UncleBen, naamini unajua kabisa kuwa ukishaona nchi inatetea na kutegemea Kodi pekee kama source of income ni tatizo kubwa sanaaa.
Nchi zote zilizoendelea ziliwekeza kwenye Agriculture na viwanda, viwanda hivi vyetu vitaendeshwa kwa source gani of energy? Umeme huu wa kusuasua hata bila viwanda?
Hili la kodi litaumiza watanzania wengi.
Mkuu kuna jambo halipo sawa huko juu kwenye mamlaka zetu ,ama watu wanajua wanachokifanya au nao wameamua kukaa kimya bora yaende ,
Kila mwisho wa mwezi TRA wanakuja kwa mbwembe nyingi kutuambia sijui mapato ya mwezi ni trilion na ushee ,wakati huo hakuna vyanzo vipya vya kodi ,wateja ndio hivyo bandarini wanakimbia ,Hili la viwanda hata sitaki kuliongelea ule ulikua uongo mtupu tu watu wapate kura zao ,
Kilimo kwanza kilikufa kibudu kabla hatujajua ni wapi tulikosea ,unaskia watu serikali yangu haitoi chakula cha msaada ,
Sawa mapato yapo mbona mmesimamisha ajira ?
Wanaotakiwa kupandishwa mshahara pia tatizo
Hela tu za field za kuwapa wanafunzi mmekosa mmeishia kuwapa nusu ....
Lakini utasikia Nataka Chato kiwanja kijengwe mara moja ,au lazima kabla ya September wizara zote ziwe Dodoma
Bana watajua wenyewe acha tuwe watazamaji