Dk slaa kwa hili tusidangnyane (nyani haoni kundule) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk slaa kwa hili tusidangnyane (nyani haoni kundule)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanaone, May 11, 2011.

 1. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  DK SLAA ASEMA "Pinda, kwa siku moja akiwa kule bungeni hupata posho ya Sh200,000 ambayo inazidi mshahara wa mwezi mmoja wa mwalimu, hata polisi anayelinda usalama wenu,
  Dk Slaa aliyekuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka jana alisema, inasikitisha kuona Mbunge wa Katavi anakuwa mbinafsi kwa kujiwekea umeme wa jua kwenye nyumba yake pekee katika Kijiji cha Usevya badala ya kuupeleka kwa wananchi wote.
  source mwananchi.

  lakini huyuhuyu dk slaa anayesema pinda hupata posho ya sh 200,000 kwa siku mbona yeye hajapinga chama chake kumlipa marupurupu na mshahara anaolipwa mbunge ambao yy mwenyewe alisema ni milioni 7. kwa ufupi dk ni muongeaji mzuri na mhamasishaji mzuri wa wananchi lkn katika vitendo ni ZIRO kabisa, yy kila siku hulia kuwa posho wanazolipwa wabunge ni kubwa leo posho anayolipwa waziri mkuu ni kubwa sasa mbona yy haonyeshi mfano kwa kukataa marupurupu ambayo chadema wameamua kumlipa, aseme tu msinilipe hizi hela ni bora tuwasomeshee yatima ktk majibo yetu, tena kwa hivyo itakuwa kakisaidia sana chadema.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,337
  Likes Received: 19,507
  Trophy Points: 280
  huyu si alijifanya kukataa gari jipya? then waandishi wa habari wakaiandika hii taarrifa? au ni kujin'garisha kwa wanatanganyika
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mtoto wa mkulima hovyo hovyo kabisa!
   
 4. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  kweli nyani haoni kundule
   
 5. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  pinda mtoto wa mkulima toka lini?
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Chadema tuna deal na sera ya nchi (national policy -not petty issues). Ndiyo maana Dr Slaa wakati anagombea hakuahidi bajaji, au kuwalipia watu madeni ya SACCOS, wala ujenzi wa vijibarabara vya hapa na pale aili apate kura.

  Yeye alijadili sera ya kodi, mfumo wa elimu, sera za ujenzi kwa ujumla, ukubwa wa serikali, anahoja kazi wakuu wa wilaya na mikoa wakati kikwete ana deal na kazi za wenyeviti wa Halmashauri na manispaa via mabajaji.


  Kwa hiyo, Slaa anataka sera ya malipo wabunge iendane na ukuaji wa uchumi wetu wala haitendi haki kwa wafanyakza wengine nchini. Dr Slaa na wenzake kususia mishahara yao ubunge kwa kuwa wanalalamika kuwa ni mikubwa siyo utatuzi, ni sawa na kumsusia mlevi pombe. Si ndo watafurahi?


  Pili, itawapunguzia watanzania umaskini kwa asilimia ngapi?

  Si, bora akachukua halafu akatumia kwenye maandamano kuwaelimisha watanzania kama anavyofanya sasa?
   
 7. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hivi hata hayo maandamano si yanatumia hela nyingi sana? gharama za mafuta + posho kwa wabunge na wajumbe wote wanaoshiriki (maana ni wengi) na wanatumia ruzuku toka serikalini ambayo ni jasho la walipa kodi hao hao.

  Je CDM kwa kutumia mamilioni hayo yanawasaidia vipi wananchi maana naye anaendekeza porojo tu za kuwasema watu. sioni kama kuna kauli anayotoa ya kuwasaidia wananchi wanaomsikiliza wajikomboe na umasikini huu.

  CDM tujenge hoja ya kuwasaidia wananchi wapate maendeleo tuache porojo za kuwasema watu. mara leo PINDA kafanya hiki mara Mangula mara Riziwan.

  Tunachoka kusikia majina tu kila siku na hayatatusaidia kupiga hatua. kujadili watu ndiyo dalili za nchi masikini.
   
 8. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  ye anastahili kulipwa coz kazi anayoifanya wote twaiona...kazi ya kutoa tongotongo machoni mwa wenzako si ya kitoto bandugu, huyo Pinda analipwa hiyo hela kwa lipi hasa??zaidi ya kulidanganya bunge kila uchao!! Juzi kakataa gari ya mil 200 kudai mtoto wa mkulima kumbe huku pembeni ana gari ya milion 500!!

  Halafu waziri mkuu gani nchi inaenda kombo namna hii yeye yupo kimya tuuuu,yaani hana tofauti na Gamba kuu pale ikulu...hili ni genge la Maghabachori--wezi wakubwa wanakula hadi mbegu za kupanda!! Sasa kama kweli Dk Slaa ni muongeaji mzuri ww kichwa maji umempa ''ZERO''..fine!! na hao(PINDA wako na Rais wako..SI WAONGEAJI NA WALA SI WATENDAJI''...utawacredit vp??hope ni below zero, -ve!!

  Fikiria kijana...we endelea tu kuwa kwenye usingizi mzito...ngoma ndo inogile hivyo!!
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Subiri Chadema ikishika dola ndo utajua faida ya majina yaliyo kwenye shame list na mengineyo!!wote hawa watakimbizana mipakani huko kukimbia njii..!!
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hivi kwanini ccm hampendi watu tujue ukweli wa mnayoyafanya? Maandamano yanamanufaa makubwa kuelezea uovu wa ccm, wewe umeona Ruzuku ya CDM tu na ccm wanapokea shilingi ngapi tuambie wamefanyia nini mkuu!?

  Mna utajiri mwingi hamjafanya lolote na masikini CDM anajikongonya na pesa zake majungu kibao.

  Tatizo hata tshet na kanga mnazotoa zinawakost sana, AIBU KWENU CCM (si mlisema chama cha msimu vinaonekana wakati wa uchaguzi tuuu! hahahhaha mnachekesha sana)
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Anachokifanya Dr hata mshahara anaolipwa hautoshi! Kazi ya kutoa elimu ya uraia hapa nchini sio kazi ndogo. Matokeo yake tutayaona kwenye uchaguzi ujao. Watu watachagua mtu kwa kutumia ufahamu wao na sio kwa kudanganya na kofia, t shirt, na kanga, au mazoea.
   
 12. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kaka usiongee usichokijua , maandamano ya CDM hayana posho either kwa Dr slaa, mbowe pamoja na wabunge na wafuasi wa chadema.
  Kila mmoja huwa tunatumia pesa zetu mfukoni kwa chakula , malazi, na pia watu wenye kipato kikubwa kwenye chama kama wabunge huwa wanachangia shilling laki tatu na nusu kwa mwezi ili chama kiweze kujiendesha kwa kulipia vyumba vya ofisi Tanzania nzima.

  Maandamano ya CDM siyo semina elekezi za magamba ambazo kila mtu analipwa , for your information ni katibu mkuu tu kwa sasa anayelipwa mshahara katika top management ya CDM wengine ambao ni wabunge hawana wanafanya kazi za kujitolea za chama.

  Kumbuka ruzuku ya chadema bado ni ndogo haiwezi kukidhi mahitaji ya chama tanzania nzima.
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ukitaka usiingliwe mkuu punguza kashfa acheni wizi watu wakose pakuwasemea sasa tatizo mmekuwa ndo chanzo cha kuleta maneno hayo na UONGO WENU (ie mkullo)
   
 14. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  Tunachotaka ni kiongozi mwenye kuonesha mfano na mwenye kufuata kauli zake, leo anasema wabunge mishahara mikubaw 3a, kesho anakubali kulipwa mshahhara sawa na marupurupu sawa na anayolipwa mbunge ambayo yeye siku zote amekuwa anayapinga.

  Huu ni unafiki, na kusema yeye anafanya kazi nyingi za chama ndio wajibu wake, uongozi ni kujitolea na si kutaka kujinufaisha.
  Tutaamini vipi kama akijakuwa RAIS wa nchi hii CDM hawatomlipa mara 10 ya mshahara wa kawaida wa rais kwa kigezo amefanya kazi ngumu ya kuipigania nchi hii.

  Tunataka mpiganaji aliye na uchungu na nchii bila kutegemea kujilipa fadhila.
   
 15. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hivi umeandika kwa kushikiwa mtutu au ndio akilizako zilivyo........hebu jisomee ulichoandika kabla ya kuposti?
   
 16. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #16
  May 11, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwanza wengi wa washiriki na wabunge ambao hawalipwi cho chote badala yake wao ndo wanachangia hiyo oparesheni ya kuwaelimisha watanzania juu ya ufisadi wa CCM.
  Pili, utawaendelezaje watanzania bila kuwatajia majina ya wezi wanaowafukarisha? Kumbuka rasilimali zetu zinatosha kutuendeleza ila zinaibiwa na hao tunaowataja ili watanzania wawajue. Wewe unataka wafanyeje? Wakachimbe bara bara na kujenga shule na zahanati wakati hawakusanyi kodi?
  Hicho wanachofanya ya kuonesha udhaifu wa ccm ndo kazi yao kwa kutumia ruzuku yao - kazi ya kambi ya upinzani ndani na nje ya bunge. siyo kujenga shule, zahanati nk kwa kuwa hawakusanyi kodi.
   
 17. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sasa naona unamsema Dr.Slaa kwa kuongelea petty issues za Pinda na Umeme wa Jua kwenye Nyumba yake, mpaka malipo ya mshahara wake yasiyowatendea haki maofisa wa chama walio chini yake, mfano: Makatibu Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

   
 18. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hawa CDM ni wazushi, Mwenyewe Mbowe kama kiongozi wa upinzani mbona hajalikataa shangingi analolitumia la serikali?? Wakati huo huo hatujasikia pesa za ruzuku zimepelekwa matawini ili kuimarisha chama badala yake wanatumbua kupitia "MRADI WA MAANDAMANO ENDELEVU" tena maandamano yanafanyika kipindi cha kilimo. ACHENI KUDHOOFISHA KILIMO KWANZA!!!!!
   
 19. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usidanganye mtu wewe! chadema mna mambo ya kike sana,usiseme mna deal na issue wakati mmekalia kuandama watu na kudandia hoja za ccm ,mmekwenda sumbawanga mnamwandama pinda,dar mnamwandama riziwan, zanzibar mnamwamndama seif shinyanga mkasema uongo balele kafa,juzi mbeya mmedanganya watu nchi imefirisika siju uchumi mmesoma wapi ambao hautofautishi kufilisika na kukopa! hamjui hata sifa ya kukopesheka?
   
 20. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hawa CDM ni wazushi, Mwenyewe Mbowe kama kiongozi wa upinzani mbona hajalikataa shangingi analolitumia la serikali??
  KWANI UMESIKIA HILO GARI LA KIONGOZI RASMI WA UPINZANI LIKO KWENYE MAANDAMANAO?
  Wakati huo huo hatujasikia pesa za ruzuku zimepelekwa matawini ili kuimarisha chama badala yake wanatumbua kupitia "MRADI WA MAANDAMANO ENDELEVU"
  NANI KAKWAMBIA MATAWI HAYAKO IMARA?

  Tena maandamano yanafanyika kipindi cha kilimo. ACHENI KUDHOOFISHA KILIMO KWANZA!!!!!
  KILIMO KWANZA KIPI? CHA YALE MATREKTA YA JEETU HAPO MWENGE AU KIPI?
   
Loading...