Dkt. Kigwangalla aliwashia moto gazeti la Jamhuri kwa 'kumchafua'

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Kigwangalla.jpg

Waziri wa Maliasili na Utalii, na Mbunge wa Nzega Vijijini, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amechukua hatua za kisheria kwa wahariri na wamiliki wa gazeti la Jamhuri kwa madai kuwa wamekuwa wakimchafua katika machapisho yao.

Ambapo amechukua hatua ya kuwaandikia barua na amewataka wamuombe radhi kwenye machapisho mawili ya gazeti hilo yatakayotoka ukurasa wa mbele, na yawe yanafuatana au kutoa fidia ya shilingi milioni 500 kwa kuchapisha habari ambayo hawakuwa na uhakika nayo na akidai kuwa wamemchafua na kumzushia uongo.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na kampuni ya Uwakili ya FMD Legal Consultants &Advocates kwa Gazeti hilo amesema kuwa kwenye makala iliyotoka tarehe 12 – 18 Novemba 2019 waliandika makala yenye kichwa cha habari ‘WANASWA UHUJUMU UCHUMI’, ndani yake ilihusisha kampuni za Kitalii za Ker and Downey, chini ya makampuni ya Friedkin, na gazeti hilo lilimtaja Dkt. Kigwangalla kwa jina na kwa cheo kuwa anawalinda kampuni hii dhidi ya makosa yao ya kikodi.

Waraka huo wa madai, ambao umevuja kwenye mitandao ya kijamii, unasema kuwa gazeti hilo lilichapa habari hizo bila kuwa na uhakika nazo, wakijua ni za uongo na walifanya hivyo kwa makusudi kwa malengo ya kumchafua Dkt. Kigwangalla ambaye ni mtu mwenye heshima kubwa na mamlaka ndani ya jimbo lake, Chama Chake na nchi yote’

Na kwamba walisambaza sana kwenye mitandao ikiwemo ya kijamii bila hata kufanya uthibitisho wa habari zenyewe wala kumuuliza Dkt. Kigwangalla ambaye anatuhumiwa.

Hata hivyo waraka huu, ambao umewafikia gazeti la JAMHURI tarehe 6 January 2020, umekutana na gazeti lingine la JAMHURI la tarehe 7 January 2020, likiwa limemuandika tena Dkt. Kigwangalla.

Zaidi soma:

IMG-20200106-WA0043.jpg

IMG-20200106-WA0044.jpg

IMG-20200107-WA0015.jpg


====
Wanajamvi
Salam;

Nimesoma makala ya gazeti la Jamhuri kuhusu kashifa ya waziri wa maliasili na utalii.

Baadae mchana nimeona taarifa ya waziri kigwangala ya kulitaka gazeti liombe radhi.

Nadhani nchi yetu ina tatizo kubwa sana kwenye mfumo wa Elimu yetu. Huyu Hamis ni daktari wa Binadamu kitaaluma,ukisoma taarifa ya gazeti la Jamhuri ni habari nzito kabisa ya uchunguzi..!! Waziri msomi kama huyu,ambaye ametajwa kwenye huo uchunguzi na wale anaotuhumiwa nao,badala akae chini kuitafakari na kufanyia kazi taarifa ya gazeti badala yake anakurupuka kushambulia gazeti na kulitishia kulipeleka mahakamani..!!

Hivi Dr.kigwangala analijua vizuri hilo gazeti!?? Amuulize Mwigulu Nchemba na january makamba wote hawa tunao huku mitaani wamelishakatwa mikia kutokana na vyanzo vya hilo gazeti.


Kwa bahati mbaya Dr.kigwangala umeangukia sehemu mbaya,unaanguka kipindi cha kuelekea uchaguzi na hutapitishwa hata kugombea ubunge.

Kigwa,una kashifa nyingi sana kwenye hiyo wizara,bahati mbaya tu vyombo vya habari vingi vinaogopa kukuandika..lakini wale wasanii unaowachukua kwenda nao kutangaza utalii inasemekana ww mwenyewe wanakutangazia chumbani kila Safari.

Pole bwana kigwa,nakuhakikishia uwaziri hufiki nao mwezi February labda mzee akupotezee akiona hili bandiko ila niamini unaondoka na maji mark my words.

Wale mademu wasanii ambao kwa sasa wameona kwako ni mzinga wa nyuki hivi punde utaanza kuonana nao ukiwa nzega nyumbani kwako. Maana ni aibu kwa waziri msomi kama ww kuhangaika na wale makahaba..wale wote wanauza sema style yao ni tofauti na hawa wengine.

Mods msiunganishe uzi wangu na nyuzi zingine...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima kutakuwa na ukweli, Kigwa lazima atakuwa amevuta pesa ndegu kwenye hii kampuni, alivyopata uwaziri wa utalii aliiandama sana hii kampuni kwa kudai ilikuwa inashirikiana na Nyalandu kuhujumu rasilimali za utalii na ilipewa vitalu kwa upendeleo na kutaka Nyalandu achukuliwe hatua za kisheria, lakini gafla kawa kimya na kuunga mkono vizuri sana kazi za kampuni hii , jamaa wa ccm ni walafi wa rushwa hata viongozi wa juu wanalijua hili.
 
Dkt. Kigwangalla akiendelea kulifuatilia hili gazeti, atapoteza Uwaziri wake. Angekuwa anaona mbele angekaa kimya.

Hili gazeti Mlione tu kama lilivyo. Mfikishieni ujumbe.

Alianza Mwiguu, akaja January Makamba na sasa ni Zamu ya Kigwangalla. Ila alijitahidi kufanya kazi tangu alipokuwa Wizara ya Afya.
 
Back
Top Bottom