Serikali yashtuka kutoka usingizini; Msekwa ajibu tuhuma za ufisadi Ngorongoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yashtuka kutoka usingizini; Msekwa ajibu tuhuma za ufisadi Ngorongoro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 19, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  *Maige amsimamisha mkurugenzi wanyamapori
  *Msekwa ajibu tuhuma za ufisadi Ngorongoro
  *Mgawo wa umeme walalamikiwa upya bungeni

  Na Waandishi Wetu
  [​IMG]


  SAKATA la kutorosha wanyamapori kwenda nje ya nchi limeishtua serikali kutoka usingizini baada ya Mkurugenzi wa
  Idara ya Wanyamapori Bw. Obeid Mbwangwa na watendaji wengine wawili kusimamishwa kazi na serikali ili kupisha uchunguzi.

  Bw. Mbwangwa amekumbwa na hali hiyo zikiwa ni siku chache baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, na siku moja baada ya wabunge kutaka hatua zichukuliwe haraka kwa wahusika, akiwamo mkurugenzi huyo na wanyama walioibwa warejeshwe ama wakiwa hai au wamekufa.

  Kutokana na agizo la Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mkurugenzi wa awali, Bw. Erasmus Tarimo Februari 8, mwaka huu na kumpatia likizo ya kusubiria kustaafu ambapo kwa mujibu wa sheria Julai 7, mwaka huu ndipo Bw. Mbwangwa alishika wadhifa huo kutoka nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa wizara hiyo.

  Tamko la kusimamishwa kazi kwa Bw. Mbwangwa na wenzake wawili ambao hawakutajwa majina ili kupisha uchunguzi, lilitolewa jana bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige wakati akifanya majumuisho ya makadirio na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2011 na 2012.

  "Mheshimiwa Spika kutokana na malalamiko mengi ambayo waheshimiwa wamelizungumzia ni suala la kutoroshwa kwa wanyamapori, ninashukuru sana na maoni ya kamati juu ya suala hili ni nimeyazingatia," alisema Bw. Maige

  "Hivyo basi kuanzia leo Agosti 18, 2011 Mkurugenzi wa Maliasili na Utalii, Obeid Mbwangwa na wenzake wawili ambao kutokana na uchunguzi wa jambo hili sitawataja hapa, nimewasimamisha kazi rasmi, ili kupisha uchunguzi wa utoroshaji wa wanyamapori hao," aliongeza.

  Kilio cha wabunge

  Wabunge jana waliendelea kuchangoa bajeti hiyo, wakiitaka serikali kuwarudisha wanyama 116 waliotoroshwa, wawe hai au mizoga kwa kuwa na kama itashindwa kufanya hivyo itakuwa imeonesha udhaifu mkubwa.

  Walisema kwa kitendo hicho, serikali imeingia doa ambalo ni tishio kwa usalama wa taifa kwa kuruhusu ndege ya kijeshi ya Qatar kuingia nchini na kuruhusiwa kukaa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa kuwapakia wanyama hao na kuwasafirisha.

  Mbunge wa Simanjiro, Bw. Christopher Ole Sendeka (CCM) alisema utoroshwaji wa wanyama hao ulifanyika kwa sababu viongozi wengi wamezoea njia za kufanya mambo kwa mkato.

  Mbunge huyo alisema nyara za taifa zinaporwa kwa kiasi cha kufedhehesha, hivyo leseni 180 za uuzaji wanyama nje zifutwe na zichomwe moto kuanzia jana.

  "Mkurugenzi wa Wanyamapori Bw. Mbangwa hawezi kukanusha kuhusika katika utoroshwaji wa wanyama hai na ndege hai kwa kutumia ndege ya jeshi la Qatar kutoka Uwanja wa Ndege KIA, kuna matatizo katika idara hiyo likiwemo suala la ukabila, hivyo waziri ana kazi ngumu kuibadilisha idara hiyo," alisema Bw. Sendeka.

  Alisema kama Bw. Maige anataka kuwafahamu ama kupata ukweli kuhusu wanyama na ndege waliotoroshwa, aandike barua Geneva Uswisi na waliohusika wataumbuka na kuchukuliwa hatua za kisheria.

  "Tupo tayari kuwapokea wanyamapori wetu wakiwa hai au mizoga, Mheshimiwa Spika bila kusita wanyama wote waliotoroshwa hapa nchini tunahitaji warejeshwe mara moja, hiki ni kibarua kizito kwa kuwa ilichangiwa na tabia mbaya serikalini, lakini lazima iwe hivyo," alisema Bw. Sendeka.

  "Ni mbaya sana kuona ndege ya jeshi la Qatar inaingia hapa nchini katika uwanja wa ndege wa KIA bila kibali na kufanya kazi yake kisha kuondoka na wanyamapori wetu wakati nchi zingine haiwezekani ndege ya kijeshi kutua na kufanya hivyo, hali ya usalama wa nchi iko hatarini," alisema Bw. Sendeka.

  Aidha mbunge wa Maswa Magharibi Bw. John Shibuda (CHADEMA) akichangia katika hotuba hiyo alisema utoroshaji wa wanyama hao ni doa kwa taifa hivyo haoni sababu ya kumsifia kiongozi yeyote kwa kuwa wanaipeleka nchi katika hali mbaya kiusalama.

  "Kutoroshwa kwa wanyamapori hao kumeidhalilisha Idara ya Usalama wa Taifa, Polisi, na mamlaka nyingine za usalama na hawa wanaoitwa intelijensia taarifa zao zilikuwa wapi tangu wanyama hao walipokuwa wanakusanywa," alisema Bw. Sibuda.

  Aidha Mbunge wa Kilindi Bi. Beatrice Shelukindo (CCM) alisema matatizo yote ya kuuza wanyamapori yanatokana na viongozi wasio waadilifu.

  "Mheshimiwa spika Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori hastahili kuwepo kwenye nafasi hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyetoa vibali 180 kwa wafanyabiashara kuuza wanyamapori nje ya nchi.

  Serikali yasitisha vibali

  Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda jana katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo aliwaeleza wabunge kuwa serikali imesitisha vibali vya usafirishaji na uuzaji wanyama nje ya nchi kwa kuwa biashara hiyo haina manufaa kwa taifa.

  Bw. Pinda alisema biashara hiyo itatazamwa upya, na itakapoanza masharti yatabadilika ikiwa ni pamoja na kiwango cha tozo kwa kuwa wafanyabiashara wanapata faida kubwa kuliko serikali

  Msekwa akanusha tuhuma dhidi yake

  Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Pius Msekwa amepuuza vikali tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wabunge na kusema kuwa ni maneno ya 'kijinga na kipumbavu'.

  Akizungumza kwa njia ya simu akiwa Dodoma jana, Bw. Msekwa alisema kwamba yupo kwenye ziara ya kikazi na madai yanayotolewa juu yake kwamba anatumia vibaya nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi ya Ngorongoro kugawa maeneo kwa wafanyabiashara ni ya kipuuzi.

  "Ndugu mwandishi nisikilize vizuri, madai hayo ni ya kipuuzi lakini nitaitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia ukweli wa jambo hilo," alisema Bw. Msekwa.

  Umeme walalamikiwa upya

  Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda ameitaka serikali itoe maelezo kuhusu kukosekana kwa umeme usiku na mchana katika maeneo mbalimbali kwa siku kadhaa licha ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kupitishwa wakati ikionesha matumaini makubwa.

  Bi. Makinda alitoa agizo hilo jana bungeni mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Nyamagana, Bw. Ezekiah Wenje (CHADEMA) kuomba mwongozo wa spika, ili bunge lijadili jambo la dharura kwa kutumia kanuni ya 87(1).

  Wakati anaomba mwongozo huo Bw. Wenje alilieleza Bunge kuwa, hakuna umeme Mwanza kwa siku nne sasa usiku na mchana, na pia tatizo hilo lipo kwenye maeneo mengi nchini ukiwemo mkoa wa Arusha, Kigoma na Dar es Salaam.

  Imeandikwa
  na Godfrey Ismaely, Rachel Balama, Dar na Pendo Mtibuche, Dodoma
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Nadhani imefika wakati wa bunge kuendesha shughuli za serikali moja kwa moja.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Rais anastaafisha kiongozi bora, anasahau kumteua Mkurugenzi Mpya anaekaimu anakaimu na Ufisadi sababu hana responsibilities na hajali

  Huo ndio mfano wa kuwa na Rais mwenye Madaraka Mengi angalia Mkuu wa Mkoa wa Dar anakaimu na pia ana Lindi, Sasa hapo hakuna uwajibikaji

  Ni Wakuu Wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Wizarani, Mashirika ya Umma wote wanakaimu Rais yeye ni kupinga Vitripu Nje - A ROLLING

  STONE... TUTAFIKA KWELI?

  Where there is no leader with vision, the people perish ...
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Hatuna imani na Rais
   
 5. Tz-guy

  Tz-guy JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nchi imeoza, kila kona ufisadi...
   
 6. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Tanzania,ni nchi ya ajabu,hiyo ndege ningekuwa mfanyakazi wa kia ingekuwa ilisha ungua siku nyingi in short ningeichoma moto
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Angesema ni ya uongo na kizushi ningemuelewa lakini hakuna ujinga wala upuuzi kwenye shutuma ambazo zina-involve maliasili ya taifa
   
 8. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Kinachonishangaza ni kwamba wakati wa kampeni JK alikuwa anasikika kila siku akitoa ahadi mpya na ikiwa akapata taarifa kwamba chama fulani cha upinzani kimemchafua alikuwa anajibu tuhuma siku hiyo hiyo au kesho yake. Sasa inashangza rais huyo huyo baada ya kuingia madarakani amekaa kimya hata kwa masuala very burning kwa taifa ambalo Oktoba 2010 alipigana kufa na kupona kuliongoza. Yuko wapi yule JK mwongeaji na aliyekuwa anajibu mapigo wakati wa kampeni mwaka jana ili ajibu mapigo kwa kuwashughulikia wanaoharibu uchumi wa nchi kama alivyowashughulikia waliokuwa wanataka kumnyima kura 2010.

  JK alitumia ubunifu na mbinu nyingi ili ashinde uchaguzi ila inashangaza anashindwa kutumia mbinu na ubunifu ku -address concern za waTZ. Ni kitu gani kimemdhoofisha? au mpaka asikie vishindo vya kumpinga vinatinga mlangoni ndo ataanza tena kuwa mbunifu?
   
 9. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  na sisi wananchi tunasubiri nini kuwaondoa hawa kina jk. Sijui kama igunga wanajua kuwa wanahitaji kutochagua ccm
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kauli mbiu ya kutimiza miaka 50 ya uhuru inasema TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUMEWEZA. Je tumethubutu kwa lipi?kukabiliana na mafisadi au kwa lipi? Tumeweza lipi ambalo tumeweza angali tuu kwenye mgao wa umeme na mafuta na hongo kila kona. Tumeendelea je maendeleo yetu waTZ yanaendana na miaka ambayo tumekua huru au serikali inaanda kauli mbiu nzuri bila vitendo ili tuonekane tuna serikali endelevu wakati inatudidimiza na kutunyonya raia wake. Ipo siku uzalendo utatushinda CCM na ufisadi wenu mtajuta na kusaga meno
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  huyu mzee ana lake jambo........................hivi atueleze ilikuwaje mstaafu Bernard Murunya ambaye ni mkeewe mwenzie anaendelea kuongezewa miaka miwili katika utumishi wa umma na kuwa kibosile pale kama siyo ujinga na upumbavu wake yeye binafsi na mteule wao JK?

  Wakati taifa linalalama na vijana kukosa ajira wao wanazuia ajira mpya kwa kuendekeza ajira za mikataba kwa wastaafu.......................

  Msekwa atueleze tangia amekuwa mwenyekiti wa Bodi Ngorongoro ni hoteli ngapi zimejengwa na campsite ngapi zimejengwa ikilinganishwa na hifadhi hiyo tangia ilipoanzishwa mwaka 1959?

  More than 85% ya ujenzi wa mahoteli na campsites umefanyika katika chini ya miaka minne iliyopita baada ya yeye kuwa chairman there...............

  kama kuhoji utendaji wake ni hoja za kipuuzi na kijinga basi wacha tuendelee kuwa hivyo.........maana yeye ni Mwenyezi Mungu na hawezi kuhojiwa............................................asifikiri huu ni mfumo wa chama kimoja ambapo walizoea kufuja mali za umma na wananchi wakiwaogopa.....................tungependa kujua huyu fisadi ana shilingi ngapi kwenye akaunti zake ndani na nje ya nchi............................ccm viongozi tunajua wamegawana maeneo ya kulipora taifa hili lakini ni jukumu letu kuendelea kuhoji juu ya matumizi ya mali ya umma bila ya kujali lugha chafu zinazutmiwa na mafisadi............
   
 12. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sasa tujiulize kama inawezekana wanyamaya wakatoroshwa kwa document halili zilizobarikiwa na watendaji wa serikli na huku watu wa UWT wakiwepo seheemu mbali mbali na wanaona bila kuzuia
  • je ni wanyama wangapi wametoroshwa na wanaedelea kutorshwa kwa njia za panya bila kutumia document ?????

  kama serikali ya tanzania na serikali zote za afrika mashariki na afrika kiujumla zinaendela kuuza wanyama Je hazioni ni kusaliti na kuhujumu uchumi nautalii wa nchi zao? Bunge la afrika la bunge la afrika mashariki yantakiwa kukubalina kutkuuza wanyama hai nje ya nchi kwa mufaa ya utalii na vivutia vyetu.

  Soon mzungu au mwarabu akienda Qatar zoo atakuwa hana shida tena ya kuja afrika mashariki zaidi sana sana atataka kuja kushuhudia vumbi na wamasai. Nadhani utalii uliobaki wao kushangaa ni kushangaa sisi wananchi na umasikini wetu na nyumba zetu za nyasi . Hivyo ndio vivutio maana kama wanyama tayari wote wanao hata kwao.

  Au zaidi wakija itakuwa kwa jili ya kuwinda na kuwauwa wanyama . kitu ambacho naamin na cheneywe kinafanywa wa bei nafuu bila kuzingatia hata umri wa wanyama. it very hard kwa msasai kuruhusiwa kuwinda lakini nia rahisi na cheap kwa mzungu au mwarabu kwa mgongo wa utalii kuruhusiwa kuwinda.

  thats is not sustaibale tourims
   
 13. only83

  only83 JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  .................Nahamu kusikia Msekwa atajibuje...
   
 14. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  He he heeeeeee! Muhindi aljisemea 'domo jumba maneno'
   
 15. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwakweli hii ni aibu kubwa kwa nchi yetu ama wakiri kuwa walifahamu mpango mzima na kuidhinisha upelekwaji nje wa wanyama hao kuliko kusema walitoroshjwa, hapa ni doa kwa TISS, TPDF, Police, MNRT na TAA
   
 16. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hebu tuwache jazba na kujiuliza hivi hizi zoos zimeanza jana na juzi tu huko duniani? Zoos ziko nyingi na zina wanyama tofauti kutoka nchi mbali mbali tangu enzi na enzi. Wanaokwenda kwa asilimia kubwa ni familia na hasa wanafunzi wanajifunza kuhusu maisha ya wanyama na viumbe vyengine mbali mbali.

  Si kweli kwa watalii ambao wako serious wataishia kumuangalia twiga na simba kwenye zoo halafu waridhike. The great migration haiwezi kutokea kwenye zoo na ni lazima mtalii aje kuangalia hapa hapa Serengeti au labda Maasai Mara. Mtalii yo yote aliye serious anataka aone mnyama kwenye mazingira yake ya asili na yuko radhi kuweka fedha zake ili afanikishe lengo lake.

  Tukihifadhi mazingira vizuri wanyama hawatapotea kwa kuwa tu ttwiga au simba mmoja amechukuliwa kupelekwa kwenye zoo. Kwa hapo tusidanganyane. Vile vile hawa wanyama wanahitajika kuwa culled (yaani kupunguzwa kwa idadi maalumu kila mwaka). Inategemea ni wanyama wa aina gani na kuna population yake kiasi gani, ndiyo maana kuna hunting quotas.

  La kuzungumzia hapa ni kwamba hao wanyama wameuzwa kwa kiasi gani na serikali imepata mapato kiasi gani lakini siyo tena kwamba twiga watamalizwa eti kwa kuwa mmoja amepelekwa nje ya nchi.
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Bintimkongwe.
  Hakuwa twiga mmoja aliyechukuliwa na lile dege la Arabuni. Walikuwa zaidi ya sita. Na wala hatujui huyu shehe kailipa serikali kiasi gani au yalikuwa maelewano baina yake na Luhanjo. By the way, nasikia waheshimiwa wa TANAPA wamejaza majengo ya kisasa huko Dubai na Qatar. Hizi si hela za madafu eti.
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
 19. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Tuhuma dhidi ya Mswekwa ni ukweli tena ukweli MTUPU, amekuwa akilazimisha, na mpaka sasa ni yeye anayelazimisha Ujenzi wa hii HOTELI. Hilo eneo ni mapitio ya FARU, EIA-report inaonyesha hivyo, wataalamu wa ngorongoro walilizungumzia hilo na kila kukicha wanapiga kelele, kuna report imepelekwa UNESCO naamini wakiendelea kilaziomisha Ngorongoro itakuwa de regesterd na UNESCO

  Huyu mzee ni jeuri na kiburi chake kinatokana na ukaribu make na Mkuu wa KAYA, kama hamjui kipindi cha kampeni Mkuu wa kaya alikuwa anaishi kwenye nyumba za ngorongoro zilizopo hapo Arusha, je Msekwa ataachaje kuwa na kiburi? kama anamlindia mkubwa maslahi?. tena alikuwa mbioni kumsaidia Ali Al bawardy miliki wa Belila kupata eneo ngorongoro ila UNESCO ILIWEKA ngumu

  Huyu mzee amekuwa hajali kabisa maslahi ya wamasai wanaoishi ngorongoro, aliendesha zoezi la kuwahamisha baadhi ya masai kutoka ngorongoro kwa uonevu mkubwa ili hali hii jamii imeishi ngorongoro bila kuzuru wanyama kwa miaka mingi

  cha msingi hawa watawala WEUSI, WANACHOKIFANYA WANATAFUNA MALIASILI ZETU LEO BILA KUANGALIA VIZAZI VIJAVYO VITARIDHI NINI

  imefika mahali sasa watanganyika tuamke HII MIZEE AINA YA AKINA MSEKWE IMEKUWA MADARAKANI KWA MIAKA ZAIDI YA 50 HAWAJATULETEA CHOCHOTE, CHA MUHIMU NI VIJANA TUAMKE NA TUWAAMBIE BASI
   
 20. il dire

  il dire Member

  #20
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  trully Nyerere huko ulipo tunakuomba utusamehe huyu mk.ree hajui halifanyalo ye ni kusafiri kuongoza nchi awezi. Adi magamba wenzake kumtetea hawezi kila pande ya nchi ameacha uozo utafikiri cancer ya damu inavyosambaa mwilini. 2015 hatufiki 2.
   
Loading...