Dkt. Mpango: Sitakuwa mpole kwa wanaochezea Muungano

Akizungumza kwenye Kongamano la Miaka 57 ya Muungano Jijini Dodoma, Dkt. Philip Mpango amesema katika kipindi chake kama Makamu wa Rais, hatokubali Muungano kuchezewa

Amesema, "Sitakubali kabisa wanaochezea Muungano wetu adhimu. Kuna baadhi ya mambo huwa watu wanasema mimi ni mpole. Watakaojaribu kuchezea Muungano hapo sitakuwa mpole"
Sawa ila tunataka muungano WENYE kutoa fulsa sawa,sio wazanzibar, sie tuwapende,lakini tukienda huko hatupati fulsa sawa kuanzia ajira,ardhi, na kupata nafasi za kisiasa,sie tulisha kubali kua ndugu,Sasa tupate fulsa sawa, so mh mpango anza na haya,
 
Akizungumza kwenye Kongamano la Miaka 57 ya Muungano Jijini Dodoma, Dkt. Philip Mpango amesema katika kipindi chake kama Makamu wa Rais, hatokubali Muungano kuchezewa

Amesema, "Sitakubali kabisa wanaochezea Muungano wetu adhimu. Kuna baadhi ya mambo huwa watu wanasema mimi ni mpole. Watakaojaribu kuchezea Muungano hapo sitakuwa mpole"
Makamu wa Rais hana uwezo wowote wa kucharukia mitazamo kinzani vinginevyo iatafitinishwa mpaka ataomba pooh

Makamu wa Rais hatakiwi kuwa 'harsh' kapewa 'tray' ya mayai mkononi akionesha ukali upande wowote kwisha habari yake.

Mh Dr. Mpango hucharuka tu endapo amehakikishiwa na mwenye mamlaka kufoka (rejea kwenye suala ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa DSM PC Makonda kuhusu kontena la vifaa kwa ajili ya shule mpaka leo kufoka kote haijulikani penati ilifungwa kwa mtindo wa majaro au chumba cha adhabu)

Majukumu ya makamu wa Rais sio utendaji (executive) so he just spoke it out to gesture his presence as the immediate stateperson's aide.
 
Raisi anatukimbusha jinsia yake nadhani kuna watu hawajui jinsia ya raisi. Mpango anatukumbusha kua yeye ni mkali kiuhalisia ni mpole saana. Kazi tunayo
 
Tena awe mkali kwelikweli. Kuuchezea muungano ni kosa kubwa
Halafu jichunguze sana kama upo sawa kichwani huwezi ukawa unaunga mkono kila kitu kinacholetwa na viongozi wa ccm utakua una shida kichwani. Mtu aliyekamilika kifikra anatambua baya na zuri.jichunguze sana.
 
Mpango hajui kazi za makamu wa Rais..
Huyu jamaa sijui vipi. Kwa mara ya tatu sasa on camera anairudia hii kauli ya “wanasema mimi mpole” and all that nonsense

Hivi huyu anayajua kweli majukumu ya VP au ndio yaleyale ya kusubiri kupangiwa cha kufanya na Rais, ambaye kwa bahati mbaya sasa huyu wa sasa na yeye hana uhakika wa nini anapaswa kufanya?
 
Halafu jichunguze sana kama upo sawa kichwani huwezi ukawa unaunga mkono kila kitu kinacholetwa na viongozi wa ccm utakua una shida kichwani. Mtu aliyekamilika kifikra anatambua baya na zuri.jichunguze sana.

Ulitaka nimpinge makamu wa rais ili wewe ufurahi? Au unataka asiwe mkali ili mumwite dhaifu???

Mwenye shida ni wewe unayepinga kila kitu lakini bado unaishi ndani ya serikali hiyo hiyo. Wenzio wamepinga na kuhamia ubelgiji wewe unapinga halafu unasubiri kutibiwa amana na muhimbili..
Unapita kwenye barabara unazopinga na kutumia na na umeme unaoupinga. Hebu tumia ubongo kuwaza buana, wewe mkubwa ujue!?

Tusipangiane imani....

Mfyuuuuuuu
 
Back
Top Bottom