Dkt Mwigulu Madelu Nchemba nampa mwaka mmoja tu kama hajahamishwa au kutumbuliwa Wizara ya fedha na uchumi

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
184
987
Nimejaribu kuangalia pamoja na teuzi nzuri za Mama yetu Mpendwa Rais Samia Suluhu, lakini kwenye wizara nyeti hii ya fedha haijapata watu sahihi. Ndugu yangu Dkt Mwigulu Nchemba ni msomi lakini siye anayetumia usomi wake katika kuchanganua mambo ya kiuchumi na biashara anazidiwa na Zitto Kabwe au Silinde. Hakika hii wizara haihitaji mwanasiasa typical, inahitaji mtu aliyetulia, asiyekua mjanja mjanja, asiye na Visasi,asiye na roho ya kuwazika kila wakati. Mwigulu na Hamad Msauni wote wanauwaza urais 2025, Concentration ya uwaziri itatoka wapi?

Mama kama hajamtimua au kubadilishia Mwigulu wizara ndani ya miezi 6 au mwaka mmoja basi tutarudi kuja kuambizana humu ndani ya mwaka mmoja. Ndugu yetu kutawala hisia zake ni mgumu sana halafu reactions zake nyingi hata mitandaoni zinajulikana.

Mwigulu hamfikii Dkt Philipo Mpango hata 1%. Hii wizara kiukweli haijapata mtu sahihi. Mama majibu utayapata kupitia Makamu wako na muda utaongea.

Anyway, Sina chuki binafsi na ndugu yangu Mwigulu Nchemba lakini kila ninapoyatazama maslahi mapana ya taifa langu naona ni bora kuusema ukweli. Mambo mengine ni hulka hata kubadilika ni ngumu ilitakiwa apewe wizara ya Vijana na mambo ya bunge.
 
Hata mimi nimeshangaa kweli. Halafu jambo lingine kila teuzi mbona watu ni wale wale ina maana bunge la watu 300+ hakuna wenye uwezo kuzidi hao!
 
Naunga mkono hoja!

Lakini kudumu kwa Mwigulu katika sekta hii ni wazi kabsa CV yake ya kuchukua Nchi 2025 itakuwa kubwa sana.
 
Sanasana mabasi ya esther yataongezeka barabarani na singida united itarudi ligi kuu, kwa wizi nasikia yuko vizuri
 
Hiyo ndo kazi ambayo watu wa upinzani mnatakiwa kuifanya, namaanisha kupiga ramli kila wana CCM wanapokabidhina madaraka na kubadilishana kama hivi.

Lile swala la kutawala hii nchi kwenu litabaki story.
Watu wakitoa mawazo yao ni wapinzani. Kweli kabisa wapinzani hawatatawla hii nchi maana, CCM 70% ya malengo yao ni kubaki madarakani 30% ndio ya kuwatumikia wananchi.
 
Dr Mpango ndo atakua amempendekeza huyo msanii.!
Hajakosea

Ila kama mwenye mamlaka (Mh. Samia) hamtaki basi

Mwigulu mwenyewe wala si kwamba anapambania vyeo, yanayotokea kwenye mitandao ni ya watu baki (his fans and non fans)
 
Hata mimi nimeshangaa kweli..halafu jambo lingine kila teuzi mbona watu ni wale wale ina maana bunge la watu 300+ hakuna wenye uwezo kuzidi hao..!
Hao wana visu vikali (connection) zaidi kuliko hao wenzao wengine wanao piga tu vigelegele na kuitikia Ndiyoooo!!!.
 
Hata mimi nimeshangaa kweli..halafu jambo lingine kila teuzi mbona watu ni wale wale ina maana bunge la watu 300+ hakuna wenye uwezo kuzidi hao..!

Mfano msukuma wa geita ungempa wizara gani, kule hakuna na hawatoshi ndio maana bingwa alikuwa anasajili kwa mkopo
 
  • Thanks
Reactions: me1
Hujui ulichoandika. Mwenzio katoa hoja wewe unaleta habari ya upinzani.
Jibu hoja kwa kujenga hoja.
Sasa kuna hoja gani ya msingi hapo ya kujadiliwa, zaidi ya ramli za kijinga?

Huyo anaetaka Mwigulu atumbuliwe ukute hata cheti cha form four hana,furaha yake ni kuona watu wengine wanalia maisha magumu kama yeye.
 
Back
Top Bottom