Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Siwezi kudanganya watumishi wa umma kuwa nitawapandishia mishahara!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Hayo ameyasema Leo akiwa mkoani Mara kwenye kampeni za kuomba kuchaguliwa kwa miaka mitano ijayo.

Ahadi hii imeniacha na maswali mawili Kama ifuatavyo: 1 Je huyu mgombea anawachukuliaje watumishi wa umma? Huwaona Kama wanaokula bure?, au makondoo tu wasio na lolote.! 2 Nini mtazamo wa watumishi juu ya ahadi hii?
========

DKT. MAGUFULI: Ukaacha kujenga reli ambayo italeta uchumi mkubwa, ukasema naipeleka hii kupandisha mishahara. Huwezi ukaacha kujenga vituo vya afya, tumejenga katika nchi nzima vituo vya afya 487. Wanaotibiwa sio wakulima na wafanyabiashara, hata wafanyakazi wanatibiwa pale.

Kwa hiyo tuliamua hiyo fedha iende kwa kujenga vituo vya afya na dispensary zaidi ya elfu moja na kitu, hospitali za wilaya 99 na hospitali za rufaa zaidi ya tatu. Hizi hospitali zinawatibu pia wafanyakazi, zinawatibu pia watoto wa wafanyakazi.

Tumeamua kutoa elimu bure kwa watoto wetu kuanzia darasa la kwanza mpaka sekondari na mikopo ya chuo kikuu tukaiongeza mpaka bilioni 450 ili mtoto wa masikini nae aweze kupata mkopo atakapokuwa chuo kikuu.

Tumitumia trilioni 1.06, hizi fedha tungeweza tukawadanganya wafanyakazi tukasema tumewaongeza mishahara, kupanga ni kuchagua, tuliamua watoto wasome bure kwanza.

Sisi wafanyakazi tunawapenda na ndio maana tunatoa hizi huduma, ndio maana katika ilani ya uchaguzi inazungumzia juu ya maslahi ya wafanyakazi.

 
Magufuli hafai kuwa kiongozi wa watu.

Huyu anafaa kuwa mnyampala wa wajenga barabara; hii kazi aliyopewa imemzidi kimo!!!
Anasema hawezi kuwaongeza mishahara kwasababu gani? Anadhani hawa Watumishi wanaishi vipi wakati hali ya Maisha inakuwa ngumu [ mahitaji muhimu kupanda bei] lakini ,mshahara umeganda pale pale toka aingie madarakani 2015!!!! Sasa hawa wakifanya vitendo nya ufisadi ili kukidhi mahitaji muhimu utawalaumu?
 
Back
Top Bottom