Does the Torah Pentateuch or Monoteuch (Je Torati ni vitabu vitano au kitabu kimoja?)

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,602
17,746
Pengine wengine wanaweza kujiuliza nini maana ya Pentateuch. Pentateuch au "Πεντάτευχος" limetokana na lugha ya kiyunani yaani kigiriki linalomaanisha "penta" (πεντά au πεντά) yaani tano na "teuch" (τευχος) mafundisho au vitabu ama kwa lugha iliyozoeleka ni vitabu vitano vyaTorah au torati.. na vinanasibiwa kuandikwa na musa Mwenyewe vilivyo na maagizo na sheria kwa Wana wa israel Kipindi wakitoka katika uhamishoni misri ,kwa hyo kuwa nami Katika Uzi ili kufanikisha uchambuzi kuwa "Torat ni Pentateuch au monoteuch"

Vitabu hivi vilivyopo sasa maarufu kama vitabu vitano vya Musa"Pentateuch" (Mwanzo,Kutoka,Walawi,Hesabu,Kumbukumbu la torati) vinanasibiwa kuandikwa na Musa kama wakristo na wayahudi wengi wanavyoamini hivyo.
Bila shaka mimi sio mpingaji kwamba torari imeandikwa na musa la hasha! Baada ya kujadili tutaamua hvyo kama kitabu kimoja cha torati ama vitabu vitano vya torati

HALI ILIVYO KWA SASA KUHUSU TORATI KWA IBRAHIMIC FAITH (IBRAHIMIC RELIGION ZOTE)

Wakristo wote na baadhi ya Madhehebu ya orthodox (Christian orthodox)

Wanaamini Torati ni mkusanyo wa vitabu vitano vya kwanza vya Biblia ya Kiebrania, yaani vitabu vya Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati, Kwa maana hiyo, Torati Maana nyingine huitwa Pentateuki au Vitabu Vitano vya Musa.Na wote wanaamini kuwa Torati imeandikwa na Musa na ilikuwa ikitunzwa vizazi mpaka vizazi na wafalme mpaka wafalme kupitia kwa walawi na makuhani.
Kumbukumbukl la torati 31:9

Waisraeli na wayahudi (Jews and judaism)

Wao wako Tofauti kidogo, kwani Kwao kuna torati za aina mbili za Torati ya kwanza huitwa Torati iliyo katika maandishi yaani "Maandiko ya torati" (תּוֹרָה שֶׁבִּכְתָב‎, Tōrā šebbīḵṯāv) Hii ndo ile iliyo na vitabu vitano, na aina ya pili ni Torati iliyo katika Hadithi na inayorithishwa kizazi mpaka kizazi "Torati ya Mdomo" (תּוֹרָה שֶׁבְּעַל־פֶּה, Tōrā šebbəʿal-pe)

Kulingana na Rabbinic Judaism, Torati ya Mdomo au Sheria ya Simulizi ( תוֹרָה שֶׁבְּעַל־פֶּה‎,Tōrā šebbəʿal-pe) ni zile sheria , amri, na tafsiri za kisheria ambazo hazikuandikwa katika Vitabu Vitano vya Musa, Vilivyoandikwa.
Torati (תּוֹרָה שֶׁבִּכְתָב‎, Tōrā šebbīḵṯāv, '"Sheria Iliyoandikwa"'), lakini hata hivyo inachukuliwa na Wayahudi wa Kiorthodoksi kama maagizo na kutolewa kwa wakati mmoja.
Kanuni hii ya jumla ya maadili ya Kiyahudi inajumlisha msururu mkubwa wa mila, desturi za ibada, Mahusiano baina ya watu na Mungu wao, kuanzia sheria za vyakula hadi Sabato na utunzaji wa sikukuu hadi mahusiano ya ndoa, desturi za kilimo, na madai ya raia na uharibifu. Kulingana na mapokeo ya Kiyahudi ya kiRabi,
Torati ya Simulizi ilipitishwa kwa Masimulizi ya Hadithi sahihi kwa mnyororo (chain) usiokatika kutoka kizazi hadi kizazi hadi yaliyomo hatimaye yaliwekwa katika mandishi kufuatia uharibifu wa Hekalu la Pili katika 70 CE,
wakati Huo ustaarabu wa Kiyahudi ulikabiliwa na tishio na kusongwa kila mahali kwa sababu ya mtawanyiko wa watu wa Kiyahudi ,Hazina kuu za Torati ya Simulizi ni Mishnah, iliyokusanywa kati ya 200-220 CE na Rabbi Yehudah haNasi, na Gemara,
mfululizo wa maelezo na mijadala inayohusu Mishnah,
ambayo kwa pamoja inaunda Talmud.
Talmud ni maandishi makuu ya Dini ya Kiyahudi Talmud ina matoleo Mawili yaliyopo,
La kwanza lilitolewa Galilaya c. 300–350 CE (The Jerusalem Talmud),
na la pili, Talmud pana zaidi iliyokusanywa katika Babylonia c. 450–500 CE (Talmud ya Babeli).
Imani kwamba sehemu za Torati ya Hadithi au Mdomo zilipitishwa kwa mdomo kutoka kwa Mungu hadi kwa Musa kwenye Mlima Sinai wakati wa Kutoka Misri ni kanuni ya msingi ya imani ya Uyahudi wa Orthodoksi, na ilitambuliwa kama mojawapo ya Kanuni Kumi na Tatu za Imani na Maimonides. Hata hivyo, si matawi yote ya Dini ya Kiyahudi ya Marabi yanayokubali uthibitisho halisi wa Sinaiti wa Torati ya Simulizi, ikiitambulisha kama matokeo ya mchakato wa kihistoria wa kuendelea kufasiri.

WAISLAMU
Waislamu kama walivyo dini zingine zote zinazojulikana kama Ibrahimic Faith au Ibrahimic Religions ,Nao wanaamini kuwa torati iliandikwa na Musa kwa Maagizo aliyokuwa Akipewa na Mungu .
Hakika tuliiteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru. Na Mitume wanyenyekevu waliwahukumu Mayahudi kwa hayo, na Walio wajuzi na wanavyuoni kwa yale waliyokabidhiwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nao walikuwa mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi, wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani ndogo [yaani faida ya kidunia]. Na wasiohukumu kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri. — Quran 5:44
Kwa hiyo huo ni ushahidi kuwa torati iliandikwa na Ipo kwa madhumuni maalumu na ushhidi kuwa Imeandikwa na musa tunaupata katika aya isemayo

Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukamweka pamoja naye nduguye, Harun, kuwa waziri - (Quran 25:35)

Ssa kwa kuwa tumeshaona wote wanaamini uwepo wa torati ama torah turudi kwenye swali Letu halisi lisemalo
torati iliandikwa kama kitabu kimoja au vitano vilivyopo?

Ukisoma katika vitabu vya kibiblia na quran Utaona kuwa torati ama torah kinatajwa kama kutabu kimoja tupitie tuone ilivyoonekana kwenye baadhi ya vitabu. tuanze kuchunguza
"Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu" Malaki 4:4, (Hii ndo ntaichambua kidgo kuliko vitabu vingine maana maneno hayatoshi kuchambua zote)

Kwa kihebrania inaandikwa
זכרו תורת משה
עבדי אשר צויתי
אותו בחרב
על־כל־ישראל חקים
ומשפטים׃

Neno תורת משה kama lilivyo Ni torati ya Musa na תורת ipo katika umoja hivyo inaonyesha ni Moja na sio nyingi kama ingekuwa katika wingi ingeandikwa הלכות משה yaani torati za musa na neno הלכות linakuwa katika wingi hii ni hivyo hivyo katika aya zote hapa chini kama zilivyoandikwa
Yohana 1:17,Yoshua 8:31, Nehemia 8:1,Yoshua 1:8 ,1 wafalme 2:3;)
Na aya yote hizo torati inatajwaa kama kitabu kimoja kilichoandikwa na Musa kwa kuamrishwa na mungu (Kutoka 34:27),
Soma pia katika qura'an 17:2 ,Qur'An 25:35.

SASA ILIKUAJE TORATI KUTOKA KWENYE MONOTEUCH KWENDA PENTATEUCH (Kitabu kimoja mpaka vitabu vitano)

Zamani torati ilikuwa Kitabu kimoja kilichoandikwa na Musa na hakikuwa na sehemu Tano kama tunavyofahamu leo ila torati imepitia misukosuko mingi kuandikwa kwake ,Zikaja enzi za Waamuzi,Zikaja enzi za Ufalme Israel mpaka kuvunjika kwa falme ya Israel kuwa falme mbili nazo nu uyahudi (Taifa la Yuda) na israel au ilikuwa ikiitwa samalia (Taifa la Samalia) jina jingine wayahudi au watu wa uyahudi au taifa la yuda walipelekwa uhamishoni kwa awamu tatu: 597 KK, 586 KK na 582 KK. Ingawa wengine tena walikimbilia Misri, baadhi waliweza kubaki nchini Yuda. Uwezekano wa kurudi ulipatikana tena Babuloni yenyewe ilipotekwa na Koreshi Mkuu, mfalme wa Uajemi (539 KK). Huyo aliwaruhusu warudi kwao na kujenga upya hekalu la Yerusalemu. Hata hivyo waliokubali hawakuwa wengi, nao walirudi vilevile kwa awamu. Kati yao kulikuwa na asilimia ya makuhani na Walawi kuliko kawaida, kutokana na uhusiano wao na ibada hekaluni. Wayahudi wengine waliona maisha huko Mesopotamia yamekuwa na maendeleo kuliko yale ya awali nchini kwao." Kama inavyoandikwa na Peter R. Ackroyd, "Exile and Restoration: A Study of Hebrew Thought of the Sixth Century B.C." (SCM Press, 1968)"

Baada ya kurudi tena yerusalem wayahudi hawakuwa tena Na torati kwani the Ark of convenants yaani sanduku la agano ambalo ndani kwake lilikuwa na torati na maamrisho mengine ya mungu (inasemekana baada ya utawala wa babel mwaka
597KK na 586Kk lilipotea haikuonekana tangu hapo soma kitabu za Ezra na Kitabu cha nehemia nivitabu vinavyosadikiwa kuandikwa miaka ya 443KK mpaka 433KK vinavyoelezea kuhusu nehemia na kujengwa kwa YERUSALEMU.
Ndipo Mfalme Astashasta kumuambia Ezra kuandika tena torati ili iwe mwongozo kwa watu wote kwani ezra alikuwa ni nabii mwenye kumbukumbu kubwa sana aliweza kuikariri torati yote soma maana ni ndefu sana siwezi kuiandika hapaa yote (Ezra 7:1-14)
Kufuatana na maombi ya watu, Ezra akisaidiwa na baadhi ya Walawi, alisoma Torati na kuieleza kwa watu waliokutanika. Inaonekana kwamba sheria hiyo ilikuwa haijasomwa kwa muda mrefu sana takribani zaidi ya miaka 100, kwa hiyo watu walisikiliza kwa uangalifu sana (ezra 8:1-8). Walipogundua jinsi maisha yao yalivyokuwa mbali na sheria hiyo, walijaa huzuni hata Nehemia aliogopa kwamba mambo aliyoyakusudia kuwa sikukuu ya furaha na karamu kubwa yatageuka kuwa wakati wa huzuni na maombolezo (ezra 9-12).
Siku mbili baada ya kumaliza sikukuu ya Vibanda (iliyokuwa tangu siku ya 15 hadi ya 22 ya mwezi ule, taz. 8:18; Law 23:34), watu walikutana tena kwa kusomewa sheria. Wakati huo baada ya kusomewa, ulifuata wakati wa kukiri dhambi na kumwabudu Mungu.

Mambo muhimu zaidi yaliyotajwa katika maandiko hayo yalihusu ndoa za mchanganyiko (30, taz. Kut 34:15-16); siku ya Sabato na mwaka wa Sabato (31, taz. Kut20:8-10; 23:10-ll; Kum 15:1-2); kodi ya hekalu (32, taz. Kut 30:11-16); mahitaji kwa ajili ya hekalu na huduma zake (33-34); sadaka za malimbuko ya nafaka na wazaliwa wa kwanza wa wanyama (35-36, taz. Hes 18:13-18) na zaka (yaani utoaji wa sehemu ya kumi ya mapato, 37-39; taz. Hes 18:21-28).


BAADAYE TORATI ILITUNZWA NA KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA MAARIFA YA UANDISHI WATU WENGI WALIANZA KUANDIKA TORATI KADRI YA UWEZO WAO.

Anaelezea Athanasius 1 Of alexandria mmoja wa baba wa kwanza wa imani ya kikistro mnamo mwaka 367 A.D kulikuwa na Torati nyingi sana na zenye maandishi tofauti tofauti Na zinazojinasibisha na Musa Amaa zimeandikwa na Musa walizifanyia uchambuzi na kuondoa zote zile ambazo ni pseoudepidegrapha apokrifa na zingine kubaki na zile zilizokuwa ni Canonical na ndio tulizonazo leo hii,(Zingine ambazo zipo njee kama Jubilee,Adam and eve na zingine) hazikukidhi vigezo vya canon

LAKINI WANATHEOLOGIA WANASEMAJE KUHUSU HII

wanatheologia elimu ya sini wamegawa Elimu ya uchunguzi Katika sehemu mbili

HISTORICAL THEORY
na
DOCUMENTARY HYPOTHESIS (Japo wanasema kwa sasa wameshahakiki na wanaita (DOCCUMENTARY FACTS)

HISTORICAL REVIEW THEORY

ni kuichunguza History ya maeneo ikiwemo majina ya mahali na majina ya miji kujua hasa Ni lini imeandikwa kwani miji na majina ya miji yalitofautia katika nyakati tofauti tofauti na hii imesaidia sana kujua baadhi vitu na hasa kugundulika kwa HYPOTHESIS IITWAYO Doccumentary hypothesis (HII NI NDEFU SANA NTATAFUTA UZI WAKE)

DOCCUMENTARY HYPOTHESIS kwa sasa INAITWA DOCCUMENTARY FACTS
Ni maelezo kuwa torati ya sasa hivi imejengwa au kutolewa katika Vyanzo vinne tofauti ambavyo wao wamevitaja kama JEPD (Yaani Jahwist sources,Elohist sources,Priestly sources na Deuteronomist source)
Kwamba kulingana na majina J ni ambayo imetaja jina ya yhwe ama jwhova ni kitabu cha torati tofauti na kilichotaja E ama elohimh na ni tofauti na kilichotoka kwa walawi na ni tofauti kilichotoka kwenye kumbukumbu la torati ) na wanasema hizo sources zinajitemea na ni zinatofautiana na zama pia kilichotokea ni Kwnye kuchanganya vitabu wakakuta wanazichanganya sources zote kwa pamoja bila kujali kama ni kitu kimoja....
Kwa mfano tutafute wazee wanne wote tuwaambie wamuelezee nyerere mmoja atamwita "kambarage" Na tukimchukua mwingine atasema Nyerere na kuna mwingine atamwita simba na kuna mwingine atamwita mjukuu wa burito na kuna mwingine atamwita julius ....ikatokea baada ya kuchukua ushaidi huo wa nyerere tukauweka maktaba ikapita miaka mingi na wakaja watu wanaotafuta simulizi za nyerere na aakadhani kuwa simulizi hizo ni za mtu mmoja na wakazichaganya bila kujali kwamba matukio yanaweza kujirudia au lah......hii pia ntaimalizia kwenye uzi mwingine

Asanteni
 
Hongera kwa bandiko bora kabisa.

Ila haya mambo yanachanganya kwa kweli, kikubwa Mungu atujalie kuepuka moto wa Jehanamu.
Kuna vitu vinachanganya na wakati mwingine imani tunazojengewa zinatunyima wigo wa kuwa na tafakuri tunduizi nje ya maandiko, ndio maana ktk mengi hatuna maarifa mtambuka.
Mkuu ni kweli kabisa, Unawza ukaambiwa kuchunguza sana ni dhambi hawataki kabisa uchunguze asili ya vitu sana sana kama imani unaambiwa na wakubwa hutakiwi kuna na shaka nayo kwa sababu wanajua ukichunguza sana utajua vibgi sana
 
Back
Top Bottom