Dkt. Slaa: Nilijiona ndani ya moyo wa Rais Magufuli

Weee ni kichaaa hamtakaa mfute legacy ya Magufuli Kwa sababu ya ukabila wenu na uchu wa Madaraka.Magufuli ni icon ya uongozi uliotukuka kwa kizazi hiki cha nyoka itachukua mia
💯 kumpata rais aliyejali wanyonge
Usisahau na legacy ya kukwapua tril. 1.5 na kwenda nayo Chato.
 
Kama bado kuna wanasiasa wachache Wazalendo Ambao nawakubali basi Dr Slaa naye yumo.

Pamoja na Kipenzi chetu Magufuli kulala. Bado tuna imani Mungu Atatuinulia Magufuli Mwingine Ambaye Atakuja kumalizia Kazi Njema Ambayo Alitufanyi Magufuli.
 
"Kupitia Rais Magufuli tulipata sauti ya Wanyonge,alikuwa Mwanademokrasia wa kweli na mpenda haki
Duh. Dr. Slaa ameshachanganyikiwa kabisa. Nadhani atakuwa na stress sana, hasa baada ya kutelekezwa na kila mtu, kuanzia mke, serikali, chama, nk. Demokrasia ipi anayoongea?
Mungu amsamehe tu ampe kuzeeka vizuri.
 
DAKTARI SLAA;NILIJIONA NDANI YA MOYO WA RAIS MAGUFULI.

Hayati Rais Magufuli aliwapenda na kuwapigania watu wa hali ya chini,mfano sasa hivi vitu vinapanda bei na gharama ya kupanda bei haimuumizi tajiri bali mlaji wa mwisho,katika walaji wa mwisho kuna matajiri wachache na masikini wengi,ambapo vitu vikipanda bei mishahara yao haipandi,Hayati Rais Magufuli alipinga vitu kupanda bei ili wasimuumize mwananchi wa hali ya chini ambae ndie mlaji wa mwisho.

Nukuu za Daktari Wilbroad Slaa.

"Rais Magufuli alikuwa na mchango pekee katika kuikumbatia amani kwa kupitia kuyaunganisha makundi ya dini,Rais Magufuli hakuacha kushiriki kumuomba Mungu iwe kanisani au msikitini,tukiacha kutambua hilo,tutakuwa tumefanya Jambo baya sana".

"Rais Magufuli alienda mbali sana katika kuheshimu dini,ni pale alipokwenda mbele ya kanisa katoliki tena bila kuomba kibali akachangisha fedha kwa ajili ya kujenga msikiti,Rais Magufuli alikuwa ni kiongozi,sifa ya kwanza ya kiongozi ni kuwaunganisha wananchi"

"Serikali mlitukosea kwa kutunyima nafasi ya kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Baba yetu aliyetupenda (Hayati Rais Magufuli) kipindi alipokuwa anaumwa kwa kushindwa kutoa taarifa"

"Kila sehemu alipopelekwa Rais Magufuli kwa ajili ya kuagwa Watanzania walishikamana kwa majonzi makubwa na kujitokeza kuonesha upendo wai,kila aliyekuwa anasema Rais Magufuli alikuwa na maadui wengi,nilikuwa nawapigia simu nawaambia hebu fungua television yako uone umati wa watu wakimuaga Rais wao kipenzi,Hayati Rais Magufuli"

"Sisi ni binadamu na tuna mapungufu yetu lakini ukiona umati wa watu kama ule waliojitokeza kumuaga Rais Magufuli ujue kuna kitu,kupitia umati ule kama una moyo unaofunguka kwa jicho la imani ulipaswa kujua Rais Magufuli alikuwa ni mtu wa aina gani".

"Kwa wasiojua ni kwamba Dk Slaa hana chama chochote cha siasa,tangu nilipojiuzulu lakini katika masuala ya Taifa Mimi bado ni Mtanzania na nitatoa kauli yangu kuhusu masuala yanayohusu Taifa langu"

"Magufuli alikuwa ni mtu ambae akishakuamini anaweka imani yake katika moyo wako na hatafuti makandokando yako,ataanza kutafuta makando kando yako akianza kusikia maneno mengine,lakini haizuii kugeuka"

"Kabla ya Rais Magufuli,tulifika katika nchi ambayo kiongozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) alikuwa na wasichana 200 na wote alikuwa anawanunulia gari,hata mchwa wanakula lakini hawawezi kula namna hiyo"

"Magufuli alikuwa ni Mzalendo na mwana wa kweli wa Afrika,na hili hatutaki kutambua,ni kawaida ya wahunzi hata chungu alichotengeneza, nyumbani kwake hakithamini,wenzetu Afrika nzima walimthamini Hayati Rais Magufuli na wangependa awe Rais wao"

"Wote tuko sawa,mfano tu nchi za Afrika zifunge bandari zao,Ulaya kule viwanda vitafungwa,ajira zitakosekana na watu watagombana kwa kuwa malighafi hazitakuwepo,kwa namna hiyo sisi ni matajiri"..

"Tulichokosa Waafrika ni kujiamini,mtu mwenye kujiamini hata kama hauna kitu,utafanya kitu na utapata kitu,ile kauli ya We are donor Country tulipaswa kuiendeleza"

"Rais Magufuli alihamasisha tufanye kazi,asiyefanya kazi na asile,hayakuwa tu maneno ya Magufuli bali yalikuwa ni maneno kutoka ndani ya Biblia"

"Ukiingia Ikulu meza ya ofisi ya Rais Magufuli,huwezi kutegemea unakuta mafaili mengi lakini meza ya Rais Magufuli ilikuwa imejaa mafaili,alikuwa anafuatilia ndio maana aligundua mengi, kwenye halmashauri walikuwa wanalipa mishahara ya watu waliofariki miaka kumi iliyopita kwa hali hiyo ulitaka Rais Magufuli afanyeje"

"Wakati nikiwa Katibu Mkuu wa Chadema,nililetewa taarifa kuwa kuna madawa ya kulevya yanasafirishwa usiku wa leo point x,kwa nia njema nikawapa taarifa wakubwa Serikalini,kumbe huyo mkubwa mtoto wake ni mbia katika biashara hiyo,nafurahi Hayati Rais Magufuli aliipiga vita biashara hiyo na alisema haiwezejani watoto wetu watoke makamasi ili watoto wao wakasome Ulaya"

"Kupitia Rais Magufuli tulipata sauti ya Wanyonge,alikuwa Mwanademokrasia wa kweli na mpenda haki, wamachinga walipewa vitambulisho na wakafanya biashara ya halali,je uko si kutenda haki!? Mama ntilie waliruhusiwa kuuza barabarani,je uko si kutenda haki!!? Au haki hadi watendewe wakubwa!?.
Huyu mzee wasipo harakisha kumpeleka kwenye matibabu si muda atavua nguo hadharani
 
Hajui kwamba huyu mtu wake aliikuta sukari ikiwa 1500 na amekufa akaiacha imeshuka mpaka 280/300?
Kwa akili hizo unadhani chadema angepawezaje mpaka leo?

Alafu huyu mzee muongo sana, Magufuri alizuia vitu kupanda bei?

Au kwa sababu yeye alikuwa Canada na mushumbushi wake hajui jinsi vitu vilivyopanda bei?

Sio Magufuri aliyewaambia wakulima mkiona Kuna njaa uzeni mazao kwa bei kubwa mnayotaka.
 
Nafikiri tupige kura hapa. Tuna sample ya kutosha.
Kuna watu bado hawaamin kwamba Magufuli alikuwa anapendwa sasa ngoja uchaguzi ufike halafu atokee mgombea aseme yeye ataofuata nyayo za JPM uone shangwe Lake.
 
Ukisoma "between the lines" katika kauli alizozitoa Dkt. Slaa utaona kuna shida sehemu fulani. Anatambua fika kabisa kile anachokisema kinakosa uhalisia.

Ijapokuwa anajitahidi kutoa sifa kwa mwendazake, lakini nyuma ya kauli zinaonyesha dalili za upweke, kutengwa, kuathirika na usaliti kwa Mbowe na CDM, ama hata pia kutaka upendeleo au kufikiriwa katika ajira na awamu ya sasa iliyopo madarakani.

This is a perfect quagmire, a fallen man from greater heights.
Yes,a free fall from greater heights
 
Nadhani hujui Politics..., JPM aliweza kuwagawa watu kuna waliompenda kindakindaki, pia zile propaganda zake ilionekana kwamba tulikuwa kwenye njia sahihi (na sababu ameondoka kabla ya muda) na walioingia kuna mambo yanafanyika inaonekana huenda alikuwa ana point na huenda alivyokuwa anasema tunaibiwa na sasa yanayotokea huitaji expert wa conspiracy theory kuonyesha kwamba JPM alikuwa anaongea ukweli (hata kama ilikuwa kweli au sio kweli); Hivyo wanasiasa watumia matukio wanaweza kusema zile ndoto na ile ahadi aliyowaahidi JPM mimi nitaitekeleza...,

Mfano issue ya Machinga haikuwa sustainable kwa muda mrefu kuendelea kubangaiza mitaani (wala haikuwa kuwatetea sababu kulikuwa hakuna sera ya kuboresha maisha yao na kuondokana na uchuuzi wao) ila wao waliamini hivyo kwamba huyo ndio anayewatetea na bila huyo wangeishi kama wakimbizi (sasa bado huoni kwamba kuna mtaji wa kura hapo)? By the time wanashituka kwamba hakuna kinachoendelea miaka mitano au kumi imepita amekuja kiongozi mwingine...

Hizo ndio siasa zetu piga uongo na Propaganda pata madaraka, fanya vitu vidogo vidogo vya kuonekana leo na sio muda mrefu hayo ya kesho muachie mwingine...
Huo mtaji wa kura unaujua ww lkn Kwa katiba hii na ccm hawategemei kura za kundi lolote mfano ni ule uchafuzi wa 2020 kura hazikua na maamuz yeyote
 
Back
Top Bottom