#COVID19 Dogo Janja ahojiwa Polisi, adaiwa kushawishi abiria wasipime COVID-19

Sasa hiyo inaleta tafsiri gani kwa huko alikopima na kuweza kupanda ndege ikiwa vipimo vilionesha hana ugonjwa halafu kumbe anao ugonjwa na ndege kapanda?
Unauliza tafasiri kwa jambo ambalo liko wazi!? kama kipimo hakijagundua kama unaumwa maana yake hutapewa matibabu stahiki haraka ikiwa daktari atazingatia majibu ya vipimo pekee, au kwa case ya covid-19 unaweza kuambukiza watu wengine......huwezi kuwaza jambo jepesi hivi halafu unataka ukashindane na wakenya kwenye soko la ajira? hao wakenya bora waje tu angalau watu waamke usingizini......
 
Unauliza tafasiri kwa jambo ambalo liko wazi!? kama kipimo hakijagundua kama unaumwa maana yake hutapewa matibabu stahiki haraka ikiwa daktari atazingatia majibu ya vipimo pekee, au kwa case ya covid-19 unaweza kuambukiza watu wengine......huwezi kuwaza jambo jepesi hivi halafu unataka ukashindane na wakenya kwenye soko la ajira? hao wakenya bora waje tu angalau watu waamke usingizini......
Nilichokuuliza na ulichojibu ni tofauti kabisa.

Ulisema kuwa unaweza kupima na kipimo kinaweza kisioneshe kama una ugonjwa na hali kiuhalisia unao ugonjwa na hiyo ndio sababu ya kupimwa tena, sasa ndio nikauliza kama Dogo janja alipima huko SA na kipimo kikaonesha hana corona lakini kiuhalisia anayo corona na akapanda ndege huku akiwa na corona ndio nikauliza nini tafsiri yake hapo?
 
Watu watatu akiwemo Abdulaziz Chende (26) maarufu Dogo Janja wamehojiwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege na kuachiwa wakituhumiwa kuwashawishi abiria wengine kukataa kufanya kipimo cha ugonjwa wa Covid-19.

Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Serikali, wenyeji wanaorejea na wageni kutoka nje wanatakiwa kuwasilisha kipimo kinachothibitisha hawana maambukizi ya Covid-19, huku wanaotoka nchi zenye maambukizi wakitakiwa kupimwa kwa kipimo maalum ambacho kitagharimu Dola 25 za Marekani, sawa na Sh57,500 kwa kila msafiri.

Inadaiwa kuwa Dongo Janja aliyekuwa akitokea Afrika Kusini alipinga kufanya kipimo hicho ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter msanii huyo wa Bongofleva ameandika, hii nchi Tanzania bado ina uonevu wa kishamba sana, sidhani kama mama yetu Rais Samia Suluhu anafahamu.. muda huu nafika uwanja wa ndege wa kimataifa nikitokea Afrika Kusini na Afrika Kusini huko nimepima na nina majibu ya corona lakini hawayataki wanataka hela kutupima upya.”

“Sasa ndugu zangu wa Tanzania mimi nina hela lakini sitoi hata kumi..., mniletee uji kituo nitakachokuwepo nikikosekana hewani shughulikeni na Polisi wa uwanja wa ndege.”

Chanzo: Mwananchi
juzi tu kasema ajivunii kuwa mtanzania
 
Sasa mbona wengine mnasema corona ya SA iliingia nchini na ndio mkawa mnahusisha na vifo vya watu na corona hiyo ya SA?

Jiwe na wapiga pambio ndio walikuwa wanasema hakuna korona ila background ilikuwa inatafuna watu.
 
Inaenda kwa wimbi wewe,wimbi la kwanza lilimuondoa rwakatale ,wimbi la pili limemuondoa kubwa la maadui,wimbi la tatu litaanza tena mwishoni mwa november 2021 kama hatutapata chanjo mapema.
Kwahiyo hivi tulivyojiachia hakuna athari hadi lije wimbi?
 
Back
Top Bottom