Wabunge CCM wamlipua Kikwete, WADAI WANAKERWA JINSI RAIS ALIVYOMGEUKA PINDA, MAKINDA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CCM wamlipua Kikwete, WADAI WANAKERWA JINSI RAIS ALIVYOMGEUKA PINDA, MAKINDA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, Feb 4, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi wetu, Dodoma

  MOTO umewaka ndani ya kikao cha wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo wawakilishi hao walifikia hatua ya kutoa maneno makali dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete.

  Wabunge hao wamesema hawaridhishwi na mwenendo wa serikali ya Rais Kikwete kiasi cha kufikia hatua ya kutishia kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

  Wabunge hao pia walipendekeza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda, Naibu Waziri Dk. Lucy Nkya na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Blandina Nyoni watimuliwe kwa kusababisha mgomo wa madaktari uliochangia kuongezeka kwa vifo vya wagonjwa waliokosa huduma za kitabibu katika hospitali mbalimbali nchini.

  Wabunge hao waliichachamalia serikali katika kikao cha ndani cha wabunge wa CCM, kilichofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini hapa, chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Mizengo.

  Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vilisema kuwa pamoja na mambo mengine, wabunge hao walionyeshwa kukerwa na mambo mawili makubwa yaliyofanywa na Rais Kikwete na kusababisha wabunge wake wa CCM waonekane wajinga mbele ya wenzao wa upinzani, hususan Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA.

  Kwa mujibu wa habari hizo, mambo hayo ni pamoja na suala la posho mpya za wabunge na jinsi Rais Kikwete alivyoamua kumgeuka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Anna Makinda, juu ya suala la posho za wabunge.

  Jambo jingine lililosababisha wabunge hao kumchambua Rais Kikwete ni suala la mabadiliko ya sheria ya Katiba ambapo mapendekezo mengi yaliyopitishwa na wabunge wa CCM bungeni yameondolewa baada ya Rais Kikwete kukubali mapendekezo ya CHADEMA.

  Miongoni mwa wabunge waomlipua Rais Kikwete katika kikao hicho, Beatrice Shelukindo (Kilindi), alieleza kutofurahishwa kwake na majibu ya Rais Kikwete kuhusu posho mpya za wabunge.

  Mbunge huyo machachari alisema kuwa anashangazwa na serikali ya Kikwete kutokuwa na mawasiliano na viongozi wenzake kiasi cha kutoa majibu yanayotofautiana katika jambo moja, hali ambayo imewashangaza wananchi wengi.

  Shelukindo alisema kauli ya Rais Kikwete kusema kwamba hajabariki posho mpya na kwamba hakuna mahali alipotia saini, imewaumbua Spika Anne Makinda na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambao walitamka hadharani kwamba Rais tayari ameshabariki posho hizo.

  Shelukindo alisema pia kwamba Rais amewaudhi katika kushughulia sheria ya mabadiliko ya Katiba, kwani muswada ulioleta sheria hiyo ulipitishwa na wabunge wa CCM baada ya wabunge wa CHADEMA kuususia na kutoka bungeni, lakini baada ya Rais kukutana nao Ikulu, sasa Bunge zima linalazimika kuipitia sheria hiyo kuhalalisha mapendekezo yaleyale yaliyoletwa na CHADEMA.

  Shelukindo alisema binafsi anakerwa na tabia ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda kuamua kutenda mambo kana kwamba hawawasiliani. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Shelukindo alifikia mahali akatishia kuwa kama Rais ndiye tatizo, wabunge wana uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

  Hata hivyo, kauli hiyo nzito ilipingwa vikali na Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka ambaye alimtaka Shelukindo afute kauli yake na kuomba radhi kwani lengo la kumchambua Rais Kikwete na serikali yake, halina nia ya kumuangusha, bali kuisaidia serikali yake.

  Kutokana na kauli hiyo, Shelukindo aliomba radhi na kufuta kauli yake, lakini alisisitiza kuwa hakuwa na lengo baya.Sendeka alijikita kwenye suala la posho na kuwataka wabunge wenzake wa CCM kuachana nayo kwani inawajengea taswira mbaya mbele ya jamii.

  Alipendekeza kuundwa tume kuchunguza tuhuma za ufisadi katika Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na John Magufuli ambapo inadaiwa kuwa zaidi ya sh bilioni 10 zimechotwa kulipia kampuni hewa ya ujenzi.

  Sendeka alisema kuwa katika tuhuma hiyo inayohusisha vigogo wanaotaka kuwania urais, kati ya malipo ya mkandarasi kampuni ya CHICO-CRSG JV, sh bilioni 10 zimeongezwa kwa lengo la kuwanufaisha vigogo hao.Kuhusu sakata la mgomo wa madaktari, Sendeka alieleza kutoridhika kwake na jinsi serikali ilivyokuwa ikilishughulikia tatizo hilo.

  Hata hivyo Sendeka na baadhi ya wabunge walipendekeza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Naibu wake na Katibu Mkuu, wajiuzuru kwa kusababisha kutokea kwa mgomo huo.

  TANZANIA DAIMA

   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sioni ukweli wa habari hii
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  I thought this comment is from a sensible person but from a demented old woman, so sorry!!!
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hata mie baada ya kuisoma nimepatwa na wasiwasi kweli,kwani niwajuwavyo wabunge wa CCM kutoa kauli tata kama hizo kwa Mh Rais haiwezekani,nikaona hebu tuiweka hapa jukwaani tupate ukweli halisi,maana tunaelewa kuwa wapo waandishi Dodoma wanaweza kutudhibitishia habari hii

  lakini pia yawezekana ikawa hivyo,kwani kuna threads inayoelezea tetesi za wabunge wa ccm kutaka kutoupitisha sheria ya mabadiliko katiba,eti hawakubaliani na mabadiliko yaliyofanywa na Mh Rais,

  lolote lawezekana Masanilo ngoja tuone
   
 5. a

  adobe JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Kumbe wanajifanya kumshupalia jk tu kwa sababu wamekosa posho,nyang'ao hawa na mitumbotumbo yao wakome.ila serikali inayoongozwa na mzaramo noma.huyu m,ramo kachemsha ktk kauli zake nyingi,oh uzio wa jangwani uvunjwe nk.labda vyakula vya nazi vimadidimiza bongo za wa pwani
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Chanzo chako cha kuaminika ni Uhuruau Jamba zako leo? kipi kati ya hivyo viwili unakiamini?
   
 7. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Poor FF, lini utajifunza kwamba enzi za habari za kuaminika kutolewa na Uhuru na Mzalendo zishapitwa na wakati??
   
 8. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Siku zote mambo yakiharibika atalaumiwa kiongozi kwa hiyo mimi nampongeza sana Kikwete pale anapogundua ameingizwa chaka na wana CCM anachukua hatua ya kusahihisha mapungufu.
   
 9. m

  moshingi JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK ni mwanasiasa mjanja, mwenye uwezo wa kuona mbali sana...
  Wakati mwingi amekuwa akijitofautisha na wabunge wa chama
  chake kwa kuwa wamekuwa wakitenda katika namna ya kukitia
  hasara chama, posho ni jambo ambalo wananchi wengi wanalipinga
  sana kwa vile tayari wabunge wanakipato kikubwa sana, hivyo kujiongezea
  posho ni kuongeza gap kati ya wananchi na CCM.
  CDM walipotoka bungeni hali ya amani nchini ilikuwa ni tete sana, ilikuwa
  ni busara sana kwake kukutana nao ili kuepusha shari...alifanya jambo jema
  kwa manufaa ya taifa wabunge wa CCM walishupalia ushabiki ambao ungeliingiza taifa
  katika machafuko... BIG UP JK!!!
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Hii habari haina ukweli, siiamini
   
 11. Teacher1

  Teacher1 JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kama kweli rais kakataa kusaini ma kuhalarisha posho mpya za wabunge basi mtazamo Ma busara zake ni kubwa kuliko wabunge wake. Sote tunaishi na kununua vitu katika maduka hayahaya iweje mtu mmoja apokee posho ya kikao inayolingana na mishahara ya miezi miwili ya wataalamu wingine? Mawazi ya chadema Kama yameingizwa basi rais wetu ameanza kufunguka na ninmshauri kuwa achuje mawazo anayopewa na wanaccm wenzake mengi ni potofu ajikite chadema ni kisima cha mawazo bora ya maendeleo ya nchi hii.
   
 12. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii habari kama niyaukweli basi wabunge wote wa ccm ni janga la kitaifa,yaani wako radhi taifa lipate katiba ya ovyo hata kwa miaka mingine 50 ilimradi wasidharaulike mbele ya wabunge wenzao wa chadema,mbona hoja za cdm kuhusiana na suala la katiba zina mashiko na nikwa manufaa ya ustawi wataifa letu wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa?Raisi kukabali marekebisho limekuwa kosa?kwa akili ya kawaida madhara ya kutoufanyia marekebisho mswaada huu ni makubwa kuliko huko kudharaulika kwao na wenzao wa cdm wako kuongelea
   
 13. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  changa la macho hilo....hivi habari sio za ukweli ni uzushi. wabunge wa CCM hawajawa na ujasiri mkubwa kiasi cha kumchambua rais
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Hawa wamekuwa wakali baada ya suala la posho kupigwa chini.
   
 15. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  kukosa posho kumewapa ujasiri wa kutoa povu!
   
 16. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  hii I'd pia inatumiwa na mama Rwakatale
   
 17. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,721
  Likes Received: 1,630
  Trophy Points: 280
  Alahaaa kumbe FF ni ID ya Mama Rwakatare???!!
   
 18. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #18
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rais kikwete amegundua kwamba wabunge wa chama chake ni wachumia tumbo na wababaishaji,hivyo ameona heri afanye jambo ambalo angalau watanzania watamkumbuka.
   
 19. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kama haina ukweli tutasubiri wahusika wakanushe
   
 20. mimimkuu

  mimimkuu Member

  #20
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chanzo cha kuaminika ni kipi?
   
Loading...