Dkt. Kigwangalla afungua duka la maziwa Kunduchi Mtongani, asema sasa anajikita kwenye ufugaji

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,965
141,968
Dkt. Kigwangalla ambaye ni waziri mstaafu wa Serikali ya awamu ya 5 amesema kwa sasa amejikita kwenye ufugaji kwa kuwa ujasiriamali unalipa kuliko kitu kingine chochote.

Kigwangalla amesema kwa sasa anamiliki shamba kubwa la mifugo huko Mvomero mkoani Morogoro ambako anazalisha ng'ombe wa kisasa akiwa amejikita kwenye uzalishaji wa madume ya mbegu na maziwa.

Jijini Dar es salaam amefungua duka la maziwa maeneo ya Kunduchi mtongani linalosimamiwa na mke wake.

Dkt. Kigwangalla amewataka vijana kujikita kwenye ujasiriamali wasisubiri ajira kwani ushindani wa ajira ni mkubwa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Watu wenye akili tunajua Dr.Kigwangwala yuko busy kwa sasa kufungua miradi yenye lengo la kutakatisha pesa alizopiga akiwa waziri wa utalii ili huko mbele ya safari tusijiulize kapata wapi pesa. Ni mbinu za kawaida sana za watawala na wanasiasa.

Kama huamini subiri utaona.
 
Watu wenye akili tunajua Dr.Kigwangwala yuko busy kwa sasa kufungua miradi yenye lengo la kutakatisha pesa alizopiga akiwa waziri wa utalii ili huko mbele ya safari tusijiulize kapata wapi pesa. Ni mbinu za kawaida sana za watawala na wanasiasa.

Kama huamini subiri utaona.
Mhhhhhh
 
Tabia za Wanadamu

Kuna makundi mengi Sana ya tabia za watu, mfano

1. Watu wanaokosea na kukiri na kuomba msamaha

2. Watu wanaokosea na wasikiri Kama wamekosa ila wakikaa pembeni wanakubali wamekosa kimya kimya na kujirekebisha bila kuomba msamaha

3. Watu ambao huamini wao hawakosei yani wanachoamini wao ndo sahihi, hawakili na hawajutii maamuzi yao
 
Back
Top Bottom