Dkt. Mpango: Rais Samia anakerwa na mauaji yanayotokea nchini. Ameagiza Jeshi la Polisi kufanya msako kubaini wanaojiuhusisha na vitendo vya mauaji

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,941

Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango, ametoa siku 7 kwa Jeshi la Polisi likiongozwa na IGP Simon Sirro, kufanya uchunguzi wa mauaji ya watu watano wakazi wa Kata ya Zanka, kijiji cha Zanka jijini Dodoma yaliyotokea hivi karibuni.

Dkt Mpango ametoa maagizo hayo hii leo Januari 26, 2022, mara baada ya kutembelea eneo lilipofanyika tukio hilo na kutoa pole kwa wafiwa.

Aidha Dkt. Mpango, amelielekeza jeshi hilo kufanya misako nchi nzima ili kuwabaini wote wanaojihusisha na vitendo vya mauaji kwani, Taifa limechafuliwa na vitendo hivyo vya kikatili na vya kinyama.

=====

Rais Samia Suluhu Hassan ameelezea kukerwa na mauaji yanayoendelea huku akimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Simon Sirro, kuchukua hatua kukomesha vitendo hivyo.

Pia ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuwakamata watu wote waliohusika na mauaji ya kikatili ya watu watano wa familia moja katika kijiji cha Zanka, Bahi mkoani hapo.

“Tukio hili la watu watano wa familia moja kuuawa na watu wasiojulikana na kutelekezwa ndani ya nyumba halikubariki na linaumiza sana. Hivyo basi, Rais Samia amenituma nije kutoa pole. Natoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kuanzia leo (jana) kuhakikisha watu wote bila kuachwa hata mmoja, wanakamatwa na taarifa iletwe kwa Rais,” alisisitiza Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango kwa niaba ya Rais.
Alisema watu wote waliohusika katika tukio hilo la kinyama polisi iwasake popote walipo bila kuacha mtu.

“Mkuu wa Mkoa pamoja na kamati yako ya ulinzi na usalama naagiza ndani ya hizo siku saba watu wote wawe wamekamatwa na kupata stahiki ya kufikishwa mahakamani, nawataka mhamie katika kijiji hiki hadi hapo mtakapo wakamata watu wote waliohusika na tukio hili,” alisema Dk. Mpango.

Pia aliiagiza Idara ya Upelelezi kuongeza nguvu katika eneo hilo na kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo ndani ya muda alioutoa.

“Inashangaza sana nyumba ipo hapa, lakini kuna majirani kweli walishindwa hata kusikia sauti au kushtuka kwanini wenzao hawaonekani kwa siku tatu na hapa kuna zizi la mifugo na ilikuwa inakwenda kuchungwa na watu wanakamua maziwa mpaka miili ya wenzao inaharibika na kutoa harufu ndipo wanashtuka, natumaini vyombo vya usalama hawa watu pia wanaisaidia polisi hata kama ni ndugu,” alisema.

Akizungumzia mauaji mengine ya kikatili yanayoendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya nchini, alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Sirro kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wanayakomesha.

“IGP yupo hapa, kama hayupo nakuagiza RPC umfikishie maagizo haya nataka kuanzia leo matukio ya mauaji ya kikatili yanayoendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya nchi yanakomeshwa, tumechoka kuendelea kuongoza nchi ambayo kila siku kuna taarifa za watu kuuana na vyombo vya usalama vipo.

“Leo mchana tu nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari nimesikia mauaji yamefanyika Mtwara na watuhumiwa ni askari polisi, lakini Mbeya baba kauawa, mtuhumiwa ni mwanawe mwanajeshi na kule Moshi mama kauawa mtuhumiwa binti yake, Jeshi la Polisi mnayo kazi ya kufanya, Rais amechoka mimi nimechoka, hatuwezi kuendesha nchi namna hii,” alisisitiza Dk. Mpango.

Aliwataka Watanzania kupendana na kuacha chuki zinazosababisha matukio ya mauaji ya kinyama. “Viongozi wa dini nawaomba mtumie nyumba za ibada kuongea na waumini, hakuna mtu mwenye haki ya kuondoa uhai wa mwenzake leo hii hata simba wenyewe hawauani, lakini sisi tunafanya mambo ya wanyama,” alisema Dk. Mpango kwa masikitiko.

Pia alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Mnkunda, kuitisha mkutano wa hadhara na wanakijiji wa eneo hilo ili kujadiliana masuala ya ulinzi na usalama.

“Wana Zanka mmenisikitisha sana mimi, hivi hamfahamu kuwa ni mkazi wa kata hii naogopa hata kusema nina shamba hapa, nchi nzima wameifahamu Zanka, lakini kwa sifa ya mauaji, inatishia sana hasa kwa nchi yetu ambayo inasifika kwa amani na utulivu sasa watu wataogopa hata kulala ndani ya nyumba zao.”

Miili ya familia hiyo iliyouawa, ilikutwa ndani ya nyumba yao Januari 22, mwaka huu, ikiwa imeanza kutoa harufu baada ya kuanza kuharibika.

Pia soma:
- Dodoma: Watu 5 wa Familia moja wauawa (January 23, 2022)
 
Kafa ndio sasa haya mauji yanatoka wapi wakati mlishangilia kifo chake mkisema sasa mnapumua?
Mauaji yalikuwepo kabla ya kristo, wakati wa kristo na baada ya kristo...

Huu uhuni nchini ulikuwepo kabla na baada ya ukoloni.

Hakuna aliyeshangilia kifo cha Magufuli kula limao kupunguza hangover ya Magufuli.

CHUI JIKE ananguruma sasa.
 
Mauaji yalikuwepo kabla ya kristo, wakati wa kristo na baada ya kristo...

Huu uhuni nchini ulikuwepo kabla na baada ya ukoloni.
...
Si wewe humu kila siku mpaka leo unashangilia wewe na wenzio mnasema mnapumua hamuawi wala kutekwa tena?
 
Hata mimi yale majitu kama yaliyoko jela kwa ugaidi nafurahia sana uwepo wao pale
Yes thats the reality of the world. Ni kama vile ulivyofurahia na kunywa mvinyo wakati Lissu katandikwa risasi ndivyo nami nilivyoangusha Ng'ombe siku yule kichaa alivyokula kifusi pale chattle.

Kuimba na kulia ni kwa kupokezana.
 
Back
Top Bottom