#COVID19 Dkt. Kigwangalla adungwa chanjo ya Corona aina ya Sputnik V

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,910
25,184

Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Nzega Vijijini Dkt Hamis Kigwangalla ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Afya ya Jamii, apata chanjo yake ya corona, Sputnik Light, kutoka ya Urusi.

Dr. Kigwangalla aliwahi kupinga vikali matumizi ya chanjo katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona mnamo mwaka 2020 lakini alibadili msimamo wake mapema mwaka huu na kuhimiza upatikanaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona kama njia pekee ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19 unaosababishwa na virusi hivyo vya corona.
 
Kama kweli jiwe lilisukumiziwa baharini likazama na kufa kutokana na ubishi na kutokuyumbishwa kwake na mawimbi ya bahari toka magharibi basi aliyefanikiwa kulidondosha ana furaha sana maana vijiwe vivyobaki ni vyepesi kuliko unyoya wa kuku 🐔, vinasukumwa na upepo tu hadi kwenye miiba vinachomeka haswa huku vikijimwambafy kuwa vimechomwa.
 
View attachment 1867537
Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Nzega Vijijini Dkt Hamis Kigwangalla ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Afya ya Jamii, apata chanjo yake ya corona, Sputnik Light, kutoka ya Urusi.

Dr. Kigwangalla aliwahi kupinga vikali matumizi ya chanjo katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona mnamo mwaka 2020 lakini alibadili msimamo wake mapema mwaka huu na kuhimiza upatikanaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona kama njia pekee ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19 unaosababishwa na virusi hivyo vya corona.
alishituka pale hii kitu ilipofika hadi ikulu,ambako usalama unategemewa kuwa ni 100%.sembuse huku kwetu mtaani
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom