Dodoma: Hatimaye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), yawasilishwa rasmi Bungeni

Taratibu mkuu. Hivi ofisi ya CAG inaongozwa na nani? Ni nani aliyesaini report watakayoijadili wakati wakifanya kazi na hiyo unayoiita ofisi ya CAG? Who is CAG? Without CAG Prof Mussa Assad, there is no CAG office. Labda tumuweke pembeni kwanza huyu au ajiuzuru kama tulivyokua tunapenda afanye, tumpate mwingine.... Lakini kwa sasa NI LAZIMA TUFANYE KAZI NA CAG Prof Mussa Assad. Pole sana mkuu, tukubali tu maana hakuna namna nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
kagoma. kinachofuata?
 
Kufuatia chagizo na presha kubwa ikiwa ni pamoja na matakwa ya kikatiba, leo tarehe 10 Aprili ikiwa ni siku ya mwisho kwa mujibu wa Katiba, Serikali imewasilisha Bungeni taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kama ilivyotakiwa. Orodha ya shughuli za Bunge leo inaonyesha taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itawasilishwa bungeni.

View attachment 1067384

Kwa kufuatia hatua hiyo, Ofisi ya CAG sasa inaweza kuzitoa ripoti hizo katika tovuti yake ili Wananchi waweze kuzisoma na kuelewa fedha zao zimetumikaje. Ni suala la uwajibikaji tu, tunatoa heko kwa watu waliopiga kelele ili takwa hili la kikatiba litekelezwe.

Kwa upande wa Serikali, niwashauri wajifunze na waendelee kuheshimu Katiba. Kuna kikundi cha watu ndani ya Serikali kwa sasa wanampotosha kwa makusudi Rais ili wajipatie sifa , waache huo ujinga.

Kwa upande wa Bunge, nyie mmethibitisha kuwa dhaifu, wananchi hawana muda na Bunge kwa sasa, bora waangalie tamthilia ya SULTAN.

=======

Siku ya saba baada ya kuanza kwa mkutano wa 15 wa Bunge, chombo hicho cha kutunga sheria katika orodha ya shughuli za Bunge moja ya hati za kuwasilishwa ni taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, ambaye Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya naye kazi kutokana na kukiita chombo hicho dhaifu.

Dodoma. Leo Jumatano Aprili 10, 2019 Bunge la Tanzania litawasilishiwa hati ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Orodha ya shughuli za Bunge leo Jumatano, Aprili 10 inaonyesha taarifa hiyo ya fedha ya mwaka wa fedha 2017/18 itawasilisha bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisa ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ikiwa ni siku ya saba tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Aprili 2, 2019. Hata hivyo orodha hiyo inaweza kubadilika.

Wakati taarifa hiyo ikiwasilishwa, jana Jumanne, Aprili 9 jioni ofisi ya CAG ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa leo Profesa Assad atakuwa na mkutano na waandishi kueleza yaliyomo katika taarifa yake ya ukaguzi.

“Nawakaribisha katika ukumbi wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (Naot) ghorofa ya pili. Jengo lipo nyuma ya jengo la hazina (Dodoma). Karibuni nyote msihofu,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ya mwaliko.

Hata hivyo, siku zote taarifa hiyo baada ya kuwasilishwa bungeni, CAG hukutana na wanahabari katika ukumbi wa Bunge kueleza yaliyomo katika ripoti yake ya ukaguzi, huenda safari hii ameamua kufanyia ofisini kwake kutokana na azimio la Bunge la kutofanya naye kazi.
Nakumbuka hawa wabunge wakati wakiapa Bungeni walisema watakuwa waaminifu kwa nci yao na kulinda sheria. Wamekula maharage ya wapi na kujisahau? wanatumia ignorance za watanzania kuamua chochote bila kujali katiba ambayo ndo msingi wa kuwa Bungeni. Anyway ngoja tujiandae 2020 kuhakikisha kila aliyekuwa kwenye hilo Bunge sana sana wa ccm harudi kwenye hilo jengo. Nitachukua fomu ya KUGOMBEA UBUNGE MWAKA KESHO "JUA LIWAKE AU LISIWAKE, MVUA INYESHE AU ISINYESHE ILI TUWEKE UTAWALA BORA TUHAKIKISHE KAMA HAWA AKINA MSUKUMA NA LUSINDE HAWAPATI NAFASI NA KUNAJISI CHOMBO KITUKUFU CHA KUTUNGA SHERIA"
 
Siku nyingine ukichelewa jaribu kupitia uone wenzio wamechangia nini, huenda swali ulilojiuliza wenzio washajiuliza na kujibiwa

Ifike hatua muiheshimu jf kwani ndio sehemu pekee mtu anakuwa huru na kufanya vitu kama yeye na sio mifumo, kanuni wala taratibu za kazi take.

Sent using Jamii Forums mobile app


Mkuu mimi sikuelewi, uwe muwazi katika lugha nyepesi na rahisi kueleweka, we are people of different calibres herein.
 
KUNA KITU KINAITWA "ARGENT THEORY" SASA BILA RIPOTI YA FEDHA HAWA WANAOJIITA WAZALENDO WATATWAMBIA NINI?
 
Siyo rahis Ku edit
Unanyofoa page zenye shida and replace them with the cooked ones , the you re bind! Definitely ni kazi, lkn kwa vile BUNGE ZIMA hakuna a kuweza kukaa chini na ku scan through, given the limited time, inakuwa imetoka!
 
Nakumbuka hawa wabunge wakati wakiapa Bungeni walisema watakuwa waaminifu kwa nci yao na kulinda sheria. Wamekula maharage ya wapi na kujisahau? wanatumia ignorance za watanzania kuamua chochote bila kujali katiba ambayo ndo msingi wa kuwa Bungeni. Anyway ngoja tujiandae 2020 kuhakikisha kila aliyekuwa kwenye hilo Bunge sana sana wa ccm harudi kwenye hilo jengo. Nitachukua fomu ya KUGOMBEA UBUNGE MWAKA KESHO "JUA LIWAKE AU LISIWAKE, MVUA INYESHE AU ISINYESHE ILI TUWEKE UTAWALA BORA TUHAKIKISHE KAMA HAWA AKINA MSUKUMA NA LUSINDE HAWAPATI NAFASI NA KUNAJISI CHOMBO KITUKUFU CHA KUTUNGA SHERIA"
Kumbuka hawa wanatumia tume yao ya uchaguzi, nani atakutangaza we we?
 
Unanyofoa page zenye shida and replace them with the cooked ones , the you re bind! Definitely ni kazi, lkn kwa vile BUNGE ZIMA hakuna a kuweza kukaa chini na ku scan through, given the limited time, inakuwa imetoka!
IKo hewani You Tube
 
Back
Top Bottom