Watanzania ifike point tukubali uhalisia na tuchukue kama funzo kwa majiji mengine, Kwa sasa jiji lenye future angalau inayoeleweka ni Dodoma, Jiji limepangwa vizuli, Miundombinu mizuli ipo na inaendelea kujengwa, Huduma za hadhi ya juu Afya, Elimu n.k na hapo wanamalizia International Airport zile Fly Emirates, Ethiopia Airline n.k tutaanza kuona mikia yao hapo. Wizara ya Ardhi badala ya kung'ang'ana na magorofa ingejikita kwenye kuokoa miji yetu bado hawajachelewa, wapange miji unaweza kua na nyumba ya kawaida kabisa lakini imejengwa kwenye maeneo yaliyopangwa ikavutia kabisa kuliko hii staili ya ukuaji wa miji ya sasa, Miji inaharibika sio mchezo kwa Dodoma nawapa salute ila haya majiji mengine sijui Dar, Mwanza, Arusha na kwingineko kulikopangwa ni katikati ya Miji tu huko kwingineko ni tafrani kila mtu anajenga akili yake inavyomtuma na tatizo ni mamlaka kukwepa kuwajibika, suala la Ardhi sio la kuachia mtumishi mmoja mmoja ni la kutengewa bajeti hasa wanaweza kuwapanga watu na kuwaacha kwenye maeneo yao ila serikali ilipe fidia maeneo yatakayotwaliwa kwa shughuli za kijamii na miundombinu, Hii staili ya sasa haifai na Migogoro haitaisha.
Note: Naiona future ya Dodoma kwingine kulikobaki tia maji tia maji