Tukiwa na watu wenye weledi kama ww na kufanya uchambuzi wa mambo kama hivi naamini kuwa Watanzania wengi watapata uelewa na kufahamu mengi sana.
Mimi ni angazie suala la Bajeti nakumbuka Mh Magufuli wakati wa kampeni alikuwa anatuaminisha kuwa Tanzania ni Nchi tajiri tunaweza kufanya mabadiriko makubwa sana katika Uchumi wetu tukaubadiri kutoka ulivyo sasa kuja kuwa uchumi wa Viwanda, naamini hivi sasa kishaanza kujua kuwa jitihada zaidi zinahitajika ili Nchi ibadirike kutoka ilipo kwenda kwenye uchumi wa Viwanda.
Suala la makusanyo ya Kodi hadi hivi sasa naona lina suasua maana tulikuwa tunatangaziwa makusanyo kila mwezi, ila kwa sasa naona wamesimamisha kutangaza nafikiri ni baada ya kuonekana mapato yanashuka kila mwezi.
Tukubaliane tu kuwa tuna safari ndefu ya kujenga Nchi yetu si yeye pekee Mh Raisi kuwa ndiye atakaye tupeleka katika mafanikio ni Watanzania wote bila kujali Vyama, kabila,jinsia, ukanda wala dini ndiyo wenye jukumu hili.
Mungu ibariki Tanzania.