The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,950
- 12,549
Kweli dokta. Nakumbuka matokeo ya jimbo la Nyang'wale na Geita yalichanganywa makusudi kabisa eti kuipa ushindi CCM. Pia matokeo ya shinyanga mkurugenzi aligoma kutangaza baada ya ccm kumlazimisha atangaze kinyume na yalivyo, na aliyetangaza akawatangaza CCM washindi kwa tofauti ya kula moja dhidi ya cdm. Majimbo mengi matokeo yalitangazwa kwa utata sana mfano segerea, kibaha, temeke, mtwara mjini, tandahimba, nyamagana, mleba yote, bukoba mjini, tarime, n.k ILA KITU NACHOKUMBUKA NI DK.SLAA RAISI WA MIOYO YA WATANZANIA KUONGOZA KATIKA MATOKEO YA UCHAGUZI KATIKA MAJIMBO KARIBU YOTE YA KANDA YA ZIWA NA MAGHARIBI MBAYA ZAIDI KITUO CHA POLISI MABATINI MWANZA AMBAPO ALIONGOZA KWA ZAIDI YA 88%
Duuh, hii kali kweli kweli na maana yake ni kuwa polisi na Jeshi vinalazimika kumtii Amiri Jeshi mkuu kwa baasi tu lakini kmwe hayumo ndani ya mioyo yao!!
Katika utafiti wangu,nimethibitisha pia kuwa hata kwenye kambi za jeshi karibu zote mzee wa kazi Dr W.P Slaa alimpiga kwa mbaaali sana "Mr Dhaifu" na inasemekana kuwa kuwa kwa kura alizoambulia huyu katika vituo vilivyoko kwenye Barracks za jeshi na police ni zile za maofisa wa ngazi za juu tu wachache wa kuteuliwa mfumo!!
Lakini asikudanganye mtu hawa askari wa ajira za kawaida hasa wa jeshi la polisi wako upande wa wananchi. Ukikuta wanagawa kipondo kwa wananchi eneo flani ujue wanatii amri tu na hawana namna kwa sababu wanaishi kwa kazi hiyo wao na familia zao na kanuni za kazi yao zinawataka wafanye hivyo!!
Hata mimi natambua kuwa Jakaya Kikwete hakushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ndiyo maana hajiamini na utawala wake unayumba kuliko tawala zote zilizowahi kutokea,na ni kwa sbb hana uhalali wa umma anaouongoza,ni Rais wa kikundi flani kidogo tu cha watu wanaodhania wana nguvu sana kuuzidi umma. Na wamshukuru Mungu sana kwani hajataka kuruhusu baya lolote kutokea dhidi ya utawala wake huu dhalimu na hii si kwa sababu nyingine yoyote labda wajione wao wana uhalali,walishinda uchaguzi kihalali...la hasha, bali Mungu huyu mwenye enzi ameruhusu waovu hawa kuendelea kupumua na kufurahia uovu wao ingalau kwa sasa ili wana wa Mungu (wana wa nchi hii) wasipate taabu,wapite na kufika salama kule anakokusudia kuwapeleka, nchi ya Kananii!!
Lakini uvumilivu wa Mungu umeshafikia kikomo na tayari amekwisha kuandaa mpango maalumu wa ukombozi kwa watu wake na ameshawaonesha wadhalimu hawa na kuwambia kwamba utawala wenu uko ukingoni......ndiyo maana haya tunayoyaona sasa yanatokea, ndiyo maana wanapambana mpaka tone lao la mwisho lakini hiyo ni kazi bure tu kwa sababu Mungu kamwe hawezi kushindana na wanadamu....Lakini hayana madhara kwa sababu mpango wa Mungu ni madhubuti na hauna madhara kwa watu wake wasio na hatia!!