Mi naona kigezo cha umri kina umuhimu wake sana katika mahusiano hasa ya ndoa; miaka kumi inaweza kuonekana sio kitu kwa sasa maana mpo kwenye 30s na 20s ila mkifika kwenye 50s na 40s huko ndipo utaweza kuiona tofauti kwa wazi zaidi. Siwezi kukupa data kamili za takwimu mbalimbali kwa sasa ila in general kuna mambo mengi ya kuzingatia kama kutofautiana kasi ya kumature, when are in your primes, focused n.k. Ni vizuri sana kama tofauti inakuwepo basi ni miaka michache tu. Siku za usoni utaanza kuona issues za energy, kulea watoto, stability nk. Ni kweli wapo wengi waliooana bila kuzingatia tofauti ya umri, na ni kweli changamoto na matatizo yapo, ila hiyo isimaanishe na wewe ufuate mkondo huohuo, kama kuna namna ya kuepuka ni vema kuitumia! Lakini sometimes pia unalazimika kuignore baadhi ya factors kama unapata mtu anayekufaa, basi suala la umri hulizingatii sana. Go for him, but be prepared for the challenges that might arise. Huna uhakika kama ukimpata wa umri unaofaa atakuwa anafaa kwa vigezo vingine pia, chemsha akili yako! Remember if you do not get what you think you want, then take what you get! Nakutakia kila la heri na Mungu akusaidie.