Dodoma: Mradi wa Barabara ya Mzunguko umezalisha ajira kwa watu zaidi ya 1,000

Torra Siabba

Senior Member
Jul 24, 2016
105
102
IMG-20230418-WA0021.jpg


Mradi wa Barabara ya Mzunguko Mkoani Dodoma una urefu wa Kilometa 112.3 na umegawanyika katika sehemu mbili.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu anasema sehemu ya kwanza ya Mradi huo inaanzia Nala – Veyula - Mtumba hadi Bandari Kavu ya Ihumwa na urefu wake ni Kilometa 52.5.
IMG-20230418-WA0022.jpg

Amefafanua kuwa gharama ya mradi kwa jumla ni Tsh. Bilioni 100.84 na inajengwa na Kampuni ya China

Mhandisi Leonard Chimagu anafafanua kuwa hadi Aprili 2023 mkandarasi wa mradi huo amefikia hatua ya 24% ya utekelezaji.

Amesema “Kwa wastani huo, kimahesabu mkandarasi yupo mbele kwa 1.5% kulingana na programu yake ya kazi.”

Sehemu ya pili ya ujenzi wa mradi huo inatarajiwa kuwa na urefu wa Kilometa 60, ikianzia Bandari Kavu ya Ihumwa - Matumbulu hadi Nala.

Mhandisi Leonard Chimagu ameeleza kuwa mradi huo unaojengwa kwa muda wa miezi 43, utagharimu Tsh. Bilioni 120.8 na unajengwa na Kampuni ya China kwa gharama ya Tsh. Bilioni 120.86 na utekelezaji wake upo katika kiwango cha 19%.
c97b81d5-c839-46c3-856b-0d85d2a5b631.jpg

fe56c14a-3a1c-488e-a6b6-d922497fd85d.jpg

Mradi huo ulianza Septemba 2021 na unatarajiwa kukamilika Machi 2025, unasimamiwa na kampuni mbili kwa gharama ya Dola Milioni 1.9

Amebainisha ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Mzunguko Mkoani Dodoma utakapokamilika utachochea kukua kwa uchumi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
Ameongeza kuwa utasaidia kupunguza msongamano wa magari ndani ya Dodoma kwa kuwa magari makubwa yanayoenda nje hayatapita katikati ya mji, pia umezalisha ajira kwa watu zaidi ya 1.000 katika sehemu zote mbili za mradi.
 
Back
Top Bottom