BRICS bado iko imara licha ya changamoto ya COVID-19 na mgogoro wa Ukraine

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Caroline Nassoro

VCG111355275804.jpg


Janga la COVID-19 limekuwa na athari kubwa kwa uchumi wa nchi mbalimbali duniani, kwani katika kudhibiti maambukizi, hatua kadhaa za lazima zilichukuliwa, ikiwemo kufunga shughuli za biashara na kijamii, jambo lilivuruga mwelekeo wa uchumi wa nchi mbalimbali na dunia kwa ujumla.

Mashirika mengi ya kimataifa na kikanda, na taasisi za kimataifa pia zimeguswa na athari za janga la COVID-19. Athari hizo zimeongezeka zaidi kutokana na operesheni maalum ya kijeshi inayofanywa na Russia dhidi ya Ukraine.

Licha ya changamoto hizo, Tume ya Biashara ya kundi la BRICS linalojumuisha nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, ilifanya Mkutano wa Biashara Juni 8.

Miaka 16 baada ya kuanzishwa kwake, dunia inakabiliwa na changamoto kubwa ya janga la COVID-19 na vita ya Ukraine, na kufanya baadhi ya watu kujiuliza kama kundi hili bado lina ushawishi mkubwa kama dunia inyoibuka kiuchumi. Jibu ni kwamba BEICS bado ina ushawishi mkubwa kama kundi linaloibuka kiuchumi.

Hivi sasa dunia bado inakabiliwa na janga la COVID-19 na athari zake kiuchumi, kijamii, na kwa maisha ya watu, na pia janga hilo limeleta kikwazo kikubwa katika Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa.

Lakini katikati ya changamoto hiyo, moja ya nchi zinazounda kundi hilo, China, imefanikiwa kuondokana na umasikini uliokithiri kwa pande zote, ikiwa ni miaka karibu 9 kabla ya muda uliopangwa katika Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030.

Pia katikati ya janga la COVID-19, kundi la BRICS limezindua Kituo cha Utafiti na Maendeleo ya Chanjo, pendekezo lililotolewa na China na Afrika Kusini. Kupitia kituo hicho, kampuni ya madawa ya China, Sinovac, imeingia ubia na kampuni ya Numolux ya Afrika Kusini na kutengeneza chanjo za COVID-19, na chanjo hizo kwa watoto kwa sasa zinaingia kipindi cha tatu cha majaribio ya kliniki.

Tukigeukia mgogoro unaoendelea sasa nchini Ukraine, vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Russia na baadhi ya nchi za Magharibi vimeongeza haja ya nchi zinazoendelea kusaidiana wao kwa wao. Licha ya nchi za Magharibi kuzitaka nchi rafiki na Russia kutoiunga mkono nchi hiyo katika operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine, jambo hilo limeshindwa.

Nchi za BRICS zimeweka wazi msimamo wake juu ya hatua hiyo ya Russia. India imeweka wazi msimamo wake wa kuendelea kununua mafuta kutoka Russia, na imeongeza kiasi cha mafuta inayonunua kutoka nchi hiyo.

Wakati huohuo, Brazil na Russia zimeendelea kuwa na uhusiano mzuri wa pande mbili na katika ngazi ya BRICS, na pande hizo zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika sekta mbalimbali, hususan ndani ya mfumo wa BRICS.
 
Back
Top Bottom