Dkt. Slaa: Sitta ni kielelezo cha mfumo uliooza, mlinda mafisadi na ufisadi

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amesema Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta ni mtu hatari ambaye CHADEMA kimegundua kuwa anaweza kufanya lolote kupata madaraka.

Dk. Slaa alisema Sitta hatakiwi kuaminiwa kwa kuwa hata alipokuwa spika, huku akiwa mwana CCM, mara kadhaa alijaribu kuomba kujiunga na CHADEMA iwapo CCM ingemtosa.

"Huyu mtu haaminiki hata katika dhamira yake, kwa kuwa tulikutana zaidi ya mara 100 na hata tukawa tunaandikiana vimemo, yeye akiwa katika kiti cha spika. Kama anabisha leo akanushe juu ya uhaini wake dhidi ya CCM," alisisitiza Dk. Slaa.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana mjini Iringa wakati akizungumza na waandishi wa habari, akijibu kauli iliyotolewa na Sitta aliyedai kwamba CHADEMA hakijastahili kupewa madaraka kwa kuwa hakina watu wenye uzoefu wa uongozi.

Sitta alidai mwenye uzoefu wa uongozi ndani ya CHADEMA ni Dk. Slaa pekee; akashutumu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kwamba uzoefu pekee alionao ni kuongoza kumbi za disko.

Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), na ambaye yumo katika fitina za kimakundi ya wanaoutaka urais ndani ya CCM, alisema hayo mjini Karagwe wiki hii, kama njia ya kijikweza mbele ya umma; na kuwashusha viongozi wa CHADEMA, ambacho chini ya uongozi wa Mbowe kimejengeka kuwa chama kikuu cha upinzani kinachotishia kuiondoa CCM madarakani.

Akijibu hoja hiyo, Dk. Slaa alidai kuwa mara kadhaa walizokutana, Sitta akiwa Spika wa Bunge alimweleza kuwa ana kundi la wabunge 55 waliokuwa tayari kuondoka katika CCM, na kwamba wangefanya hivyo siku tatu kabla ya Bunge la mwaka 2010 kumalizika.

CHANZO: GUMZO LA JIJI
 
Hii mbona sio siri..kila mtu anajua kwamba sitta ndio alikua awe mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kwa tikiti ya chadema,kweli vikao vingi kumbembeleza kama alivyokiri kiaina dk. slaa vilifanyika,na ni kweli pia kulikua na wabunge wengi ambao ilikua wamfuate sitta,hapa pia wapo watu kama Nape ambae nae alikua njia moja,na wote walidhamiria kufanya hivyo baada ya kuona ccm wakati ule ilikua imemezwa na ufisadi na mafisadi kina LOWASSA huku JK akionekana kuwapenda zaidi mafisadi hao kuliko wapiganaji kina sitta,mwakyembe,selelii,mama kilango,mzee shelukindo,victor mwambalaswa,saidi mkumba,ole sendeka,mpendazoe n.k.

Baadae ya kina sitta kung'atwa sikio na jk kwamba anataka kujivua na kuivua ccm gamba ufisadi na mafisadi na anawategemea wao katika hilo ndio wakaona kumbe wanaongea lugha moja,kukisafisha chama na kukitoa mikononi mwa mafisadi na kukirejesha kwa wenye nacho ambao ni wakulima na wafanyakazi,hivyo wakaamua kughairi na kufuta mpango wao wa kwenda chadema au ccj.

Ndio maana mnaona hizi hasira na povu jingi la chadema dhidi ya wabunge hao niliowataja,na zaidi Nape na SITTA wanaona aliwaangusha sana maana hawakuandaa mgombea urais wakimtegemea yeye.Baada ya sitta kuwaangusha ndio zikaanz jitihada za kumbembeleza slaa na kumuahidi pesa zake za ubunge na stahili zote za ubungo chama -chadema kitakua kinamlipa jambo ambalo linatekelezwa mpaka leo,slaa akanushe kama halipwi marupu rupu yote kama mbunge na chadema,ntamwaga data za uthibitisho zikiwemo payment voucher alizoweka sahihi yake.Wanasiasa ni wa waongo sana na wamekuwa wakitutumia tu wananchi.Slaa aeleze ukweli wote kuhusu sakata la sitta na ahadi ya ugombea urais kwa tiketi ya chadema,asichague ya kuongea kama ameamua kusema aseme yote,vikao zaidi ya 100 na kada wa ngazi za juu wa ccm walikua wakizungumza nini nae?
 
Duh, propaganda ndani ya propaganda. Wenye akili hatuambiwi tunafikiria na kupembua pumba na mchele.

Asanteni lakini.
 
MIMI NILIDHANI UNAKANUSHA KUMBE ALIYOSEMA DK SLAAH NI KWELI!!??

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
KIM KARDASHI,
naona unajichanganya mkuu wangu!! Ilikuwaje Dr haaidiwe/alipwe pesa na anaendelea kulipwa pesa hadi leo(kwa maneno yako) na akina Sitta wakati unasema aliwatosa!!?

Alishawatosa, sasa wanaendelea kumlipa pesa na malupulupu mengine kwa misingi ipi!!?
 
Nimeanza kuamini DR Slaa anavuta mshiko wa ubunge kama kawaida. Nilikuwa najiuliza inakuwaje Dr. Slaa atulie kimya baada ya matokeo tata ya uraisi!! Wanamageuzi tulitegemea atoe angalau tamko kufuatia matokeo baada ya kura kuhesabiwa, tofauti na tulivyozoea.
 
Sita ni mnafiki hafai hata kupewa ubalozi wa nyumba kumi. Sababu ya utawala wa JK kuyumba kwa kiasi kikubwa kunachangiwa na ufitini wa sita na kutaka kujionyesha yeye na kikundi chao kikiratibiwa na nape (Kinaonyeshwa kwenye Blog ya CCM) ni wasafi kuliko viongozi wengine wote. Lakini kimsingi ndio huyo Sita alifisadi Fedha ya Bunge kwa kujenga Nyumba ya gharama kubwa jimboni kwake akiita nyumba ya Spika, akidhani ni life speaker. Aidha hadi leo pamoja sio speaker anang'ang'ania kukua kwenye makazi ya speaker msasani. Huyo huyo anasema ni mpinga ufisadi. Kama anaona chama ni cha kifisadi ahamie kwingine, vinginevyo awakemee wenzake kwenye vikao vya ndani sio anazunguka mkoani kujipatia umaarufu wa kitoto
 
Dr Slaa our terminator!!!!!!!!!!!!!!!! Sita yani ameshuka mpaka sifuri
 
SITA by 2015 atakuwa political reject kama akina Malecela na wengineo wengi.Mtu anafikiria uraisi wakati hata jimbo limemshinda,Urambo ni wilaya ya mwishomwisho kimaendeleo katika Tanzania,hajawahi kusaidia chochote jimboni kwake zaidi ya kujijengea ofisi ya kifahari katikati ya nyumba za wakazi za tope ambazo zipo hadi katikati ya mji.Mji hauna maji na barabara za vumbi kila kona,ukiingia tu Urambo unapata feeling ya umaskini wa kutupwa,atumie huu muda uliobaki kabla ya kustaafu kabisa hiyo 2015 asaidie watu wake na aache kuuota uraisi,
 
Gwand zinaposhikwa baya hutoa harufu ya Kikwapa?

Slaa alikuwa wapi kabla? asiseme yote hayo mpaka aliposhikwa pabaya?
 
Dr Slaa anapiga kelele za nini wakati hata yeye mwenyewe aliasi ccm

Tofauti ni kuwa yeye aliasi na amebaki na uasi dhidi ya CCM hadi leo. ...Au unadhani magamba hayajamfuata na ahadi za uwaziri kama yalivyomfuata Sitta?
 
Gwand zinaposhikwa baya hutoa harufu ya Kikwapa?

Slaa alikuwa wapi kabla? asiseme yote hayo mpaka aliposhikwa pabaya?

CDM hawakurupuki kama Nape. Ameshasema hawapendi kuongelea mtu bali wanapenda kuongelea issues. Ila unapowachokoza kuattach personal issues wanamajibu tena muafaka kama haya. Si unakumbuka Makamba alivyodisappear kiaina alipoambiwa ataje mwenyewe sababu za kufukuzwa ualimu? Mambo mengine yanahitaji timing mkuu si kuropoka tu.
 
Hii mbona sio siri..kila mtu anajua kwamba sitta ndio alikua awe mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kwa tikiti ya chadema,kweli vikao vingi kumbembeleza kama alivyokiri kiaina dk. slaa vilifanyika,na ni kweli pia kulikua na wabunge wengi ambao ilikua wamfuate sitta,hapa pia wapo watu kama Nape ambae nae alikua njia moja,na wote walidhamiria kufanya hivyo baada ya kuona ccm wakati ule ilikua imemezwa na ufisadi na mafisadi kina LOWASSA huku JK akionekana kuwapenda zaidi mafisadi hao kuliko wapiganaji kina sitta,mwakyembe,selelii,mama kilango,mzee shelukindo,victor mwambalaswa,saidi mkumba,ole sendeka,mpendazoe n.k.

Baadae ya kina sitta kung'atwa sikio na jk kwamba anataka kujivua na kuivua ccm gamba ufisadi na mafisadi na anawategemea wao katika hilo ndio wakaona kumbe wanaongea lugha moja,kukisafisha chama na kukitoa mikononi mwa mafisadi na kukirejesha kwa wenye nacho ambao ni wakulima na wafanyakazi,hivyo wakaamua kughairi na kufuta mpango wao wa kwenda chadema au ccj.

Ndio maana mnaona hizi hasira na povu jingi la chadema dhidi ya wabunge hao niliowataja,na zaidi Nape na SITTA wanaona aliwaangusha sana maana hawakuandaa mgombea urais wakimtegemea yeye.Baada ya sitta kuwaangusha ndio zikaanz jitihada za kumbembeleza slaa na kumuahidi pesa zake za ubunge na stahili zote za ubungo chama -chadema kitakua kinamlipa jambo ambalo linatekelezwa mpaka leo,slaa akanushe kama halipwi marupu rupu yote kama mbunge na chadema,ntamwaga data za uthibitisho zikiwemo payment voucher alizoweka sahihi yake.Wanasiasa ni wa waongo sana na wamekuwa wakitutumia tu wananchi.Slaa aeleze ukweli wote kuhusu sakata la sitta na ahadi ya ugombea urais kwa tiketi ya chadema,asichague ya kuongea kama ameamua kusema aseme yote,vikao zaidi ya 100 na kada wa ngazi za juu wa ccm walikua wakizungumza nini nae?

1) Du! wenzake wanabembeleza kuteuliwa tena mpaka kwa rushwa, lakini yeye kumbe alibembelezwa? .....Hii ni sifa ambayo hata baba wa taifa aliitaja.
2) Hivi Dr analipwa kama Mbunge? this is too low? ukilinganisha na status yake katika jamii na kazi anayoifanya. He deserves far more than that. Chama inabidi kireview kipato chake.
 
Back
Top Bottom