Dodoma: Akamatwa kwa kufoji namba za gari (SU) na kusafirisha wahamiaji haramu

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Polisi Dodoma wanamshikilia Joachim Joseph wa Arusha kwa kusafirisha Wahamiaji 16 Waethiopia wasio na vibali kutoka Kilimanjaro akiwapeleka Mbeya kisha Afrika Kusini huku akitumia namba feki za SU kwenye Land Cruiser hii ili asisimamishwe, namba zake ni T752 BVL.

=====

Polisi Dodoma wanamshikilia Joachim Joseph mkazi wa Arusha kwa kusafirisha Wahamiaji 16 wasio na vibali ambao ni Raia wa Ethiopia wakitokea Mkoa wa Kilimanjaro kuelekea Mkoa wa Mbeya ili kuwavusha mpaka kelekea Afrika Kusini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi Martin Otieno amesema dereva huyu amekamatwa akiwa na gari aina ya Landcruser namba T 752 BVL lakini alitumia mbinu ya kufunga namba za Shirika la Umma ambazo ni SU 35970 ili asishtukiwe au kusimamishwa barabarani.

su.jpg
 
Hivi hao waethiopia wao South Africa wanapaona kama Newyork,kipi kinawashinda kuja na passport wakati wanaunguza mamillion kuitafuta Tunduma
Passport wataipata wapi Sasa? Na nani yuko tayari kugongesha passport yake kuruka nje ya nchi bila sababu maalaum/ya ulazima?

Mambo Sio malaini hivyo kwenye nchi nyingine hizi.

Tuendelee kumwagilia moyo.. Bongo raha sana.
 
Polisi Dodoma wanamshikilia Joachim Joseph wa Arusha kwa kusafirisha Wahamiaji 16 Waethiopia wasio na vibali kutoka Kilimanjaro akiwapeleka Mbeya kisha Afrika Kusini huku akitumia namba feki za SU kwenye Land Cruiser hii ili asisimamishwe, namba zake ni T752 BVL.

=====

Polisi Dodoma wanamshikilia Joachim Joseph mkazi wa Arusha kwa kusafirisha Wahamiaji 16 wasio na vibali ambao ni Raia wa Ethiopia wakitokea Mkoa wa Kilimanjaro kuelekea Mkoa wa Mbeya ili kuwavusha mpaka kelekea Afrika Kusini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi Martin Otieno amesema dereva huyu amekamatwa akiwa na gari aina ya Landcruser namba T 752 BVL lakini alitumia mbinu ya kufunga namba za Shirika la Umma ambazo ni SU 35970 ili asishtukiwe au kusimamishwa barabarani.

Watu 16 kwenye Landcruiser!!!
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Back
Top Bottom