Dodoma kwawaka Moto: Sendeka ageuka Mbogo

Dodoma kwawaka Moto: Sendeka ageuka Mbogo

Yawezekana Ole Sendeka yuko kambi ya Picha hasa ukizingatia tifu lake na mamvi


QUOTE=Donatila;11216703]
pindahasira_300_182.jpg

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema taarifa nyingi za mjadala wa akaunti ya Escrow iliyofunguliwa kutokana na mgogoro wa malipo ya gharama za umeme kati ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ambao unaendelea bungeni, umeongezwa chumvi na wakati ukifika Watanzania watatolewa taarifa kamili.

Kauli hiyo ya Pinda aliitoa kanisa kuu la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika wakati wa kumsimika Dk Jackson Chilongani kuwa Askofu wa Sita wa dayosisi hiyo.

Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Jacob Chimeledya aliitaka Serikali kutoa taarifa juu ya akaunti ya Escrow ili wananchi wajue kilichotokea ili ijulikane ukweli upi na uvumi upi kwani iko hatari ya kutengeneza taifa lenye kuamini uvumi.

Dk Chimeledya alisema Watanzania sasa wanaishi kwenye hali ya sintofahamu kwani hawajui yupi anasema ukweli na yupi ni `mzushi’. Alisema ni lazima Serikali itoe maelezo kwa wananchi juu ya kashfa hiyo ili wajue kilichotokea kwani ipo hatari ya kutengeneza taifa linaloishi kwa kuamini uvumi.

“Hatutakiwi kuishi kwenye taifa linaloamini uvumi… taifa halitapiga hatua kwa taarifa za kusikia tu bila kujua ukweli uko wapi, nini kimetokea na hatua gani imechukuliwa,” alisema.

Pia Askofu Chimeledya alitumia fursa hizo kuuzungumzia mchakato wa Katiba iliyopendekezwa na Bunge, akiitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi kabla ya kupiga kura ya maoni Aprili mwaka kesho.

Alisema wananchi waachiwe waamue baada ya kuisoma katiba hiyo na si kuwafuata wanasiasa ambao wamekuwa na milengo tofauti kutokana na wengine kushawishi wananchi kupiga kura ya ndio huku kundi lingine likitaka Katiba hiyo kupigiwa kura ya hapana.

Alisema kama Serikali haitasimama imara kusimamia mchakato huo, basi utatekwa na watu wenye nia mbaya.

“Makundi yote yakae kimya Katiba hii ni ya wananchi, waachiwe waamue na si kuwasemea watu wapige kura ya ndio au hapana.

Askofu huyo aliwataka viongozi wa kanisa hilo kuongoza vizuri kwani ni aibu kwa Mkristo au kiongozi wa kanisa kuharibu kanisa, kinachotakiwa kila mmoja kuchukua nafasi yake kuongoza kanisa vyema.

Akitoa salamu za Serikali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuhusiana na kashfa ya Escrow na IPTL alisema taarifa nyingi zimeongezwa chumvi. Hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani kuzungumzia suala hilo, huku akisisitiza kuwa, wakati ukifika Serikali itatoa maelezo ya kina na kuwafanya Watanzania wapate ukweli.

Sakata la madai ya kuchotwa kwa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo linalotawala kwa sasa nchini, hasa baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Swerikali (CAG) kuwasilishwa bungeni, na sasa ikitarajiwa kujadiliwa bungeni kwa siku mbili kuanzia keshokutwa. Akizungumzia Katiba Inayopendekezwa, alisema Serikali itatoa nakala za kutosha za katiba hiyo ili wananchi wengi wasome na kupata fursa ya kutoa maoni yao.

Aidha, alisema Kanisa la Anglikana nchini limetoa mchango mkubwa katika kuendeleza huduma za jamii kwa kujenga shule, hospitali, vituo vya afya na miradi mingine ya kijamii. Pia aliutaka uongozi wa kanisa hilo kuibua fursa za miradi ya maendeleo ili kusaidia familia masikini kuwa na miradi midogo ikiwemo ya ufugaji kuku.

Kwa upande wake, Dk Chilongani aliahidi kuboresha elimu na huduma za jamii na kusimamia kikamilifu vitenga uchumi vya kanisa hilo.

“Sikuota kuwa askofu ni neema ya Mungu,” alisema.

Chanzo :Habari leo
[/QUOTE]
 
Mjini Dodoma jioni hii katika cha Kokas kinachoendelea Seneka aamua kuwa Mbogo:

SENDEKA asema tutauana lakini PINDA hajiuzulu katu.
Kikao cha wabunge wa CCM kinachiendelea mchana huu kimekuwa moto mbali. Christopher Ole Sendeka mbunge wa Simanjiro amesema wako radhi kuchinjana bungeni lakini si Pinda kujiuzulu. "Ajiuzulu amekosa nini, ripoti zote hazimtaji popote kuhusika. Kama tatizo ni nia yake ya u Rais, kwani Pinda hana haki ya kugombea? Nasema niko radhi tuchinjane bungeni lakini si kuona mtu anasulubiwa kwa maslahi ya wabinafsi wachache wenye malengo yao ya kisiasa. Kwa hili nitasimama kidete. .."alisema Sendeka huku ukumbi wote ukiwa kimya

sendeka hapatani na lowassa ,ana wasiwasi kama pinda akijizulu lowasa atapata urais kilaini
 
Sendeka mmoja wa watu wapumbavu sana na wasiojua upumbavu wako ndio maana hupayuka kwa sauti kubwa

Hasomi, anaongozwa na hisia na ushabiki wa kipuuzi... report iko wazi, accountability principles zinafahamika nk. If you ask Ole Sendeka arejee principles za uwajibikaji, hawezi kujibu

He is one of a waste wanaopata nafasi ya kupayuka bila sababu, his days kama mbunge are numbered vilevile
 
kwa kiswahili lugha yako Mama tafadhali!

Sijuwi kutafsiri majina wala siioni mantiki yake.

Bush, sijaona akiitwa vingine hata anapoandikwa kwenye magazeti ya Kiswahili.
 
Back
Top Bottom