Kuna gazeti moja la kila wiki nahisi kama kumbukumbu zangu ziko sawa Raia Mwema, kama nitakuwa nimewasingizia wanisamehe, walieleza namna jinsi watu wa usalama walivyojifungia Kempiski kuchakachua Matokeo na Mkuu wa kaya kupata asilimia 60 ya kura zote kwa madai nchi ilikuwa haijajiandaa kwa ajili ya ujio wa chama kingine na kigezo cha usalama wa nchi na watu wake. Zanzibar CUF ilishawahi kushinda jamaa wakachakachua na inajulikana mpaka kituo kimoja cha Televisheni kiliwahi kufungiwa, gazeti la Majira likapigwa marufuku Zanzibar, Bakhressa akachomewa unga wake n.k Huku tunaona Tido wa TBC alivyopigwa chini. Zote hizi ni nadharia dhanifu(hypothesis) katika kujenga hoja wadau mpo huru kunikosoa pale ambapo sipo sawa ama nikiwa nimedanganya. JK amechangiwa sana na udini ambao utamtafuna mpaka aingie kaburini ameigeuza nchi kuwa United Islamic Republic of Tanzania. Sasa hivi anahangaika na hao vikasuku vyake kumsafisha. Na kama huamini anzisha kikanisa chako hata mtaani cha watu 10 zindua kitu kama harambee ya uongo na kweli mwalike kama hajaja hii ni katika kuudanganya umma wa Watanzania kuwa yeye sio mdini. CDM walipoanza kupamba moto wakadai CDM ni chama cha Kikatoliki wakamwandama mpaka Kardinali wakisema ni muuza madawa. Kiongozi wa CUF akaenda msikitini akidai kwamba imewalazimu wao kumtetea JK kwa sababu ni Muislamu mwenzao. Hili nalo liliwapunguzia sana kura CCM na litawamaliza 2015 kama CDM wakijipanga sawa sawa bila hata ya hao UKAWA kwa sababu CUF ni wanafiki na wamejijenga kimtindo wa udini ni chama cha waislamu hata hao wenye majina ya Kikristo ni Waislamu. Muulizeni W. Lwakatare chanzo cha mgogoro CDM na huyo mwanasiasa kijana umechangiwa kwa kiasi fulani na CUF kupitia CCM na ujio wa Lwakatare CDM.
Kwa CCM Dr Slaa bado ni tishio kubwa kwao na naweza kusema anawanyima usingizi. Mara wamzushie kafa, mara wadai kachukua mke wa watu, mara kudai alikuwa padri na siasa kibao za maji taka bado hawatamweza. CCM ni chama kinachopoteza mwelekeo na kitaanguka kama chama cha KANU kule Kenya ambao waliendekeza ukabila ambao unawatafuna mpaka leo.
Tutamlaani JK kwa kuendekeza Udini katika nchi yetu , Udini ambao unahatarisha amani ya nchi yetu na CCM itakufa kwa mtindo huo. Upinzani mnatakiwa msimame na CDM kama CDM kihakikishe mmeshika dola mwaka 2015. Habari za usalama wa nchi, CDM chama cha "wakristo" tena wakatoliki (JK hana aibu na wala fadhila kwa wakatoliki waliomsomesha shule za awali na kati huko Msoga kwao), kuwa CDM chama cha kikabila"Wachagga" hazina hoja wala mantiki kwenu nyinyi kama chama kilichodhamiria kuishika dola na mtashangaa hao hao CCM watakihama chama chao na kuja kujipendekeza CDM kwa kigezo cha madaraka.
Mwisho ni swali kama mtindo ni huu wa kuchakachua, kuna umuhimu gani wa kuwa na upinzani nchini?