Uchaguzi 2020 Dkt. Mahera: Kuna watu wana chokochoko, wasimamizi wa uchaguzi fuateni sheria kuepuka shari

Tafadhali aliye jirani / karibu na Mkurugenzi huyu wa NEC tena ( Poti wangu kabisa ) wa 'Kizanaki' aniulizie kwanini hii takwimu ya Idadi kamili ya Vituo vya Kupigia Kura nchi nzima inabadilika badilika?

Leo tumetajiwa ni 81,567 ila Wiki iliyopita niliona mahala sasa sijui ile 'Takwimu' aliitoa Yeye au labda hicho Chombo cha Habari cha Mtandaoni 'Kilikengeuka' ambapo idadi yake niliona ni 81,511. NEC wawe nalo makini sana hili.
Labda kwa mujibu wa PhD ya hesabu hakuna tofauti.
 
Huyu Mahera kitambo sana ameshaingia kwenye 18 za Bensouda.
Mchana anasisitiza kufuata sheria lakini gizani anawaagiza wakurugenzi kuminya haki za watu. Tunamwambia, mkurugenzi atakayeminya haki za mawakala atakuwa anatutafuta maneno sisi raia na atayapata! Mkurugenzi atakayedhulumu haki za mawakala anatafuta ugomvi mpatieni huo ugomvi!!
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt.Wilson Charles amewaagiza wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria ili kuepuka malalamiko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Dkt.Charles ametoa agizo hilo wakati anafungua mafunzo ya uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo Kanda ya Ruvuma yenye mikoa ya Njombe, Ruvuma,Mtwara,Lindi,Iringa na Mbeya.Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

“Kama unavyoona Taifa letu sasa hivi kuna baadhi watu wanachokochoko sana,kwa hiyo mjitahidi kufanya kazi kwa kanuni na sheria za uchaguzi ili kuepuka shari ya watu hao’’,alisisitiza Dkt.Charles.

Amesema hadi sasa NEC imeshatuma sehemu kubwa ya vifaa vya kufanikisha uchaguzi Mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu na kwamba vifaa hivyo vimekwishaanza kusambazwa na inatarajiwa hadi kufikia Oktoba 24 kila Halmashauri nchini itakuwa imepokea vifaa vyote vya uchaguzi.

Amewashauri wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo kuanza kuvipakua vifaa hivyo na kuvisambaza katika maeneo yote na kwamba wasisubiri hadi Oktoba 27.

“NEC katika uchaguzi wa mwaka huu tunataka kuwa tofauti ukilinganisha na mwaka 2015,kwanza serikali imetuletea fedha zilizotokana na kodi za walipa kodi kwa wakati,hivi tunavyoongea zaidi ya shilingi bilioni 120 nimezishusha ngazi ya Halmashauri’’,alisisitiza Dkt.Charles.

Amewataka wasimamizi hao kufikisha vifaa vya uchaguzi ngazi ya Kata kwa wakati ili wale ambao wamezoea kulalamika kuwa NEC imechelewa kufungua vituo na kuchelewesha vifaa katika uchaguzi wa mwaka huu wakose cha kusema.

Kwa mujibu wa Dkt. Charles,kuanzia Oktoba 24 hadi 26 NEC itaanza kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo,wasimamizi Wasaidizi wa vituo na makarani waongozaji.

“Wasimamizi wa majimbo,mnatakiwa kuyapa umuhimu mkubwa na wa kipekee mafunzo haya hasa kwa kuzingatia kuwa watendaji mtakaowafundisha ndiyo watakaosimamia zoezi la upigaji kura na kuhesabu kura vituoni’’,alisema Mkurugenzi wa NEC.

Dkt.Charles pia amewaagiza wasimamizi wa majimbo kuwaapisha mawakala wa vyama vya siasa ifikapo Oktoba 21 mwaka huu na kusisitiza kuwa vyama vya siasa ambavyo vitaleta mawakala muda ukiwa umekwisha, mawakala wake hawataapishwa na hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura.

Mkurugenzi huyo wa NEC amesema daftari la kudumu la wapigakura lina jumla ya wapigakura milioni 29,188,347 na kwamba katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kutakuwa na vituo 81,567 vya kupigia kura kwa nchi nzima.

Amesisitiza kuwa baada ya wapigakura, kupiga kura zao sheria inawataka kuondoka vituoni na kurudi nyumbani kusubiri matokeo. na kwamba hakuna sheria inayosema wabaki vituoni.

Gaspar Balyomi ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tunduru,akizungumza baada ya kupata mafunzo hayo ameahidi kusimamia maelekezo yote ya NEC ili kuhakikisha wananchi wanapiga kura katika vituo husika kwa uhuru na kurudi nyumbani kusubiri matokeo.

Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mbinga Mji Grace Quintine amesema mafunzo hayo yamewakumbusha kuzingatia kanuni na sheria za uchaguzi tangu kuanza kwa mchakato wa kuelekea uchaguzi Mkuu.

Mimi sijaelewa. Kwa hiyo mtu ukiishapiga hauruhusiwi kwenda sehemu yeyote tofauti na nyumbani na ukae nyumbani kusubiri matokeo? Kwa hiyo mtu ukienda kanisani, kwa kinyozi, hospitali, kazini, beach, kuangalia mpira kwa jirani n.k. unaweza kushtakiwa kwa kuvunja sheria? Na ukitoka nyumbani kwenda kazini au sehemu nyingine kabla ya matokeo kutangazwa nako utakuwa umevunja sheria? Mbona wanatuchanganya?

Amandla......
 
Hivi kwa tume kujiamulia kuwapeleka mawakala wa vyama katika vituo watakavyoamua tume wenyewe, si kwamba wanawapotezea hawa mawakala haki yao ya msingi ya kupiga kura?
Inaonekana hujui. Ukweli ni kwamba, Tume imeagiza vyama viwapangie mawakala wao vituo,ndipo waende kuapishwa.
 
Kwa maelezo niliyosikia akiyatoa Lissu juzi ni kuwa pamoja na vyama kupendekeza vituo vya hao mawakala, tume bado ina uwezo wa kubadilisha wapi hao mawakala waende. Ndiyo maana akawa anasema wanaweza kucheleweshwa kwa makusudi kufika katika vituo vyao.
 
Ajitahadhari, bado ni kijana midogo. Uchaguzi ukichafuka yeye ndiye wa kwanza kulaumiwa na wa kwanza kwenda The Hague.
 
Kwa nini Tume inaogopa kusaidiwa na wenye nchi(wananchi) kulinda vituo vya kupigia kura,kuna shida gani wakisubiri matokeo hapo hapo??
 
👇🏽👇🏽👇🏽Mambo ni 🔥
It's simple -unaandika HELLO kwenda namba hiyo +16202675770
Na hatujuani huko inawezekana hata jirani yako au mwenza wako yuko humu, hamtambuani! Uzuri hata ujumbe ukituma hawaoni DATA PROTECTION ya hali ya juu
Mwambie na mwenzako!
#TutaelewanaTu #Uchaguzi2020
 
Sisi hapa Geita tumejiandaa na kidumu cha Petroli iwapo Upendo na Lissu wasipotangazwa hiyo 28 msimamizi atatutambua
Kila siku huwa nawaambia dawa ya hao jamaa ni vidumu tu,mapolisi hawawezi kuwepo kila kwenye Mali zao ikiwemo nyumba.Unajua chama chakavu kimebaki na wazee na wamama wote waoga
 
Mimi sio kama nilikuwa nahamasisha Vurugu la hasha ila Chadema ikishinda halafu walete mchezo wa kuiba ndio wataona moto
Mimi nilikuwa CCM kwa miaka mingi na sasa nimehamia Chadema mbinu zao nazijua sasa waache Wananchi waamue
 
WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI ZA MAJIMBO KWENYE MIKOA YA SINGIDA NA DODOMA NA MOROGORO WANATOA MAELEKEZO YA KUIPENDELEA CCM TENA MA ARO KATA WAPO KWENYE PRESHA KUBWA NEC HAPA MUWE WAANGALIFU KWENYE MIKOA HII

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt.Wilson Charles amewaagiza wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria ili kuepuka malalamiko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Dkt.Charles ametoa agizo hilo wakati anafungua mafunzo ya uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo Kanda ya Ruvuma yenye mikoa ya Njombe, Ruvuma,Mtwara,Lindi,Iringa na Mbeya.Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

“Kama unavyoona Taifa letu sasa hivi kuna baadhi watu wanachokochoko sana,kwa hiyo mjitahidi kufanya kazi kwa kanuni na sheria za uchaguzi ili kuepuka shari ya watu hao’’,alisisitiza Dkt.Charles.

Amesema hadi sasa NEC imeshatuma sehemu kubwa ya vifaa vya kufanikisha uchaguzi Mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu na kwamba vifaa hivyo vimekwishaanza kusambazwa na inatarajiwa hadi kufikia Oktoba 24 kila Halmashauri nchini itakuwa imepokea vifaa vyote vya uchaguzi.

Amewashauri wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo kuanza kuvipakua vifaa hivyo na kuvisambaza katika maeneo yote na kwamba wasisubiri hadi Oktoba 27.

“NEC katika uchaguzi wa mwaka huu tunataka kuwa tofauti ukilinganisha na mwaka 2015,kwanza serikali imetuletea fedha zilizotokana na kodi za walipa kodi kwa wakati,hivi tunavyoongea zaidi ya shilingi bilioni 120 nimezishusha ngazi ya Halmashauri’’,alisisitiza Dkt.Charles.

Amewataka wasimamizi hao kufikisha vifaa vya uchaguzi ngazi ya Kata kwa wakati ili wale ambao wamezoea kulalamika kuwa NEC imechelewa kufungua vituo na kuchelewesha vifaa katika uchaguzi wa mwaka huu wakose cha kusema.

Kwa mujibu wa Dkt. Charles,kuanzia Oktoba 24 hadi 26 NEC itaanza kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo,wasimamizi Wasaidizi wa vituo na makarani waongozaji.

“Wasimamizi wa majimbo,mnatakiwa kuyapa umuhimu mkubwa na wa kipekee mafunzo haya hasa kwa kuzingatia kuwa watendaji mtakaowafundisha ndiyo watakaosimamia zoezi la upigaji kura na kuhesabu kura vituoni’’,alisema Mkurugenzi wa NEC.

Dkt.Charles pia amewaagiza wasimamizi wa majimbo kuwaapisha mawakala wa vyama vya siasa ifikapo Oktoba 21 mwaka huu na kusisitiza kuwa vyama vya siasa ambavyo vitaleta mawakala muda ukiwa umekwisha, mawakala wake hawataapishwa na hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura.

Mkurugenzi huyo wa NEC amesema daftari la kudumu la wapigakura lina jumla ya wapigakura milioni 29,188,347 na kwamba katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kutakuwa na vituo 81,567 vya kupigia kura kwa nchi nzima.

Amesisitiza kuwa baada ya wapigakura, kupiga kura zao sheria inawataka kuondoka vituoni na kurudi nyumbani kusubiri matokeo. na kwamba hakuna sheria inayosema wabaki vituoni.

Gaspar Balyomi ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tunduru,akizungumza baada ya kupata mafunzo hayo ameahidi kusimamia maelekezo yote ya NEC ili kuhakikisha wananchi wanapiga kura katika vituo husika kwa uhuru na kurudi nyumbani kusubiri matokeo.

Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mbinga Mji Grace Quintine amesema mafunzo hayo yamewakumbusha kuzingatia kanuni na sheria za uchaguzi tangu kuanza kwa mchakato wa kuelekea uchaguzi Mkuu.

Ni bahati mbaya sana tume ya uchaguzi kuongozwa na mtu wa aina ya Dk Mahera.
 
Back
Top Bottom