Dodoma: Rais Magufuli aagiza kuchunguzwa kwa Airtel kama ni mali ya TTCL! Wapotoshaji wa Takwimu wachukuliwe hatua kali

Hili limedhihirika kila siku katika hotuba zake na nahisi ana ID JF. Muda huu anahutubia katika uzinduzi wa jengo la ofisi za NBS yaani National Beaural for Statistics ambapo ameelezea msemo wa vyuma kukaza kwamba ameona mchoro unaotembea kwenye mitandao ya kijamii ukionyesha vyuma vikizunguka huku oil ikiwa unamiminiwa kulainisha vyuma hivyo.

Rais ametolea mifano mingi inayotembea kwenye mitandao ya kijamii kitendo kinachoonyesha huyu ni mwanamitandao mwenzetu na narudia tena huenda ana ID yake hapa JF.

NAOMBA MODS WA JF WAWASILIANE NAYE ILI WAMSAIDIE RAIS KUWA NA VERIFIED ID HAPA JF ILI TUFURAHIE UWEPO WAKE MUBASHARA......
NAWASILISHA.
Akiwa verified haita msaidia sana nadhan hivyo hivyo ilivyo ni sahihi zaid , akisha kuwa verified kuna mambo yatampita.
 
Leo karibu hotuba yote niliona amekomaa na hizi habari za vyuma sijui nani kamkwaza mzee baba
Nami pia.Kwa mara ya kwanza leo yuko composed,amejenga hoja vizuri mno kuhusu kukua uchumi ingawa kama kawaida alichomekea na vitisho juu (tradition dies hard).
Ni lazima Watanzania tupime upepo,whether sheria ya takwimu ilianzishwa kwa nia mbaya au la,ni muhimu tuifuate kwa sasa wakati tunatafuta njia mbadala ya kuirekebisha.
La sivyo,wafungwa kweli!!
 
Jengo ambalo lingeweza kuzinduliwa na DC,delegation iko wapi??Hachoki kuonekana kwenye TV kila siku.Kweli Zitto hakukosea!!!
Mshaanza na issue za uzinduzi. Hamkosi cha kuzungumza. Watanganyika Hatuna jema.
 
Hili limedhihirika kila siku katika hotuba zake na nahisi ana ID JF. Muda huu anahutubia katika uzinduzi wa jengo la ofisi za NBS yaani National Beaural for Statistics ambapo ameelezea msemo wa vyuma kukaza kwamba ameona mchoro unaotembea kwenye mitandao ya kijamii ukionyesha vyuma vikizunguka huku oil ikiwa unamiminiwa kulainisha vyuma hivyo.

Rais ametolea mifano mingi inayotembea kwenye mitandao ya kijamii kitendo kinachoonyesha huyu ni mwanamitandao mwenzetu na narudia tena huenda ana ID yake hapa JF.

NAOMBA MODS WA JF WAWASILIANE NAYE ILI WAMSAIDIE RAIS KUWA NA VERIFIED ID HAPA JF ILI TUFURAHIE UWEPO WAKE MUBASHARA......
NAWASILISHA.
Sio lazima. Atakuwa whatsapp.
 
Hapo pa vyuma kukaza hapo ni kweli kwa hali ya sasa inahtaji kufanya kaz kwa bidii sana.

Nashauri serikali iongeze jitihada ktk uwekezaji wa kilimo badala ya viwanda.

Kuhusu kukamata watu wanaosema vyuma vimekaza, hii hapana.. Itakuwa alikuwa ananogesha.
 
Hili limedhihirika kila siku katika hotuba zake na nahisi ana ID JF. Muda huu anahutubia katika uzinduzi wa jengo la ofisi za NBS yaani National Beaural for Statistics ambapo ameelezea msemo wa vyuma kukaza kwamba ameona mchoro unaotembea kwenye mitandao ya kijamii ukionyesha vyuma vikizunguka huku oil ikiwa unamiminiwa kulainisha vyuma hivyo.

Rais ametolea mifano mingi inayotembea kwenye mitandao ya kijamii kitendo kinachoonyesha huyu ni mwanamitandao mwenzetu na narudia tena huenda ana ID yake hapa JF.

NAOMBA MODS WA JF WAWASILIANE NAYE ILI WAMSAIDIE RAIS KUWA NA VERIFIED ID HAPA JF ILI TUFURAHIE UWEPO WAKE MUBASHARA......
NAWASILISHA.
Haha anasoma na kupitia kimya kimya
 
Kwa maneno ya mkuu unaweza kutafsiri kwamba Nchi hii kila mtu alikua mwizi! Kama hata mama ntilie wanalalamika vyuma kukaza sijui mama ntilie nao walikua majizi wa nini,,

Tafsiri yake yale MAJIZI yalikuwa yanakula kwa Mama Ntilie:):):)
 
Mwambieni Ndugai aitishe bunge la Dharura ili mpitishe sheria au kiongezwe kifungu kwenye Penal code cha mtu anayelalamikia ugumu Wa maisha kushtakiwa.
.Hata mie nilitaka kusema hivo hivooooo...., yani huku tunakoelekea sasa ni Mungu tu anayejua
 
Wezi lazima walalamike, hilo lipo wazi. Sote tunajua hilo.
Na wewe ulikuwa unamuibia nani? mbona unamaisha duni tu na hata kibarua huna unashinda JF full time upate posho ya buku 7? nashangaa majobless ndio mashabiki wa mtu anayesababisha mnakosa vibaruwa vya kujikimu.
 
Wadau tujadili hoja za msingi tafadhali
1. Umiliki wenye utata wa airtel tanzania
2. Sheria ya utoaji takwimu nchini
Hebu tujikite kwenye hizo hoja mbili hapo juu tafadhali ndipo penye umuhimu mkubwa zaidi na tusitoke nje ya mada.
 
*YALIYOSEMWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JOHN POMBE MAGUFULI KWENYE HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU ILIYOFANYIKA MAKULU, DODOMA LEO JUMATANO DISEMBA 20, 2017*

“Ninawaomba Watanzania mpuuze uzushi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba uhumi umeshuka. Tumieni takwimu zilizokusanywa na ofisi ya takwimu ya taifa.” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Dar es Salaam sasa hivi Nyumba zimeanza kushuka bei, walikuwa wanalipisha kwa Dola lakini leo nyumba hizo wamezikimbia. Tusitake kutangaza kuwa vyuma vimekaza kwa nia mbaya, watu hao muwapuuze. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Ukuaji wa uchumi wetu unaendelea vizuri. Nusu ya mwaka huu nchi yetu imeongoza katika kanda ya afrika mashariki kwa kukua vizuri. Mfumuko wa bei mpaka mwezi November ulifikia asilimia nne. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Tulipokuwa tunapata uhuru tuliambiwa kwamba umri wa mwisho wa kuishi ni miaka 41, kwa sasa tunaambiwa ni miaka 60, na mimi bado sijafikisha miaka 60, bado ninasiku za kuishi. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani takwimu ni muhimu. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

"Suala la takwimu ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi yoyote. Hasa takwimu zikiwa sahihi. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Ninasikia watu wanalalamika kwamba vyuma vimekaza. Ninaomba niwahakikishie kwamba vitakaza kweli kweli. Tutalegeza vyuma kwa wale ambao wako radhi kufanya kazi kwa juhudi. Tunachukua hizi hatua ili kutengeneza maisha mazuri ya Watanzania. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Wale wanaolalamika kubanwa watabanwa kwelikweli. Tutabana vichwa, tutabana miguu, tutabana matumbo, tutabana kila kitu. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Wale waliokuwa wamezoea hela za burebure zitaendelea kubana, lakini kwa wale wanaochapa kazi vyuma haviwezi vikabana, vinaachia kwa sababu wameamua kutumia fursa za kufanya kazi. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Tunafanya mazungumzo na nchi ya Israel kuhakikisha kwamba tunanzisha kitengo cha huduma kwa wagojwa mahutui katika hospitali ya Benjamin Mkapa hapa Dodoma. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Serikali inaendelea kuhakikisha kwamba kasi ya ukuaji wa uchumi inaenda sambamba na ukuaji wa hali ya uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Ninaomba kutoa onyo hasa kwa wale ambao wanakuja na takwimu zao za mifukoni. Mamlaka husika mtumie sheria zilizopo kuwabana wale ambao wanataka kuwapotosha Watanzania kwa takwimu zao za uongo. Ukukosea kutoa takwimu, umeichafua nchi. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

"Ukikosea kutoa takwimu, umeichafua nchi. Ndiyo maana kuna watu waliobobea katika masuala ya takwimu. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

"Niwaombe Watanzania, ukitaka takwimu yoyote nenda kwa wataalamu wa takwimu. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

"Nawaonya wale wote wenye kutoa takwimu za uongo na za upotoshaji. Naagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua wote wanaotoa takwimu za uongo tofauti na zile zinazotolewa na ofisi ya takwimu. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

"Serikali inafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kwamba maendeleo ya kiuchumi yaliyopatikana yanaendana na hali ya kiuchumi ya wananchi. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

"Suala la takwimu ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi yoyote. Hasa takwimu zikiwa sahihi. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

"Rais Dkt Magufuli amevitaka vyombo vya habari na wataalamu wa mitandao kuacha kutafuta takwimu za kupikwa na badala yake wawaone wataalamu wa takwimu ili wapate takwimu sahihi. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

“Waziri wa fedha, hakikisha unafuatilia suala la AirtelTanzania . Kwa taarifa nilizonazo Airtel ni mali ya TTCL_TANZANIA. Kuna michezo michafu sana inaendela...hakikisha unafuatilia suala hili kabla ya mwaka huu kuisha. ” – Rais Magufuli [HASHTAG]#OfisiYaTaifaTakwimu[/HASHTAG],Dodoma

Imetolewa Na;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi
UVCCM TAIFA
 
Back
Top Bottom