Dkt. Francis Michael: Kufanyia Elimu Mageuzi tutaanzia kwenye kubadilisha Mitaala(syllabus)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael, amesema Mabadiliko ya Mitaala ni swala pana ambalo linatakiwa liangaliwe kwa Upana wake. Katika Kufanyia Elimu Mageuzi unaanzia kwenye kubadilisha Mitaala. Ameyasema hayo wakati alipopokelewa Dodoma kwenye Ofisisi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akitoke Wizara ya Utalii leo Tarehe 20 Juni 2022.

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alitoa wito kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kufanya mabadiliko katika mitaala ya elimu (syllabus).

Rais Samia alitoa wito huo tarehe 19 Juni 2022 wakati akizindua Taasisi ya Wanawake Initiatives Foundation (MIF) na kueleza kuwa Zanzibar inakabiliwa na changamoto nyingi katika sekta ya Elimu.

Aidha, Rais Samia alitaka pia kuwepo na umakini katika sifa za walimu wanaoajiriwa, utungaji wa mitihani pamoja na uwezeshwaji wa vitendea kazi kwa wakaguzi.

Rais Samia alisema licha ya ufaulu kupanda kiasi kwa mwaka 2021 na kupungua kwa idadi ya waliopata sifuri, bado iko haja kwa Wizara hiyo pamoja na wadau kutafuta ufumbuzi wa kutatua changamoto zilizopo.

Rais Samia pia aliwataka wazazi, walezi na jamii kubeba jukumu la kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo ipasavyo na kuhakikisha kuwa wanapata muda wa kujisomea.
 
Sio syllabus na Lugha ya kufundisha ibadilishwe shule zote ziwe English medium hakuna maana viongozi wote wa Serikali akiwemo.yeye watoto wanasomesha English medium wanakwepa nini kusomesha swahili medium schools?
 

Attachments

  • Screenshot_20220620-192936_Instagram.jpg
    Screenshot_20220620-192936_Instagram.jpg
    46 KB · Views: 7
Isije ikawa kama yule jamaa aliyeunga biology, chemistry na physics na kufanya somo moja aliloliita unified science. Mambo yaliharibika sana
 
Kule Mali Asili ba Utalii alifanya mageuzi yoyote? Tuanzie hapo kwanza. Haiwezekani ana siku moja tu ofisi za elimu tayari ameshaanza kuongelea mabafiliko ya sylabus wakati Mali Asili alikuwa mzigo.
 
Sio syllabus na Lugha ya kufundisha ibadilishwe shule zote ziwe English medium hakuna maana viongozi wote wa Serikali akiwemo.yeye watoto wanasomesha English medium wanakwepa nini kusomesha swahili medium schools?
Kweli kabisa nakuunga mkono kwa hili na kibaya zaidi ni mchanganyiko wa lugha huku kiswahili kule kiingereza matokeo yake ni vurugu tu wachague lugha moja ya kufundishia mwanzo mwisho Kama ni syllabus watabadili sana hakutakuwa na mafanikio yoyote
 
Back
Top Bottom