Dodoma: Hatimaye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), yawasilishwa rasmi Bungeni

Terrible Teen

JF-Expert Member
May 1, 2017
916
2,634
Kufuatia chagizo na presha kubwa ikiwa ni pamoja na matakwa ya kikatiba, leo tarehe 10 Aprili ikiwa ni siku ya mwisho kwa mujibu wa Katiba, Serikali imewasilisha Bungeni taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kama ilivyotakiwa. Orodha ya shughuli za Bunge leo inaonyesha taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itawasilishwa bungeni.

Soma pia:

90CB8967-74EB-41E3-BFE7-21EDFF2156DA.jpeg

Kwa kufuatia hatua hiyo, Ofisi ya CAG sasa inaweza kuzitoa ripoti hizo katika tovuti yake ili Wananchi waweze kuzisoma na kuelewa fedha zao zimetumikaje. Ni suala la uwajibikaji tu, tunatoa heko kwa watu waliopiga kelele ili takwa hili la kikatiba litekelezwe.

Kwa upande wa Serikali, niwashauri wajifunze na waendelee kuheshimu Katiba. Kuna kikundi cha watu ndani ya Serikali kwa sasa wanampotosha kwa makusudi Rais ili wajipatie sifa , waache huo ujinga.

Kwa upande wa Bunge, nyie mmethibitisha kuwa dhaifu, wananchi hawana muda na Bunge kwa sasa, bora waangalie tamthilia ya SULTAN.

=======

Siku ya saba baada ya kuanza kwa mkutano wa 15 wa Bunge, chombo hicho cha kutunga sheria katika orodha ya shughuli za Bunge moja ya hati za kuwasilishwa ni taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, ambaye Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya naye kazi kutokana na kukiita chombo hicho dhaifu.

Dodoma. Leo Jumatano Aprili 10, 2019 Bunge la Tanzania litawasilishiwa hati ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.

Orodha ya shughuli za Bunge leo Jumatano, Aprili 10 inaonyesha taarifa hiyo ya fedha ya mwaka wa fedha 2017/18 itawasilisha bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisa ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ikiwa ni siku ya saba tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Aprili 2, 2019. Hata hivyo orodha hiyo inaweza kubadilika.

Wakati taarifa hiyo ikiwasilishwa, jana Jumanne, Aprili 9 jioni ofisi ya CAG ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa leo Profesa Assad atakuwa na mkutano na waandishi kueleza yaliyomo katika taarifa yake ya ukaguzi.

“Nawakaribisha katika ukumbi wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (Naot) ghorofa ya pili. Jengo lipo nyuma ya jengo la hazina (Dodoma). Karibuni nyote msihofu,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo ya mwaliko.

Hata hivyo, siku zote taarifa hiyo baada ya kuwasilishwa bungeni, CAG hukutana na wanahabari katika ukumbi wa Bunge kueleza yaliyomo katika ripoti yake ya ukaguzi, huenda safari hii ameamua kufanyia ofisini kwake kutokana na azimio la Bunge la kutofanya naye kazi.
 
Mkuu achana na Sultan bana, hivi unaanzaje kuikosa kuiangalia ili uangalie watu wanaobishana kama wapo kwenye kijiwe cha kahawa

“ᴬⁱⁿ̇`ᵗ ᵃ ʷᵒᵐᵃⁿ ᵃˡⁱᵛᵉ ᵗʰᵃᵗ ᶜᵃⁿ ᵗᵃᵏᵉ ᵐʸ ᵐᵒᵐᵐᵃ`ˢ ᵖˡᵃᶜᵉ”
 
Kufuatia chagizo na presha kubwa ikiwa ni pamoja na matakwa ya kikatiba, leo tarehe 10 Aprili ikiwa ni siku ya mwisho kwa mujibu wa Katiba, Serikali imewasilisha Bungeni taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kama ilivyotakiwa.

Kwa kufuatia hatua hiyo, Ofisi ya CAG sasa inaweza kuzitoa ripoti hizo katika tovuti yake ili Wananchi waweze kuzisoma na kuelewa fedha zao zimetumikaje. Ni suala la uwajibikaji tu, tunatoa heko kwa watu waliopiga kelele ili takwa hili la kikatiba litekelezwe.

Kwa upande wa Serikali, niwashauri wajifunze na waendelee kuheshimu Katiba. Kuna kikundi cha watu ndani ya Serikali kwa sasa wanampotosha kwa makusudi Rais ili wajipatie sifa , waache huo ujinga.

Kwa upande wa Bunge, nyie mmethibitisha kuwa dhaifu, wananchi hawana muda na Bunge kwa sasa, bora waangalie tamthilia ya SULTAN.
Mkuu Terrible Teens, tunaomba source vinginevyo huuni uongo.

Unless useme taarifa itawasilishwa leo na sio kusema imewasilishwa leo.

Source ya Kuwasilishwa kwa taarifa ya CAG ni order paper ambayo huwa inaanzwa kusambazwa saa 2:00, saa hizi saa 2:00 taarifa hii umeipata wapi?.

Uwasilishwaji wa Taarifa ya CAG, unafanyika kwa uwazi. Bunge linaanza saa 3:00 asubuhi, hivyo kama ni leo tutaona.

Na taarifa hiyo ya GAG ikiishapokelewa tuu mezani, hapo hapo taarifa hiyo inapandishwa online kwenye website ya NAO na kwenda viral.
P
 
Rombo imedinda tema madini wamumunye hohohoho,mbwa mkali cheni mbovu dedede

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huu ni uongo, unless useme taarifa itawasilishwa leo na sio

Source ya Kuwasilishwa kwa taarifa ya CAG ni order paper ambayo huwa inaanzwa kusambazwa saa 2:00, saa hizi saa 2:00 taarifa hii umeipata wapi?.

Uwasilishwaji wa Taarifa ya CAG, unafanyika kwa uwazi. Bunge linaanza saa 3:00 asubuhi, hivyo kama ni leo tutaona.
P
Mkuu Mayala, unabishana na anayeandaa ORDER PAPER? we elewa Ripoti zinaingia leo na sina sababu ya kusema uwongo hapa.
 
Na sikiliza ea radio hapa, Natha Kingu analiongelea.

Back
Top Bottom