#COVID19 Dogo Janja ahojiwa Polisi, adaiwa kushawishi abiria wasipime COVID-19

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Watu watatu akiwemo Abdulaziz Chende (26) maarufu Dogo Janja wamehojiwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege na kuachiwa wakituhumiwa kuwashawishi abiria wengine kukataa kufanya kipimo cha ugonjwa wa Covid-19.

Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Serikali, wenyeji wanaorejea na wageni kutoka nje wanatakiwa kuwasilisha kipimo kinachothibitisha hawana maambukizi ya Covid-19, huku wanaotoka nchi zenye maambukizi wakitakiwa kupimwa kwa kipimo maalum ambacho kitagharimu Dola 25 za Marekani, sawa na Sh57,500 kwa kila msafiri.

Inadaiwa kuwa Dongo Janja aliyekuwa akitokea Afrika Kusini alipinga kufanya kipimo hicho ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter msanii huyo wa Bongofleva ameandika, hii nchi Tanzania bado ina uonevu wa kishamba sana, sidhani kama mama yetu Rais Samia Suluhu anafahamu.. muda huu nafika uwanja wa ndege wa kimataifa nikitokea Afrika Kusini na Afrika Kusini huko nimepima na nina majibu ya corona lakini hawayataki wanataka hela kutupima upya.”

“Sasa ndugu zangu wa Tanzania mimi nina hela lakini sitoi hata kumi..., mniletee uji kituo nitakachokuwepo nikikosekana hewani shughulikeni na Polisi wa uwanja wa ndege.”

Chanzo: Mwananchi
 
Dar es Salaam. Watu watatu akiwemo Abdulaziz Chende (26) maarufu Dogo Janja wamehojiwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege na kuachiwa wakituhumiwa kuwashawishi abiria wengine kukataa kufanya kipimo cha ugonjwa wa Covid-19.

Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Serikali, wenyeji wanaorejea na wageni kutoka nje wanatakiwa kuwasilisha kipimo kinachothibitisha hawana maambukizi ya Covid-19, huku wanaotoka nchi zenye maambukizi wakitakiwa kupimwa kwa kipimo maalum ambacho kitagharimu Dola 25 za Marekani, sawa na Sh57,500 kwa kila msafiri.


Mwananchi

1.PNG
 
Kama kipimo alichopima SA kimeshapita masaa 72 hapo hana namna lazima na huku apimwe (Kwa mujibu wa maelekezo mapya ya wizara ya afya), vinginevyo yupo sahihi kuhoji kupimwa tena.
Rapid test ni lazima kwa SA kwa sababu ni nchi ambayo ina variant wa covid-19.

Yaani kuna SA-variant. Lakini hakuna Rwandan-variant of covid.

Hizi nchi mbili kwa mfano, zinakuwa treated tofauti.
 
Kama alishapima South Africa haina haja kupima tena. Huo ni uonevu na unyang'anyi.

Swali la kizushi hivi dogo Janja umri wake umeganda tu? Huwa haongezeki miaka?
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom