Kuna watu ni hodari wa kuiponda Dar.
Wa Kaskazini Utaskia Chugga ni nchi ile baba,
Wa Kanda ya Ziwa utaskia Mwanza ni bonge la jiji.
Wa Nyanda za juu,utaskia sifa kibao kuhusu Mbeya.
Na sasa kuna hawa wa Dodoma...
Tembelea hayo majiji yenyewe ndiyo utakapochoka....
- Unaweza maliza zunguka hayo majiji kwa masaa mawili na ukayamaliza
- Viwanja vya bara ni vya kuhesabika
- Aina za bata ni za kuhesabika
- Ukosefu wa baadhi ya huduma
- Majiji ambayo ikifika saa 4 usiku, Usafiri unakoma.
- Maeneo yenye mikusanyiko ya watu inahesabika
Arusha,Mwanza,Mbeya na Dom yanastihili sifa lakini siyo kwa kuiponda Dar...
Hakuna jiji la kuifikia Dar ndani ya nchi, ukweli wenye kuuma.