Wizara na Taasisi za Serikali walipaswa wamwambie Rais mipango yao ya kisekta katika kututafutia dola

Michael Uledi

Senior Member
Mar 29, 2023
132
322
Tayari tumeingia kwenye tatizo kubwa la kiuchumi kama Nchi na tusipokuwa na maono makubwa ya jinsi ya kutoka hapo kwa kuwa na mipango ya muda mrefu na muda mfupi basi tumekwisha.

Wataalam wetu wanasema tatizo la ukosefu wa USD katika Uchumi wa Tanzania ni tatizo la Nchi nyingi za Afrika.Sijajua kama Nchi ya Misri au Nigeria pia kuna tatizo kama hilo.

Tatizo kubwa ambalo nadhani tunalo ni ukosefu wa balance kwa maana mizania kati ya mikopo tunayokopa kama Nchi dhidi ya Mitaji au Uwekezaji unaingia ndani ya Nchi kama FDI's + Nchi kukosa Makampuni ya Serikali ambayo yanafanya biashara Nje ya mipaka letu na kutuletea USD za kutosha kurudi Ndani ya Uchumi wetu.

Nimeandika several times jinsi gani Serikali inaweza "kumtongoza " Salim Bhakresa angalau tuwe na subsidiary kampuni ndani ya kampuni kubwa ya Bhakresa Group of Kampani ambayo ingetuwezesha kurudi na USD ndani ya Uchumi wetu.Tuna Uwekezaji wa Kampuni za Rostom Aziz Zambia na Kenya lakini je,tunawatumiaje wazalendo hawa angalau Serikali kubwa na hisa katika kampuni zao?

Sheria yetu ya Madini inasema Madini ambayo tunauza Nje ya Nchi kupitia Wafanyabishara wetu zile USD tunazopata zinapaswa kurudi Nchini!Nimemsikia Naibu Waziri Mkuu Mh Dotto Biteko,kabla ya kuondoka Wizara ya Madini, akiwakomalia Wafanyabishara wa Madini watekeleze sheria hiyo haraka.

Mh Antony Mavunde Waziri Mpya wa Madini anapaswa kunyonya uzoefu kwa Dotto Biteko kwa lengo la kusaidia kuongeza USD kwenye Uchumi wetu.Sasa nilitegemea kila Wizara na taasisi za Umma zituambie Mipango yao Mahususi katika kukusanya USD kupitia maeneo yao ni ipi?Wizara ya Madini,Biashara,Mipango na Uwekezaji, Uchukuzi,Ujenzi na zingine!Hawa wote wanapaswa wamwambie Mama Samia mipango yao ya muda mrefu katika kuleta USD zaidi kwenye Uchumi ni ipi?

Lakini pia kwa sasa option muhimu ni kusitisha baadhi ya vipande vya miradi ya SGR, Mfano vipande kutoka Dodoma Tabora, Kigoma na Mwanza!Kama tutaendelea kukopa kwa ajili ya vipande hivyo kwa sasa Nchi itaingia shimoni soon!Tunapaswa kujipanga upya na tumalizie vipande vya Dar Moro Dodoma basi!

Mchumi mmoja aliwahi kuonya kwamba kwa jinsi tunavyotekeleza miradi mingi kwa wakati mmoja, Tanzania inaweza kuingia kwenye balaa kubwa!Akihojiwa na Gazeti la Tanzania la The Citizen Mwaka 2020 au Mwaka 2021 kama sijakosea Mchumi huyo alisema Tanzania inaweza kuingia katika balaa kubwa kwa kutekeleza miradi mikubwa tena kwa mikopo ambayo yote tunailipa kwa USD.Ule haukuwa unabii bali ni suala la hesabu za Kiuchumi tu ambazo wataalam wetu hawazioni.

Hebu tukae upya na wawekezaji wa miradi yetu mikubwa hasa hawa wa Madini pale Nyanzaga,Kabanga Nickel,jamaa zetu wa Ngwala kutoka Australia na wengine watupe mpango wa "kufasttrack" miradi yao kwa lengo la kuanza kuzalisha sasa angalau waanze kutupa USD zao kabla ya Mwaka 2024 kwani bila hivyo tutakwama!

Hili suala la ukosefu wa USD kwenye Uchumi wa Tanzania kama tutakaa na kusubiria miujiza basi ipo siku linaweza kuwa na implications kubwa kwa Siasa za Tanzania maana USD ndio utumika kuagiza Mafuta,itatumika kuagiza vifaa vya Uchaguzi Mkuu ujao wa 2024 na 2025.USD hiyo hiyo inatumika "kuservice" Madeni yetu makubwa yote,USD hiyo hiyo inatumika katika safari za nje za Viongozi wa Nchi na Maofisa wa Serikali!

Tunapaswa kuja na akili kubwa kwani tayari tulishaingia kwenye "king" na hatuwezi kutoka kama tunawaza mawazo ya kwenda WB (Banki ya Dunia) na kuomba Mkopo wa 500 USD Milioni tena ambazo tutazilipa kwa USD hizo hizo tena na riba juu!Ni kama tumeyapeleka mbele Matatizo tu kwamba badala ya kutokea 2923 yaje yatokee Mwaka 2025 wakati wa Uchaguzi Mkuu! Implications za maamuzi hayo ni makubwa kwa sisi kama Chama dola katika Chaguzi!

Ebu tumsaidie Mh RAIS kuja na akili kubwa ya kuondoka hapa haraka!

+255692473785.
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia
Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.

tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.

Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.

Amina Tena Amina Amina Tena amina

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MWALIMU JK NYERERE
 
Kuna watu wakiona hii coment wanatamani kupasuka......
 
Tayari tumeingia kwenye tatizo kubwa la kiuchumi kama Nchi na tusipokuwa na maono makubwa ya jinsi ya kutoka hapo kwa kuwa na mipango ya muda mrefu na muda mfupi basi tumekwisha.

Wataalam wetu wanasema tatizo la ukosefu wa USD katika Uchumi wa Tanzania ni tatizo la Nchi nyingi za Afrika.Sijajua kama Nchi ya Misri au Nigeria pia kuna tatizo kama hilo.

Tatizo kubwa ambalo nadhani tunalo ni ukosefu wa balance kwa maana mizania kati ya mikopo tunayokopa kama Nchi dhidi ya Mitaji au Uwekezaji unaingia ndani ya Nchi kama FDI's + Nchi kukosa Makampuni ya Serikali ambayo yanafanya biashara Nje ya mipaka letu na kutuletea USD za kutosha kurudi Ndani ya Uchumi wetu.

Nimeandika several times jinsi gani Serikali inaweza "kumtongoza " Salim Bhakresa angalau tuwe na subsidiary kampuni ndani ya kampuni kubwa ya Bhakresa Group of Kampani ambayo ingetuwezesha kurudi na USD ndani ya Uchumi wetu.Tuna Uwekezaji wa Kampuni za Rostom Aziz Zambia na Kenya lakini je,tunawatumiaje wazalendo hawa angalau Serikali kubwa na hisa katika kampuni zao?

Sheria yetu ya Madini inasema Madini ambayo tunauza Nje ya Nchi kupitia Wafanyabishara wetu zile USD tunazopata zinapaswa kurudi Nchini!Nimemsikia Naibu Waziri Mkuu Mh Dotto Biteko,kabla ya kuondoka Wizara ya Madini, akiwakomalia Wafanyabishara wa Madini watekeleze sheria hiyo haraka.

Mh Antony Mavunde Waziri Mpya wa Madini anapaswa kunyonya uzoefu kwa Dotto Biteko kwa lengo la kusaidia kuongeza USD kwenye Uchumi wetu.Sasa nilitegemea kila Wizara na taasisi za Umma zituambie Mipango yao Mahususi katika kukusanya USD kupitia maeneo yao ni ipi?Wizara ya Madini,Biashara,Mipango na Uwekezaji, Uchukuzi,Ujenzi na zingine!Hawa wote wanapaswa wamwambie Mama Samia mipango yao ya muda mrefu katika kuleta USD zaidi kwenye Uchumi ni ipi?

Lakini pia kwa sasa option muhimu ni kusitisha baadhi ya vipande vya miradi ya SGR, Mfano vipande kutoka Dodoma Tabora, Kigoma na Mwanza!Kama tutaendelea kukopa kwa ajili ya vipande hivyo kwa sasa Nchi itaingia shimoni soon!Tunapaswa kujipanga upya na tumalizie vipande vya Dar Moro Dodoma basi!

Mchumi mmoja aliwahi kuonya kwamba kwa jinsi tunavyotekeleza miradi mingi kwa wakati mmoja, Tanzania inaweza kuingia kwenye balaa kubwa!Akihojiwa na Gazeti la Tanzania la The Citizen Mwaka 2020 au Mwaka 2021 kama sijakosea Mchumi huyo alisema Tanzania inaweza kuingia katika balaa kubwa kwa kutekeleza miradi mikubwa tena kwa mikopo ambayo yote tunailipa kwa USD.Ule haukuwa unabii bali ni suala la hesabu za Kiuchumi tu ambazo wataalam wetu hawazioni.

Hebu tukae upya na wawekezaji wa miradi yetu mikubwa hasa hawa wa Madini pale Nyanzaga,Kabanga Nickel,jamaa zetu wa Ngwala kutoka Australia na wengine watupe mpango wa "kufasttrack" miradi yao kwa lengo la kuanza kuzalisha sasa angalau waanze kutupa USD zao kabla ya Mwaka 2024 kwani bila hivyo tutakwama!

Hili suala la ukosefu wa USD kwenye Uchumi wa Tanzania kama tutakaa na kusubiria miujiza basi ipo siku linaweza kuwa na implications kubwa kwa Siasa za Tanzania maana USD ndio utumika kuagiza Mafuta,itatumika kuagiza vifaa vya Uchaguzi Mkuu ujao wa 2024 na 2025.USD hiyo hiyo inatumika "kuservice" Madeni yetu makubwa yote,USD hiyo hiyo inatumika katika safari za nje za Viongozi wa Nchi na Maofisa wa Serikali!

Tunapaswa kuja na akili kubwa kwani tayari tulishaingia kwenye "king" na hatuwezi kutoka kama tunawaza mawazo ya kwenda WB (Banki ya Dunia) na kuomba Mkopo wa 500 USD Milioni tena ambazo tutazilipa kwa USD hizo hizo tena na riba juu!Ni kama tumeyapeleka mbele Matatizo tu kwamba badala ya kutokea 2923 yaje yatokee Mwaka 2025 wakati wa Uchaguzi Mkuu! Implications za maamuzi hayo ni makubwa kwa sisi kama Chama dola katika Chaguzi!

Ebu tumsaidie Mh RAIS kuja na akili kubwa ya kuondoka hapa haraka!

+255692473785.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Waruhusu uraia pacha halafu waangalie dola zitakavyojaa mpaka wataziwekea vizingiti zisifurike.

Tutakuja kupiga dili kubwa za kujenga nchi halafu jioni tunaenda baa za Uswahilini na kutoa tip za $100 kwa mabaamedi mpaka tupigwe stop na Mwigulu Nchemba.
 
Back
Top Bottom