OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,021
- 114,387
HATUA ya kupungua kwa mizigo inayotoka nje ya nchi kwenye Bandari ya Salama haitokani na ongezeko la kodi, anaadika Regina Mkonde.
Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mpango amesema kuwa, pamoja na kuwepo kwa madai kwamba, mizigo kutoka nje ya nchi imepungua kutokana na ongezeko la kodi “kauli hii si ya kweli.”
Dk Mpango ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa uorodheshwaji wa hisa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mpango amefafanua kuwa, kuyumba kwa soko la China ndiyo sababu ya mizigo hiyo kupungua kwa kuwa, Tanzania inashirikiana na nchi hiyo katika masuala ya kiuchumi.
“Muangalie uchumi wa China unavyokwenda, soko lake limepungua ulimwenguni, kutokana na sababu ya nchi kuwa na ushirikiano wa kiuchumi na china kumeathiri.
Kodi haiathiri chochote kile, na kelele zote zinazoendelea zinafanywa na wale wakwepa kulipa kodi.
“Waambie waache porojo, waende kwenye takwimu, hata kwa nchi jirani ya Kenya mizigo inayoingia imepungua kwenye Bandari ya Mombasa. Waende wakapate ripoti.”
Amesema kuwa, serikali ipo makini na wafanyabishara ambao hawataki kulipa kodi.
“Walipe kodi tu ili serikali iweze kuwahudumia, haiwezekani bandari itoe huduma kwa wafanyabiashara pasi na wao kulipa kodi, hapana.”