Hiyo ndio hali halisi na ndio ukweli wa bandari yetu mizigo mingi ilikuwa hailipiwi kodi hivyo ni bora wasije kabisa....!
kwa experience ya wengi upande wa magari ICD's binafsi kuna usalama zaidi,na gari unaikuta intactNaipongeza serikali kwa hatua hii ya kudhibiti kwa sasa tunajua kabisa tunapata mizigo ya aina gani na kiasi gani.. Nina hakika kwa sasa mtu akiagiza gari lake hato ibiwa...!
Sio kufuta! Ni kusisitisha kutokana na makubaliano yao kwamba ikiwa bandarini kuna mizigo basi babdari kavu watapata kazi vinginevyo ni kinyume chake! ITVHali hii imepelekea uongozi wa mamlaka ya bandari kufuta bandari kavu hii ni baada ya wafanya biashara kuikimbia.
Chanzo itv
Wengine hawapo kwenye TV mkuu.Mbona haraka ivo usha post huku
Utasafirisha kwa ndegeKama meli hazitakuja tutawezaje kuuza mbaazi...?na msimu ndio huu umekwisha anza wanunuzi ni wa huko India sisi hapa nchini hatutumii Mbaazi ila kidogo hivi , ukizingatia mbaazi hazivumilii wadudu ni rahisi sana kushambuliwa na wadudu kama meli haziingii nchini Zitasafirishwaje....?
I dont believe hili...Waondoke tu,majitu yalikuwa hayalipi kodi hayo
Sababu Ni udikteta uchwara
UncleBen, naamini unajua kabisa kuwa ukishaona nchi inatetea na kutegemea Kodi pekee kama source of income ni tatizo kubwa sanaaa.Hivi ni kodi tu kupanda ama kulipwa ndio ikimbize wateja wote ?? Aisee kuna kitu hakipo sawa hapa
Hilo ndiyo tatizo la nchi kuendeshwa kwa staili ya ONE MAN SHOW.....
Hashauliki wala haambiliki.......................
Kila kitu anataka kutoa maagizo yeye tu na hataki mtu yoyote atoe sababu zozote za kutotekelezwa kwa maagizo yake......
Tulimsikia JPM akitamba kuwa wacha hizo meli ziende kwenye hizo bandari za nchi ambazo wanazokubali bandari zao kupitisha mizigo bila kulipa kodi!
Lakini Mkuu wa nchi angetakiwa kuwa msikivu zaidi ili kujua sababu halisi za kupungua mizigo bandarini badala ya kufanya conclusion kuwa mizigo hiyo imepungua kutokana na wale waliokuwa hawalipi kodi kuhamishia mizigo yao kupeleka kwenye bandari za nchi nyingine zinazoruhusu bandari zao kupitisha mizigo bila kulipa kodi!
Kauli nyingine ya kibabe ya Mkulu ni ile ambayo alitoa kuwa watalii wasiotaka kulipa VAT waliyoianzisha ni bora wasije nchini, kwa kuwa yeye anataka watalii matajiri wenye uwezo wa kulipa kodi!
Kwa ubabe huo wa Presidaa wetu tayari sekta ya utalii nayo ishapata athari kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa watalii wanaoingia nchini.....
Naamini kwa mwendo huu nchi yetu inaelekea kuwa Zimbabwe nyingine, kwa kuwa hulka ya Rais wetu inashabiana sana na yule Mzee asiyetaka kung'atuka kule Zimbabwe.........
Chama kidumMsijali watanzania, Magufuli atawaletea Tanzania ya asali, maziwa na viwanda! Hiyo ndiyo Tanzania ya Magufuli.. CCM hoyeee
