Dkt. Tulia Ackson apitishwa kwa kauli moja na Wabunge wa CCM kugombea uspika

Kikao cha Kamati ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (cocas) kilichofanyika leo tarehe 31 Januari 2022 chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg. Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa na Waziri Mkuu wa JMT katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma kimempitisha kwa kauli moja Ndg. Dkt. Tulia Ackson kuwa Mgombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho.

Idadi ya wabunge waliopiga kura walikuwa ni 340 na walipiga kura za ndiyo au hapana.

Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Tanzania unatarajiwa kufanyika kesho tarehe 01 Februari 2022 katika Bunge la Tanzania/Bungeni jijini Dodoma.

Dkt. Tulia Ackson ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania. Kama atachaguliwa siku ya kesho kuwa Spika wa Bunge la Tanzania atakuwa ni mwanamke wa pili kushika wadhifa huo baada ya kutanguliwa na Ndg. Anna Makinda.

View attachment 2102737
Kamati ya Wabunge wa CCM (CCM Parliamentarians' Caucus)
 
Maigizo kama ya watoto wa chekechea. Tofauti ni kuwa haya yamejaa unafiki na yanaongozwa tamaa/uroho kuliko wa SHETANI.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom