Dkt. Hassan Abbas azungumzia Ukomo wa Serikali kwenye Uchaguzi. Rais yupo hana ukomo na Mawaziri wapo ila wana ukomo

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi,

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas yuko Live on Times FM, 100.5, Azungumzia kuhusu ukomo wa Serikali wakati wa Uchaguzi, Rais wa JMT yeye yupo, in full, hana ukomo, pia mawaziri bado wapo ila wao wana ukomo!, hawaruhusiwi kutoa ahadi za kiserekali, na siku rais mpya akiapishwa tuu, uwaziri wao ndipo hukomea hapo. Wakuu wa mikoa na watumishi wengine wote, wao wanaendelea, ila hawatakiwa kupiga kampeni kukishabikia chama chochote.

Tuendelee kumsikiliza.
Kwa wenye simu janja, pakua appl hii ya Radio garden, sikiliza redio zote duniani kupitia simu yako ya mkononi.

Radio Garden

Tumsikilize Dr. Hassan anamwaga madini

*MAMBO 10 ALIYOYASEMA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI , DKT. HASSAN ABBASI KATIKA MAHOJIANO NA TIMES FM LEO TAREHE 23/09/2020*

1. Wakati wanasiasa wakiendelea na kampeni za uchaguzi, Serikali bado ipo na kazi mbalimbali zinaendelea kama ilivyopangwa, sheria za nchi zipo na wasemaji wa nchi wapo; ukitugusa na uongo wako tutakujibu;

2. Miradi mbalimbali mikubwa na midogo inayolenga kuboresha maisha ya Watanzania inaendelea vyema na tutaendelea kutoa takwimu za kila mara kuhusu utekelezaji;

3. Kuhusu faida za ndege hili tumeshalieleza sana kwamba ndege ni ajira hivyo zimeshaingiza zaidi ya ajira 400 za moja kwa moja; ndege ni mapato hivyo zimeshaongeza mapato ya Shirika na Serikali kutoka Bilioni 2.5 kwa mwezi hadi Bilioni 15 kwa mwezi na kodi zaidi zinalipwa zinazokwenda kuhudumia wananchi;

4. Kuhusu madai kwamba ndege zilinunuliwa bila uwazi wala bajeti yake haijulikani Dkt. Abbasi alihoji wanaotoa madai hayo kama wanaishi Tanzania au vipi! Alisema ununuzi ulikuwa kwa mujibu wa kifungu kipya cha 65A cha Sheria ya Ununuzi wa Umma (marekebisho ya 2016) ambayo inaruhusu, kwa nia ya kupata bei bora na thamani ya fedha, taasisi ya ununuzi kununua moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji wa bidhaa husika badala ya mawakala wanaopandisha bei;

5. "Kama kuna mtu alikuwa na wakala wake mfukoni katika ununuzi wa hizi ndege imekula kwao, Serikali imenunua moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wanaojulikana Kimataifa kama Boeing na Bombardia na sheria inaruhusu hivyo na ilipata bei ya chini kuliko hata zile zilizoainishwa kwenye tovuti zao," alisema.

6. Kwamba ndege hizi haijulikani zinanunuliwa kwa fedha kutoka wapi, Dkt. Abbasi alisema Watanzania waendelee kuwakataa wanaotoa hoja hizo dhaifu kwa kuwa ni matapeli wasiojua lolote linaloendelea nchini;

7. Akimwaga ushahidi wa bajeti za mwaka 2016/17, 2017/18 na 2019/20 kutoka Fungu 2006 na mradi namba 4294 (Acquisition of New Aircrafts-ATCL), Dkt Abbasi alisema kwa miaka takribani minne mfululizo Serikali imekuwa ikitenga wastani wa TZS Bilioni 500 kwa mwaka na zinajadiliwa na zinapitishwa na Bunge kupitia fungu hilo, akashangaa wanaodai kuwa fedha za ndege hazijulikani zinatoka wapi kama ni watu wanaoishi Tanzania au ndio wamekuja nchini juzi kushangaa maendeleo yetu!!!;

8. Akaulizwa hoja kama hiyo kuhusu usiri katika ujenzi wa reli ya SGR na Mradi wa Umeme Rufiji na fedha zinakotoka Dkt. Abbasi akaainisha vipande vyote vya ujenzi wa reli na Mradi wa Umeme kuwa vilishindanisha wataalamu wa ndani na nje. Akatoa mfano mradi wa SGR Dar kwenda Moro walijitokeza washindani zaidi ya 40, Moro kwenda Makutupora walijitokeza washindani takribani 36 na sasa akawaalika "wenye watu wao" waache kupiga kelele bali wawalete washiriki Zabuni iliyotangazwa Agosti mwaka huu ya ujenzi wa SGR kwa kipande cha Mwanza-Isaka. Kuhusu mradi wa Umeme Rufiji alisema zabuni ilitangazwa wazi na takribani makampuni manne yalishiriki kutoka mataifa ya Afrika, Ulaya na Asia;

9. Aidha, Dokta Abbasi alizidi kusisitiza kuwa fedha zote za miradi hii zipo kwenye bajeti na zinapitishwa na Bunge kila mwaka huku akitaja mradi wa Rufiji kuwa mpaka sasa TZS Trilioni 1.432 zimeshatolewa;

"Kuna wageni wengi nchini kwa sasa kwa hiyo tuwavumilie, mtu anahoji hela za SGR hazijulikani zinatoka wapi, nataka tuamini yeye ndio hajulikani ametoka wapi na anataka nini, anayehoji hii akasome fungu 2005, mradi namba 4281 kwenye Sekta ya Uchukuzi aone kila mwaka Bunge liliidhinisha sh. ngapi kwa miradi ya SGR kuanzia mwaka 2017/18," alisema na kuwataka Watanzania kuwapuuza waropokaji wanaoumizwa na maendeleo yanayotokea.

10. Akasisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea kutekeleza mambo makubwa yenye mwangwi mkubwa katika kuwanufaisha Watanzania na kuwataka Wananchi kuendelea kutimiza wajibu wao na kuwakataa mabeberu na mawakala wao.

Akaulizwa beberu ni nani? Akajibu: "Beberu hana rangi wala utaifa, beberu ni mtu, taasisi au taifa lolote ambalo tukiwa hatuna hospitali, barabara, madaraja, ndege na vingine muhimu kwa maendeleo wanatubeza; tukianza kuvijenga na kuvifanyia kazi wananuna na kujaribu kuhujumu na kuvibeza bila hoja; mtu wa namna hii awe Mtanzania au si Mtanzania ni beberu tu," alisema.

Paskali
 
Daaa huyu Rais anapendelewa sana!Inakuwaje Rais aruhusiwe kutoa rushwa ya uchaguzi? Sababu hiyo hiyo inayomkataza waziri kutoa fedha za miradi kwenye majukwaa ya kampeni,kwanini hiyo hiyo isimdhibiti Rais?

Katiba na sheria za nchi yetu zina mapungufu makubwa ila kwasababu ziko infavor kwa watawala,ndio maana zinabaki hivyo hivyo!
Nyerere alipoona hilo alipaswa kuchukua hatua na sio kuishia kutoa angalizo tu!
 
Daaa huyu Rais anapendelewa sana!Inakuwaje Rais aruhusiwe kutoa rushwa ya uchaguzi?Sababu hiyo hiyo inayomkataza waziri kutoa fedha za miradi kwenye majukwaa ya kampeni,kwanini hiyo hiyo isimdhibiti Rais?..
Hujui maana ya rushwa wewe
 
Tuko pamoja chief. Hata mimi naelewa hivyo kwa mujibu wa katiba. Hawa wanao lalama juu ya katiba ni vyema wakamlalamikie Nyerere na wezake.

Sisi tunaendelea kuifuata katiba.
 
Hilo mbona kila mtanzania analijua!
Hata mwalimu aliyestaafu 2006 analijua hili vizuri labda yeye ndo anadhani hawajui. Mawaziri wanafanya makusudi kufanya ziara na kutoa ahadi, Wakuu wa wilaya ndo kabisaa.

Wiki iliyopita nilikuwa na safari ya kikazi mkoani Rukwa nikakuta Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda yuko jukwaani anamnadi mgombea wa CCM Nkasi kaskazini. Anafafanunua tunayoona yanavunjwa kila siku?
 
Back
Top Bottom