Dk.Slaa: Tulishinda urais mwaka 2010

Dk.Slaa: Tulishinda urais mwaka 2010

Kuna gazeti moja la kila wiki nahisi kama kumbukumbu zangu ziko sawa Raia Mwema, kama nitakuwa nimewasingizia wanisamehe, walieleza namna jinsi watu wa usalama walivyojifungia Kempiski kuchakachua Matokeo na Mkuu wa kaya kupata asilimia 60 ya kura zote kwa madai nchi ilikuwa haijajiandaa kwa ajili ya ujio wa chama kingine na kigezo cha usalama wa nchi na watu wake. Zanzibar CUF ilishawahi kushinda jamaa wakachakachua na inajulikana mpaka kituo kimoja cha Televisheni kiliwahi kufungiwa, gazeti la Majira likapigwa marufuku Zanzibar, Bakhressa akachomewa unga wake n.k Huku tunaona Tido wa TBC alivyopigwa chini. Zote hizi ni nadharia dhanifu(hypothesis) katika kujenga hoja wadau mpo huru kunikosoa pale ambapo sipo sawa ama nikiwa nimedanganya. JK amechangiwa sana na udini ambao utamtafuna mpaka aingie kaburini ameigeuza nchi kuwa United Islamic Republic of Tanzania. Sasa hivi anahangaika na hao vikasuku vyake kumsafisha. Na kama huamini anzisha kikanisa chako hata mtaani cha watu 10 zindua kitu kama harambee ya uongo na kweli mwalike kama hajaja hii ni katika kuudanganya umma wa Watanzania kuwa yeye sio mdini. CDM walipoanza kupamba moto wakadai CDM ni chama cha Kikatoliki wakamwandama mpaka Kardinali wakisema ni muuza madawa. Kiongozi wa CUF akaenda msikitini akidai kwamba imewalazimu wao kumtetea JK kwa sababu ni Muislamu mwenzao. Hili nalo liliwapunguzia sana kura CCM na litawamaliza 2015 kama CDM wakijipanga sawa sawa bila hata ya hao UKAWA kwa sababu CUF ni wanafiki na wamejijenga kimtindo wa udini ni chama cha waislamu hata hao wenye majina ya Kikristo ni Waislamu. Muulizeni W. Lwakatare chanzo cha mgogoro CDM na huyo mwanasiasa kijana umechangiwa kwa kiasi fulani na CUF kupitia CCM na ujio wa Lwakatare CDM.

Kwa CCM Dr Slaa bado ni tishio kubwa kwao na naweza kusema anawanyima usingizi. Mara wamzushie kafa, mara wadai kachukua mke wa watu, mara kudai alikuwa padri na siasa kibao za maji taka bado hawatamweza. CCM ni chama kinachopoteza mwelekeo na kitaanguka kama chama cha KANU kule Kenya ambao waliendekeza ukabila ambao unawatafuna mpaka leo.

Tutamlaani JK kwa kuendekeza Udini katika nchi yetu , Udini ambao unahatarisha amani ya nchi yetu na CCM itakufa kwa mtindo huo. Upinzani mnatakiwa msimame na CDM kama CDM kihakikishe mmeshika dola mwaka 2015. Habari za usalama wa nchi, CDM chama cha "wakristo" tena wakatoliki (JK hana aibu na wala fadhila kwa wakatoliki waliomsomesha shule za awali na kati huko Msoga kwao), kuwa CDM chama cha kikabila"Wachagga" hazina hoja wala mantiki kwenu nyinyi kama chama kilichodhamiria kuishika dola na mtashangaa hao hao CCM watakihama chama chao na kuja kujipendekeza CDM kwa kigezo cha madaraka.


Mwisho ni swali kama mtindo ni huu wa kuchakachua, kuna umuhimu gani wa kuwa na upinzani nchini?
 
Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kimesema kilishinda uchaguzi mkuu wa Mwaka 2010 chini ya mfumo wa vyama vingi.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa,Ambaze pia alikuwa mgombea wa CHADEMA katika uchaguzi huo,Ameyasema hayo katika mahojiano maalum na Waandishi wa Gazeti la Mwananchi.

Source Mwananchi toleo la leo Jumamosi.
Kachoka huyo mzee, amebaki kubwabwaja tu
 
Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimresema kuwa kinaamini kilishinda uchaguzi wa rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 chini ya mfumo wa vyama vingi.

Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa, ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi huo, alibainisha hayo hivi karibuni wakati wa mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili.

Dk Slaa alisema kuwa ana uhakika kuwa chama chake kilipata kura nyingi zaidi za urais, tofauti na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Mrisho Kikwete aliyetangazwa mshindi.

“…Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, tulikataa kumtambua Rais Kikwete, ingawa wakati ule hatukujua kwa uhakika kama tulishinda. Kadiri nilivyozunguka, ndiyo kadiri tulivyoanza kuamini kwamba tulishinda,” alisema Dk Slaa.

Alisema kuwa takwimu walizonazo zinaiaminisha Chadema kwamba ilishinda Uchaguzi Mkuu wa urais mwaka 2010.

“Sababu, unafika kwenye jimbo wanakusomea kura ulizopata katika uchaguzi ule wakizilinganisha na alizozipata Kikwete na Profesa Ibrahim Lipumba… wanasema Dokta hapa ulimshinda… kwa kura 20,000, pale ulimshinda kwa kura 15,000 pale ulimshinda kwa kura…,” alifafanua na kusisitiza:

“Sasa ndiyo, tuna uhakika kama tulishinda na ndiyo maana Kikwete hajawahi kwenda kwa wananchi kushukuru kwa kumchagua, tofauti na tabia yake. Anachofanya sasa ni kwenda kuzindua miradi.”

Hata hivyo, Dk Slaa alisema hawakuweza kuendelea na madai yoyote kwa sababu kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi, mshindi wa urais akishatangazwa hairuhusiwi kupinga kwa namna yoyote hata mahakamani, akieleza kuwa hiyo pia ndiyo sababu ya kuhitaji Katiba Mpya.

Tume ya uchaguzi na CCM

Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema anasubiri kwanza kusoma kwenye vyombo vya habari alichokisena Dk Slaa ndiyo ataweza kuzungumzia suala hilo.

“Kwa kuwa wewe ndiyo umeniambia Dk Slaa amesema hivyo, ngoja nione kwanza halafu tume itatoa maelezo,” alisema Jaji Lubuva.

Alipopigiwa simu Makamu Mwenyekiti wa CCM- Bara, Philip Mangula ili atoe ufafanuzi kuhusu suala hilo, alimsikiliza mwandishi wetu, kisha akasema yupo katika kikao na kukata simu.

Wizi wa kura

Alipoulizwa kama wanaelewa kura zinavyoibwa kutokana na malalamiko ya mara kwa mara ya Chadema na vyama vingine vya upinzani, Dk Slaa alisema:

“Watu wengi wanafikiri huo ni wimbo tu wa kila siku, sasa kama tunaibiwa tunyamaze? Tuseme uongo kama hatukuibiwa kura…? Hakuna uwanja sawa katika uchaguzi.

“Uchaguzi kimsingi ni uwanja wa mpira. Umeshaona kama katika uwanja wa mpira upande mmoja kuna kichuguu na kinaachwa pale? Kinaondolewa. Kilichokosekana nchi hii ni dhamira ya kuondoa vichuguu katikati ya kiwanja cha mpira; usipoondoa hivyo vichuguu hutapata uchaguzi wa haki hata siku moja.”

“Kumbuka Arumeru tulitangaza, tukasema tumegundua vituo hewa 55 vyenye jumla ya wapigakura 20,000, tulitangaza. Bahati nzuri pale tuliweza kusimamia na mnakumbuka pale tulivyotukanana na ofisa wa polisi ambaye leo ni DCI, unaweza kumpigia simu Mwigulu Nchemba akueleze jinsi tulivyotunishiana misuli… tukafanikiwa pale kuokoa kura 20,000,”alisema.

Aliongeza: “Kalenga tulipiga kelele mwanzoni kabisa kuhusu kuwapo majina mapya kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, kama daftari liliboreshwa… yaliingiaje kwenye daftari hili la 2010. Ndiyo maana hatuna imani na Tume ya Uchaguzi….”

Alibainisha: “Mimi nina uzoefu wa kesi za uchaguzi katika ushindi wangu mara tatu Jimbo la Karatu hakuna hata mara moja ambayo sijapelekwa mahakamani.

“Mara ya mwisho niliponea chupuchupu, ndiyo akili ikafunguka. Hukumu ilitolewa niwafungulie CCM kesi ya kughushi. “Kwa sababu mahakama ilikuta kura zaidi ya 5,000 kupitia fomu namba 21b (result form) siyo sandukuni ndipo walipoibia, lakini kwenye matangazo ya awali nilishinda kwa kura 1,060, wamekwenda mahakamani wakasema wamenishinda kwa kura 177.

“Kwa miezi mitatu niliangalia bila kugundua, nikipiga hesabu naona ni kweli, kumbe walitengeneza vituo hewa na katika vituo vya kujumlisha kura na kuvipa namba kama iliyopo kwenye fomu halali za matokeo na kujaza kura za wizi. Waliipa CCM kura 300, Dk Slaa kura 20, za kwao zilipanda zangu zilishuka, makahama imesema kazi hiyo haikufanywa kijijini bali na wataalamu, ndiyo maana tunataka Tume Huru ya Uchaguzi ili kuwa na uwanja sawa katika uchaguzi.”

Wingi wa wanachama CCM/Chadema

Kuhusu wingi wa wanachama wa Chadema na CCM, Dk Slaa alisema: “Kwa taarifa yako nina taarifa ya mkaguzi aliyewauliza CCM orodha ya wanachama wake ikashindwa kutoa. Kama hawana orodha ya wanachama, hiyo milioni sita wanaitoa wapi? Uongo, ‘nawachalenji’ watoe hadharani….”

“Ushahidi wa pili, kujua kama una wanachama ni uhai wa wanachama. Taarifa ya CCM ya 2010 inaonyesha kwamba walikuwa wanapata kutoka kwa wanachama wao Sh9 bilioni za kadi kama ada, zimeshuka hadi Sh2 bilioni, utahesabu ni wangapi hao. Wasitudanganye…, tuna vyanzo vingi vya kupata taarifa.

Mimi sitakupa leo nina wanachama wangapi kwa sababu tunafunga kompyuta kwenye kila kanda, jimbo na kata, tumeanzisha ‘data base’ baada ya kukamilika nitakwambia tuna wanachama wangapi,” alisema na kuongeza:

“Uongo wa CCM usikudanganye kwamba nguvu yao ni wanachama, kama nguvu yao ni wanachama, uchaguzi haupigiwi kura na wanachama, kura zinapigwa na wapigakura, wananchi wanaotaka huduma kwa sababu wanalipa kodi.

Wanapiga kura ili wapate kiongozi ili asimamia kodi zao, waondokane na maisha magumu, wapate huduma za afya na elimu bora...”


Source: Mwananchi
Alichosema slaa ni sahihi kwamba mwanzoni hawakuamini kama walishinda, ila kadri walivyozunguka waligundua kuwa walishinda kwa sababu siku zote kwenye mikutano wanakuwa na watu wengi ila amesahau kuwa siyo wote wanaojaa kwenye mikutano hasa ya chadema wanajitokeza kupiga kura
 
Khaa!! Kwa maneno haya ya kujichanganya naona Nape alikuwa sahihi kabisa


''Babu anazeeka vibaya"
 
Maneno ya BABU yana mkanganyiko mkubwa.

Juzi kwenye Press conference alikiri kuwa hawakuwa tayari kushika dola kwa sababu walikuwa kiharakati zaidi.

Ila sasa wamevua uanaharakati na kujiunga na siasa na sasa wako tayari kushika dola hapo mwakani.

Sasa hili la ushindi 2010 anamdanganya nani?
Mzee hana tofauti na nyoka wa mdimu
 
Khaa!! Kwa maneno haya ya kujichanganya naona Nape alikuwa sahihi kabisa


''Babu anazeeka vibaya"
Umeonae, huyu mzee ameanza sarakasi za kuelekea 2015, safari hii wasimlegezee na kauli zake za kipumbavu
 
Ndoto za vichaa bana, baada ya kupoteza mvuto, hawa vichaa akina slaa pamoja na uzee wake hana busara ni kama zombie
 
Chadema kupambana chini ya uongozi wa SLAA na MBOWE ni sawa na kutaka kitunguu umekiinamia jamani, tuwekeeni damu changa

Thatha Hawa wazee wanafaa sana huo ni mtazamo wangu.wanao wapinga wengi ni ccm usiogope lakini.
 
Hata kwenye ubunge usalama wa taifa uliwasaidia? Mbona CHADEMA ilipata wabunge 23 tu? Uongo hauna marefu!

Kwa mTZ yeyote mwenye akili wizi ulikuwa nje nje hata jimbo la Kawe na Ubungo kama si kukomalia CDM isingeshinda. Majimbo mengi wizi ulishamiri sana na sio kwenye upigaji tu hata kwenye kujumlisha! Hata kwenye udiwani wagombea wa CDM walioshinda walihongwa ili wa CCM atangazwe mshindi. Kwa vile wananchi hawako makini (wepesi kusahau) ndio maana unaona tumekaa kimya ila siku ya siku ikifika CCM mtaisikia kwenye historia.

Kama chaguzi za mtaa na vitongoji unakuja keshokutwa na daftari la wapiga kura halijaboreshwa unategemea nini? Hiyo Tume ya Uchaguzi sio huru inangojea Rais akurupuke boresheni daftari halafu itakuwa zima moto wengi watashindwa kujiandikisha!

Semeni ukweli jamani CCM hawako tayari kuondoka madarakani kwa sanduku la kura! Itafika sasa wananchi tutaanza ngumi mtaani halafu watasema upinzani umevunja amani kumbe ni wao wenyewe. Inauma sana.
 
Sio swala la msingi Sana kwa kipindi huku lakini chadema walishinda uchaguzi huo kwa asilimia 64.
Aidha usalama wa taifa walishiri kubaka demokrasia na kuchagua kuwakandamiza wananchi wa taifa hili.

Na ndio sababu mambo hayaendi! Elimu, Afya hakuna maboresho ya maana. Maisha bora tuliyoahidiwa yako wapi? Kiongozi ndiye tunayemtegemea awe na maono ya kutuletea maendeleo lakini wapi, kama haushinda kihalali dhamira inamsuta hawezi fanya kitu chenye baraka. BRN ndio kwanza inazidi kuturudisha nyuma!
 
Huyu mzee chizi nadhani anahitaji tiba huu uongo ananufaika nao nini mtu zima hovyo kabisa.
bw mdogo ni kweli kwamba mwigulu ,nkamia walipewa ulaji baada ya kutukana wapinzani lakini kulingana na muda sioni kama hilo linaweza tokea kwako,usitafutie laana bure kwa kutukana wakubwa,najua tumbo linakusumbua lkn kumbuka haya mambo ni yahapa duniani tu,fuata mila zakwenu simiyu.(kolomije)
 
Maneno ya BABU yana mkanganyiko mkubwa.

Juzi kwenye Press conference alikiri kuwa hawakuwa tayari kushika dola kwa sababu walikuwa kiharakati zaidi.

Ila sasa wamevua uanaharakati na kujiunga na siasa na sasa wako tayari kushika dola hapo mwakani.

Sasa hili la ushindi 2010 anamdanganya nani?

Unavisha nini? Ukweli Chadema ilishinda
 
Itafika sasa wananchi tutaanza ngumi mtaani halafu watasema upinzani umevunja amani kumbe ni wao wenyewe. Inauma sana.

Amani ya Tanzania italindwa kwa gharama yeyote. Anza hizo ngumi uone kazi ya vyombo vya dola.
Nawachukia sana watu wasiopenda Amani.
 
Kweli dokta. Nakumbuka matokeo ya jimbo la Nyang'wale na Geita yalichanganywa makusudi kabisa eti kuipa ushindi CCM. Pia matokeo ya shinyanga mkurugenzi aligoma kutangaza baada ya ccm kumlazimisha atangaze kinyume na yalivyo, na aliyetangaza akawatangaza CCM washindi kwa tofauti ya kula moja dhidi ya cdm. Majimbo mengi matokeo yalitangazwa kwa utata sana mfano segerea, kibaha, temeke, mtwara mjini, tandahimba, nyamagana, mleba yote, bukoba mjini, tarime, n.k ILA KITU NACHOKUMBUKA NI DK.SLAA RAISI WA MIOYO YA WATANZANIA KUONGOZA KATIKA MATOKEO YA UCHAGUZI KATIKA MAJIMBO KARIBU YOTE YA KANDA YA ZIWA NA MAGHARIBI MBAYA ZAIDI KITUO CHA POLISI MABATINI MWANZA AMBAPO ALIONGOZA KWA ZAIDI YA 88%
 
Amani ya Tanzania italindwa kwa gharama yeyote. Anza hizo ngumi uone kazi ya vyombo vya dola.
Nawachukia sana watu wasiopenda Amani.

Amani gani we mjinga usiye na haya wala soni, watu wanaishi maisha ya kimaskini kupindukia kwasababu ya ccm, hiyo amani wanaipata wapi? Sema watanzania ni watulivu tu kwasababu ya ujinga lakini muda unakuja hata Mungu anajua hilo.
 
Back
Top Bottom