna taasisi za Serikali zinataka malipo kwa dola hadi leo?

kalanga

Member
Feb 2, 2011
72
125
Mheshimiwa Rais, Waziri wa Fedha na Gavana wa BOT, wakati Rais anafungua tawi la bank ya CRDB makao makuu ya nchi Dodoma alisema ni marufuku kufanya malipo kwa hela ya Dola hapa nchini, lakini mbona kuna Taasisi za Serikali tena ambazo zipo chini ya Wizara ya fedha mpaka leo kuna malipo wanalazimisha kulipa kwa Dolla.

Mfano ni chuo cha IFM kuna kozi ya Masters ya IT and Management wanaitoa kwa kushirikiana na chuo cha India wanalazimisha wanafunzi walipie Ada kwa dolla badala ya shilingi.

Namuomba Waziri wa fedha aliangalie hili.
 
waubani

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
539
250
anajua matumizi ya dola yapo ndio maana ameagiza hivyoo. au hukumuelewa
 
JICHO TAI

JF-Expert Member
May 27, 2013
1,107
2,000
mkuu wewe umesoma hiyo kozi? ulipofanya application si ulikuwa unajua kuwa wanalipa kwa dola? sasa kilio hiki kimetoka wapi? na kwa ufahamu wangu hivi vyuo huwa wana MoU ambayo inavifanya vyuo hivi kulipa fee ya ushiriki kwa dola na gharama za kuwalipa hivyo fee wanaleta ankara za malipo ya idadi ya wanafunzi kwa dola. Sasa unataka nani aumie? unaposema chuo umeongelea serikali sasa unataka serikali ndo iingie hasara kwa kulipia upungufu utakaojitokeza? Unapochagua kozi chagua unayoimudu mkuu siyo kuja kulalamika
 
Gari Moshi

JF-Expert Member
Jan 29, 2013
560
500
Ukitaka kuagiza gari Japan au kungineko nako utaagiza kwa Tsh ? Unajua mifano mingine ni kama ya kukurupuka, hivi unaweza kufananisha Afrika ya kusini na Tanzania kwa chochote?Wao hata magari wanabuni na wanatengeneza aina karibu zote underlicence. Kilimo ndio kabisa tuende shule upya halafu tunajiringanisha nao. Basi linganisheni hadi mishahara. Hawaja fika pale walipo kwa miaka miwili au mitano ama hata hiyo kumi, " Ukiwa umeshapoteza uelekeo mwendokasi hauna maana tena "
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,296
2,000
Mheshimiwa Rais, Waziri wa Fedha na Gavana wa BOT, wakati Rais anafungua tawi la bank ya CRDB makao makuu ya nchi Dodoma alisema ni marufuku kufanya malipo kwa hela ya Dola hapa nchini, lakini mbona kuna Taasisi za Serikali tena ambazo zipo chini ya Wizara ya fedha mpaka leo kuna malipo wanalazimisha kulipa kwa Dolla.

Mfano ni chuo cha IFM kuna kozi ya Masters ya IT and Management wanaitoa kwa kushirikiana na chuo cha India wanalazimisha wanafunzi walipie Ada kwa dolla badala ya shilingi.

Namuomba Waziri wa fedha aliangalie hili.

Wewe waambie wakupe Invoice kwa shilingi watakupa tu. Ukilipa wao wananunua dola kukulipia huko India at a cost to you!
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
23,071
2,000
mkuu wewe umesoma hiyo kozi? ulipofanya application si ulikuwa unajua kuwa wanalipa kwa dola? sasa kilio hiki kimetoka wapi? na kwa ufahamu wangu hivi vyuo huwa wana MoU ambayo inavifanya vyuo hivi kulipa fee ya ushiriki kwa dola na gharama za kuwalipa hivyo fee wanaleta ankara za malipo ya idadi ya wanafunzi kwa dola. Sasa unataka nani aumie? unaposema chuo umeongelea serikali sasa unataka serikali ndo iingie hasara kwa kulipia upungufu utakaojitokeza? Unapochagua kozi chagua unayoimudu mkuu siyo kuja kulalamika
Wakati Rais wenu anatoa hili agizo hakujua haya?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom