Dkt. Bashiru: Siyo kweli kwamba CCM itatumia wingi wao Bungeni kubadilisha Katiba ili kumuongezea muda Rais Magufuli kukaa madarakani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
BASHIRU.jpg

Katibu mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru amekanusha uvumi unaoenezwa na wapinzani kwamba wabunge wa CCM watatumia wingi wao bungeni ili kumuongezea Rais Magufuli muda wa kukaa madarakani iwe zaidi ya miaka 10.

Dkt. Bashiru amesema Rais Magufuli atahudumu madarakani kwa miaka 10 kwa mujibu wa katiba ya sasa na kwamba propaganda za wapinzani hasa Chadema zipuuzwe.

Nawatakia ninyi nyote Dominica yenye baraka!

Maendeleo hayana vyama!
 
Mbona hata Rais alishaweka wazi hataongeza hata sekunde moja hii ipo wazi kabisa.
 
Wapinzani wakikosa hoja huwa wanakuja na vioja. Nakumbuka haya waliwahi kuyasema hata ktk miezi ya mwisho mwisho ya utawala wa JK kwamba anapanga kuongeza siku za kukaa madarakan, JK akawajibu kwamba hatozidisha hata dakika 1 ya kukaa madarakan kwa mujibu wa sheria. Sasa leo tena badala ya kuja na hoja zenye mashiko wao wanakuja na hoja za masikitiko.
 
Ccm sio wa kuwaani sana maana shein alishawahi kuzidisha muda
 
Wabunge wakiamua ni kwamba wananchi wameamua!
Huo utakuwa mgogoro mpya na utaenda kueleta kishindo kikubwa sana tutaomba kuwe na referendum na tuwe na chombo huru kitakacho simamia hizo kura zetu.

Hii nchi ina watu smart hawawezi kujaribu kufanya hilo jambo kama watu wangekuwa wanajiongezea tuu tungempata wapi yeye?
 
Back
Top Bottom