Dkt. Mpango: Kodi si tatizo Bandarini

Dkt. Mpango: Kodi si tatizo Bandarini

Hivi kweli kabisa tumekosa washauri wazuri wa uchumi kwa nchi yetu?
Nchi ambayo 50% ya mapato yake inatumiwa kulipa mishahara na bado Kuna watu wana jeuri.....
Inasikitisha kafeli uchumi na ni ishara kwamba ataendela kufeli kwa miaka mitanoi
 
Natafakari kwa sauti:
J. K. Nyerere alibana kwa kiasi chake,
A. H. Mwinyi akaachie kidogo,
B. W. Mkapa nae akaja akabana,
J. M. Kikwete akalegeza, sasa kaja
J. P. Magufuli... mwendo ndo kama ulivyo.. Mie nadhani ni nyakati tu zinaongea. Wote wamefanya/wanafanya kwa kadri ya utashi waliojaliwa na Mungu. Tumpe muda JPM.
 
Ni bora kuwa na mizigo michache inayolipiwa kodi kuliko kuwa na lundo la mizigo ya mafisadi isiyolipiwa kodi. Hapa kazi tu
 
Vitabu vyote vya dini vinaeleza kuwa Mungu wetu anataka mwenye dhambi yoyote atubu ili kama alikuwa akiishi kama shetani aishi kama Malaika.

Mwenyezi Mungu hatamani binadamu yeyote aishi kama shetani.

Tumeshangaa tumepata Presidaa ambaye ametangaza hadharani kuwa atawafanya watanzania waishi kama mashetani........

Sasa nchi yetu naona Mwenyezi Mungu ameanza kuipiga laana kutokana na matamshi hayo ambayo yanaenda kinyume kabisa na matakwa ya Mungu ya kutotaka binadamu yoyote hata kama alikuwa na dhambi kiasi gani asiishi kama shetani, badala yake atubu dhambi zake na aweze kuishi kama Malaika.

Na viongozi wetu wa dini hata kidogo kukosoa kauli tatanishi wao wako kimya. Penye makosa lazima ukweli usemwe. Siyo sahihi kumshusha aliye juu ili aje chini. Ni sahihi aliye chini kumpandisha. Katika hili mimi binafsi naona haiko sawa.
 
japo amekurupuka, ni mapema sana kupima uhai kwa bandari kwa miaka 3 au 5 ijayo.

mbegu lazima ioze ili iote.
 
Bandari. Ilikuwa ina kazi nyingi, mizigo mingi, wafanyazi walikuwa busy, lakini mapato ya bandalini yalikuwa yakiwekwa mifukoni. Wakubwa wa custom wengine walikuwa na nyumba 75. Wafanya biashara waliokuwa wakigawana pesa hizi wafanyakazi majipu sasa wanashock, shock ikiisha na kufanya biashara kwa sheria za nchi mambo yatakuwa sawa.
 
Hiyo ndio hali halisi na ndio ukweli wa bandari yetu mizigo mingi ilikuwa hailipiwi kodi hivyo ni bora wasije kabisa...!

Naipongeza serikali kwa hatua hii ya kudhibiti kwa sasa tunajua kabisa tunapata mizigo ya aina gani na kiasi gani.. Nina hakika kwa sasa mtu akiagiza gari lake hato ibiwa...!
hapo unachangia,huku machozi yakikulenga lenga!
 
Acha ujinga! Taarifa za upungufu wa mzigo bandarini hazitokani na VAT. Comparatively gharama zetu ziko chini kuliko bandari zingine. Ukweli ni kwamba mizigo iliyokuwa inafurika ilikuwa ya Mafisadi na ilikuwa hailipiwi kodi! Sasa wamekwama! Ni bora ije michache lakini walipe! Upotoshaji wa UKUTA ni propaganda useless!!
Kwenye Maelezo Yangu Kuna Sehemu Nilipolitaja Neno VAT?
 
Bandari. Ilikuwa ina kazi nyingi, mizigo mingi, wafanyazi walikuwa busy, lakini mapato ya bandalini yalikuwa yakiwekwa mifukoni. Wakubwa wa custom wengine walikuwa na nyumba 75. Wafanya biashara waliokuwa wakigawana pesa hizi wafanyakazi majipu sasa wanashock, shock ikiisha na kufanya biashara kwa sheria za nchi mambo yatakuwa sawa.

Safi sana.

Ni lazima sheria na taratibu zifuatwe.
 
Na viongozi wetu wa dini hata kidogo kukosoa kauli tatanishi wao wako kimya. Penye makosa lazima ukweli usemwe. Siyo sahihi kumshusha aliye juu ili aje chini. Ni sahihi aliye chini kumpandisha. Katika hili mimi binafsi naona haiko sawa.
Wakikosoa nyinyi ndio wa kwanza kuwaambia wa-deal na waumini wao. Hii nchi ina wanafiki balaa!
 
Hali hii imepelekea uongozi wa mamlaka ya bandari kufuta bandari kavu hii ni baada ya wafanya biashara kuikimbia.
Mamlaka ya Bandari nchini TPA imesema inakabiliwa na upungufu wa mizigo ambapo sasa kwa siku inahudumia magari 1500 tu tofauti na uwezo wake wa kuhudumia magari 3500 kwa siku yatokayo nje ya nchi na kuwa kutokana na hali hiyo hawawezi kupeleka magari kuhifadhiwa bandari kavu kwani hata yenyewe haina mzigo wa kutosha.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Deusdedit Kakoko amesema hayo baada ya kumalizika kikao kilichoitwa cha ndani kati yake na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini kilicholenga kujua hali halisi ya bandari ilivyo na mipango yake ya kuiboresha.

Aidha mkurugenzi mkuu huyo wa mamlaka ya Bandari amesema kulikuwepo na udanganyifu katika utoaji wa mizigo bandarini kwa baadhi ya mawakala wa forodha ambao mzigo wa kupeleka nje ya nchi ulikuwa ukiuzwa hapa nchini kitu ambacho kimekanushwa vikali na chama cha mawakala wa forodha.

Awali katibu wa jukwaa la wahariri Neville Meena amesema walifika bandarini hapo na kufanya kikao cha ndani na uongozi wa bandari hiyo baada ya kuwepo alichokiita mtikisiko katika utoaji wa huduma katika mamlaka ya bandari nchini.

Chanzo itv

Kutoka magari 3500 hadi 1,500 tathmini je kati ya magari 3500 mangapi yalikuwa yanalipia ushuru, hatuwezi kusema magari yanayohudumiwa kwa sasa kuwa ndio yalikuwa yanalipiwa ushuru na ambayo hayapo hayakuwa yanalipiwa la hasha lazima tuweke makadirio kama magari 2500 hivi ndio yalikuwa yanalipiwa. Sasa swala lingine ni kwamba kati ya hayo magari 1500 yapi ni ya transit maana yake hayalipiwi ushuru wa hapa nchini lazima yatakuwa kama 800 maana nimewahi kufika bandarini kuona magari ambayo hawa wageni wanayatoa ni mengi sana. Tukubali lazima kuna shoti ya ushuru je serikali itaendelea kutegemea ushuru wa viwanda vya ndani na kodi za wananchi tukizingatia hatuna viwanda kiivyo lol hapa KAZI KUBWA ni kufikiria jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kuendesha serikali maana DENI ambalo serikali inalipa nje ni kubwa sana Eh mwenyezi MUNGU TUSAIDIE.
 
Hiyo ndio hali halisi na ndio ukweli wa bandari yetu mizigo mingi ilikuwa hailipiwi kodi hivyo ni bora wasije kabisa...!

Naipongeza serikali kwa hatua hii ya kudhibiti kwa sasa tunajua kabisa tunapata mizigo ya aina gani na kiasi gani.. Nina hakika kwa sasa mtu akiagiza gari lake hato ibiwa...!
Siyo suala la udhibiti. Kama ilikuwa ni suala la udhibiti wa ulipaji wa kodi, uchambuzi ulifanywa na kugundua tatizo ni mlipa kodi au au sera ya kodi? Nielewavyo mimi tatizo ni tozo jipya la VAT ambayo halihitajiki kwa mizigo inayopitia bandari yetu kwenda nchi za jirani.

Kama kwenu hakuna bandari sawa; lakini mimi naelewa bandari ni kitega uchumi na kina wajibu wa kimataifa kwa nchi zisizo bandari zinazopakana na nchi yenye bandari. Azimio la UN linataka nchi yenye bandari kupitisha mizigo ya nchi zinazopitisha mizigo yao kwa tozo za kodi za haki na halali. VAT si haki wala halali kutozwa kwa transit good.

Hayo ni ya CCM pekee.
 
Hivi mizigo ya wizi inaumhimu gani wa kuwepo ni bora ibaki michache ambayo unalipa kodi hakuna namna nyingine.
 
Kwenye Maelezo Yangu Kuna Sehemu Nilipolitaja Neno VAT?
Nakufundisha ujue hill kwa kuwa unawaunga mkono wazembe kwenye uvivu wa kufikiri. Amka wewe!! Unakosoa kitu usichokijua. Ndio tunakufundisha hivyo ukawaekeze kwenye kijiwe chenu pale!!
 
Kutoka magari 3500 hadi 1,500 tathmini je kati ya magari 3500 mangapi yalikuwa yanalipia ushuru, hatuwezi kusema magari yanayohudumiwa kwa sasa kuwa ndio yalikuwa yanalipiwa ushuru na ambayo hayapo hayakuwa yanalipiwa la hasha lazima tuweke makadirio kama magari 2500 hivi ndio yalikuwa yanalipiwa. Sasa swala lingine ni kwamba kati ya hayo magari 1500 yapi ni ya transit maana yake hayalipiwi ushuru wa hapa nchini lazima yatakuwa kama 800 maana nimewahi kufika bandarini kuona magari ambayo hawa wageni wanayatoa ni mengi sana. Tukubali lazima kuna shoti ya ushuru je serikali itaendelea kutegemea ushuru wa viwanda vya ndani na kodi za wananchi tukizingatia hatuna viwanda kiivyo lol hapa KAZI KUBWA ni kufikiria jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kuendesha serikali maana DENI ambalo serikali inalipa nje ni kubwa sana Eh mwenyezi MUNGU TUSAIDIE.
Hayo ni makadirio yako ambayo umekadiria wewe.
 
Back
Top Bottom