Dkt. Dugange amtaka Mkandarasi wa Barabara ya Igwachanya - Itulahumba Kukamilisha kwa Wakati

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

DKT. DUGANGE AMTAKA MKANDARASI WA BARABARA YA IGWACHANYA-ITULAHUMBA KUKAMILISHA KWA WAKATI

NAIBU Waziri OR TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Igwachanya - Itulahumba yenye urefu wa kilometa 19.25 itakayogharimu Sh. Bilioni 9.86 kwa kiwango cha lami kuanza kazi kwa wakati na kuikamilisha katika muda uliopangwa kwenye mkataba.

Mhe. Dkt Dugange ametoa agizo hilo wakati akishuhudia makabidhiano ya mkataba baina ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na mkandarasi kampuni ya Summer Communication Ltd itakayoanza kujengwa Desemba, 5 mwaka huu katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.

Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Igwachanya na Itulahumba waliojitokeza katika tukio hilo, Mhe. Dkt Dugange amemshukuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi hicho cha fedha na kumtaka mkandarasi huyo kuzingatia thamani ya fedha pamoja na kujengwa kwa kiwango bora kwa kuwa ni barabara muhimu itakayoifungua wilaya hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Claudia Kitta ametoa rai kwa mkandarasi wa mradi huo kutoa fursa ya ajira kwa wananchi wa eneo hilo badala ya kutoa ajira kwa wananchi wa maeneo ya mbali.

Naye, Meneja wa TARURA Wilaya ya Wanging'ombe, Boniface Kasambo amesema mradi huo utakamilika ndani ya miezi 20 na kukamilika kwake kutarahisisha usafiri kwa abiria na mazao, kuimarisha kipato cha wananchi pamoja na kuifungua Wilaya hiyo.
F_ibNCcWcAAE60f.jpg
F_ibNCgXgAAfu80.jpg
F_ibNCcXsAA-bF3.jpg
F_ibNCeW0AAGS4i.jpg
 
Itakuwa jambo jema zoezi likifanikiwa. Itarahisisha usafiri toka Mbeya - Njombe
Walimaji wa lemon 🍋 watapata masoko kwa urahisi zaidi
 
Back
Top Bottom