Uchaguzi 2020 Dkt. Mahera: Tume inaweza kuwafungia kufanya kampeni wagombea wa vyama wanaosambaza matusi badala ya sera

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Charles Mahera amesema kwamba "Kama tume tunaweza kuamua kuwafungia hata kufanya kampeni, wagombea wa vyama ambao kazi yao ni kusambaza matusi na sio sera kwa kuwa sheria ipo na imetaja adhabu, tunatoa rai wabadilike na kuzingatia maadili ya uchaguzi waliyosaini"

''Kama watu walikuwa wamemchagua mtu atatangazwa kama kashinda, hatumtangazi mtu kwa shinikizo la watu, watu wauze sera zao ili wananchi wawachague kwa manufaa yao na si ya watu wa nje'

Dkt. Mahera ameyasema hayo kwenye kikao na watoa huduma ya Habari Mitandaoni leo Sep 15, 2020, ambapo pia amewataka kutumia kalamu na taaluma yao kulinda amani ya nchi kwa kufuata miongozo na taratibu za kutangaza habari za uchaguzi mkuu.

NEC.jpg
 
Back
Top Bottom