Dkt. Tulia Ackson apitishwa kwa kauli moja na Wabunge wa CCM kugombea uspika

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Kikao cha Kamati ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (party caucus) kilichofanyika leo tarehe 31 Januari 2022 chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg. Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa na Waziri Mkuu wa JMT katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma kimempitisha kwa kauli moja Ndg. Dkt. Tulia Ackson kuwa Mgombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho.

Idadi ya wabunge waliopiga kura walikuwa ni 340 na walipiga kura za ndiyo au hapana.

Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Tanzania unatarajiwa kufanyika kesho tarehe 01 Februari 2022 katika Bunge la Tanzania/Bungeni jijini Dodoma.

Dkt. Tulia Ackson ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania. Kama atachaguliwa siku ya kesho kuwa Spika wa Bunge la Tanzania atakuwa ni mwanamke wa pili kushika wadhifa huo baada ya kutanguliwa na Ndg. Anna Makinda.

images (27).jpeg
 
Adamoo, Bwire, Lijenje na Ling'wenya siyo magaidi bali ni makomando wazalendo walio uzwa na luteni(Urio) wao mrafi na mroho wa pesa kwa watesi wake kina Kingai.

Sikudhani kama hii nchi yangu ya JMT kuna makomando wa hovyo kama huyu luteni Urio.
 
Bila shaka hakukuwa na mbunge mwanaume hata mmoja kwenye hicho kikao narudia BILA SHAKA.
 
Acheni wafu waongozane wao kwa wao.

Siku ujinga utakapowaisha watanzania ndo siku hiyo nzi wa kijani watakapogundua kuwa kumbe sehemu yao ya kuishi siyo kwenye nyumba bali chooni.
 
Dkt. Tulia Ackson ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania. Kama atachaguliwa siku ya kesho kuwa Spika wa Bunge la Tanzania atakuwa ni mwanamke wa pili kushika wadhifa huo baada ya kutanguliwa na Ndg. Anna Makinda.

Bi. Anna Makinda
 
Majitu ya CCM mapumbavu sana yani kazi kushikiwa akili yani wote mnapiga kura ya kumpitisha hata kama humtaki ndo chama kinamtaka. Poleni sana mbogamboga
 
Ndiyo anachuana na akiwemo yule mwenye degree 50

Ova
Ingekua hivyo ingekua poa Sana, hapo walikua wanapiga kura ya ndio kwa jina moja tu alafu wanaita uchaguzi. Bora hata kura ingekua ya ndiyo na hapana
Hii nchi ni kama tuna laana
 
Ingekua hivyo ingekua poa Sana, hapo walikua wanapiga kura ya ndio kwa jina moja tu alafu wanaita uchaguzi. Bora hata kura ingekua ya ndiyo na hapana
Hii nchi ni kama tuna laana
Kuna demokrasia ya vyama vingi na demokrasia ya chama kimoja, kuna uchaguzi wa watu wengi na wa mtu mmoja. Hakika huu ulikua ni wa mtu mmoja.
Wanaoafiki waseme ndioooooo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom