TANROADS Yatoa Ufafanuzi Kuharibika kwa Barabara ya Kigoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941


Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umeeleza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha uharibifu wa barabara eneo la Busunzu kwenye barabara kuu ya Kigoma-Mwanza umetokana na mabadiliko ya kimazingira (Geo-Environmental).

Akitoa ufafanuzi wa suala hilo, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma amesema eneo hilo liko kwenye mradi wa barabara ya Mvugwe hadi Nduta Jct yenye urefu wa kilometa 59.35 na taarifa za kuonesha nyufa walizipokea tangu Februari 24 mwaka huu.

“Sisi TANROADS tangu Februari 24 mwaka huu, tulipewa taarifa na Mhandisi Mshauri kwamba wameanza kuona nyufa za mipasuko katika sehemu ya barabara, tuliwashauri kuendelea kuangalia lakini baada ya siku mbili walituambia wanaona kuwa nyufa hizo zinaongezeka kila kukicha”, amesema Mhandisi Choma.

Mhandisi Choma amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa sehemu ile imepatwa na kitu kinachoitwa land slide (kushuka kipande kikubwa cha ardhi) ambayo imechangiwa na tatizo la geo-environment (tatizo la kimazingira) ambalo linahitaji uchunguzi wa kina na unaendelea kwa sasa.

“Tuliona ni vyema pia tutumie taasisi nyingine nje ya TANROADS na tuliialika taasisi inayofanya uchunguzi wa kiuhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwani tuliona kuifumua hiyo sehemu na kuijenga upya pasipokujua tatizo lake ni nini kuna hatari ya kutokea tena”, amefafanua Choma.

Mhandisi Choma ameeleza kuwa kutokana na barabara hiyo kuanza kutumika, TANROADS imemuelekeza Mhandisi Mshauri kufunga eneo hilo kwani lingeweza kuleta hatari kwa watumiaji wa barabara na sasa wanatumia barabara ya mchepuo.

Amesema kuwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa kina, TANROADS itachukua hatua stahiki za kushughulikia tatizo hilo ambapo uchunguzi hautafanyika kwa eneo hilo tu bali katika eneo lote la barabara hiyo ili kuepukana na changamoto hiyo kutokea tena.
 
26 March 2024
Busunzu, Kigoma

KUHARIBIKA KWA BARABARA KIPANDE CHA MITA 50 ENEO LA BUSUNZU, KIGOMA

1711538214587.png


TANROAD mkoa wa Kigoma wanafuatilia kujua hali hiyo iliyotokea ktk barabara hiyo kutoka Kigoma kwenda Mwanza.

Mhandisi wa TanRoad wanawasiliana na wasanifu, mhandisi mshauri, wahandisi wasimamizi na mjenzi mkondarasi kampuni ya kutoka nchini China na wataalamu GeoEnviromental kuona nini ni tatizo.
 
Bokoban System Geo activities Rheomorphism....ukidumbukia hapo unajikuta upo KIVU mashariki unashangaa shangaa......

Yule wa Staativii karusha hii mambo busikubusiku bila MAWANI
 

MENEJA TANROADS KIGOMA ATOA UFAFANUZI KUHARIBIKA KWA BARABARA KIPANDE CHA MITA 50 ENEO LA BUSUNZU"​

27TH MARCH, 2024
p0f2e8eeaa471e327c9c84e6150d58ca.png

"MENEJA TANROADS KIGOMA ATOA UFAFANUZI KUHARIBIKA KWA BARABARA KIPANDE CHA MITA 50 ENEO LA BUSUNZU"

Kigoma

26 Machi, 2024


Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kigoma Mha. Narcis K. Choma ametoa ufafanuzi kuhusu kipande cha video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha kuharibika kwa kipande cha mita 50 eneo la Busunzu kwenye barabara kuu ya kutoka Kigoma kwenda Mwanza.



Amesema uchunguzi wa awali kuwa unaonesha kuwa barabara hiyo imepatwa na kitu kinaitwa landslide (kushuka kwa kipande kikubwa cha ardhi) na matatizo ya mabadiliko ya kimazingira (Geo-environmental) ambayo yanahitaji uchunguzi mkubwa zaidi wa kina ambao unaendelea hivi sasa.



Akizungumza na Waandishi wa Habari Habari leo tarehe 26 Machi 2024; Meneja huyo ameeleza TANROADS ilishapata taarifa na kuanza kuchukua hatua "tangu tarehe 24 mwezi wa pili 2024 tulipewa taarifa na Mhandisi Mshauri akishirikiana Kampuni ya Kitanzania kwamba wameanza kuona mipasuko katika barabara kwenye eneo hilo la Busunzu tukawashauri waendelee kuiangalia’’



“Baada ya siku mbili wakasema wanaona mipasuko ile inaongezeka kila kukicha, TANROADS tulichukua hatua ya kuhusisha kitengo chetu cha uchunguzi wa kimahabara na nyenzo ili wafanye uchunguzi wa kina kwa sababu wao wanavyovifaa vya kisasa vya kuweza kujua shida ni nini, tukaona ni vema vilevile kutumia Taasisi nyingine nje ya TANROADS kwa hivyo tumealika taasisi inayofanya uchunguzi wa kihandisi kutoka Chuo kikuu cha Dar- es Salaam ili kujua tatizo ni nini’’. ameeleza.



Amesema “tumeona kufumua hiyo sehemu na kujenga upya kuna hatari ya kutokea tena mipasuko kama hiyo ambapo kwa kuwa barabara hiyo ilishaanza kutumika Mkandarasi Mshauri amelekezwa afunge eneo hilo lisiendelee kutumika kwa sababu linaweza kuwa hatari kwa watumiaji wa barabara, kwa sasa magari yanapita kwenye barabara pembeni kwa hiyo barabara imeendelea kupitika kama kawaida.



Amesema usanifu ambao ulifanyika katika barabara hiyo ulionesha eneo hilo la Milima lazima likatwe kupunguza mlima uliokuwepo na ilifanyika hivyo walipima uwezo wa udongo na kuweka matabaka yote kama inavyotakiwa.



Ameongeza kuwa kama uchunguzi utaonesha ni makosa ya Mkandarasi au ni makosa ya kiutendaji hatua stahiki zitachukuliwa “Wananchi wa Kigoma wasiwe na wasiwasi tutaendelea kufuatilia kwa karibu kujua tatizo ni nini ili tulitatue tupate barabara ambayo ni bora na yenye viwango
Source : tovuti ya TANROADS
 
26 March 2024
Busunzu, Kigoma

KUHARIBIKA KWA BARABARA KIPANDE CHA MITA 50 ENEO LA BUSUNZU, KIGOMA

View attachment 2945978

TANROAD mkoa wa Kigoma wanafuatilia kujua hali hiyo iliyotokea ktk barabara hiyo kutoka Kigoma kwenda Mwanza.

Mhandisi wa TanRoad wanawasiliana na wasanifu, mhandisi mshauri, wahandisi wasimamizi na mjenzi mkondarasi kampuni ya kutoka nchini China na wataalamu GeoEnviromental kuona nini ni tatizo.
Hapo pana Calvat kweli? Hili haiwezi kuwa hujuma kweli hili? 😳
 
Back
Top Bottom