Kwa hili Rais anastahili pongezi

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,481
NILIPATA kuandika miaka ya nyuma kuwa Tanzania inateswa na mambo makuu mawili; Ujuaji na ukosefu wa uadilifu.

Mosi; watu wanajua sana. Sehemu yenye kuhitaji utaalamu, yule ambaye fani haimhusu anaweza kuzungumza na kuonekana anajua zaidi.

Mwaka jana, Jumuiya ya Wanasheria Tanganyika (TLS), ilitoa taarifa kueleza tafsiri ya usahihi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kuendelea na Baraza la Mawaziri lililoachwa na Dk John Magufuli.

TLS walitafsiri Katiba ya nchi. Bila shaka kwa kuzingatia ibara ya 56, inayotaka mawaziri (akiwemo waziri mkuu), lazima kuapa kwa rais aliye madarakani.

Vilevile, ibara ya 57 (1) (f), inayoelekeza Baraza la Mawaziri kuvunjika wakati Rais mpya anapotaka kula kiapo.

Mshangao wangu, waraka wa TLS, uliosaniwa na aliyekuwa Rais wao, Dk Rugemeleza Nshala, ulipingwa vibaya sana. Tena na watu ambao hawajawahi kusoma sheria hata nusu siku.

Hio ndio Tanzania. Kila mtu anajua. Taifa ambalo watu wake hawajui kutofautisha ukosoaji na nongwa. Kupishana mitazamo na chuki.

Taifa ambalo mtu anaweza kuuhubiri ubaya wa mtu kwa sababu alisimuliwa. Nchi ambayo unaweza kuchukiwa kwa sababu ya ulichonacho. Ama akili, maarifa, cheo au mali halali.

Tanzania ni jamhuri ambayo mitandao inaweza kukuhukumu kwa shauri ambalo hulijui. Wapo watasimulia ulivyo na maisha yako mpaka mwenyewe utashangaa: “Hivi mimi nimekuwa hivi lini?”

Pili; ukosefu wa uadilifu. Hili unaweka ubinafsi. Mtu anaweza kuunga mkono jambo kwa sababu ya kutazama masilahi yake. Anaweza kupinga lenye faida kwa umma kwa kujitazama yeye.

Kuhusu uadilifu ongeza na ufisadi, uamuzi mbaya kwa nchi kwa kusukumwa na upigaji. Kwa vile yeye anapata, basi bora nchi ipigwe. Ilimradi yeye na kizazi chake wataogelea neema.

MITAZAMO BILA MANTIKI

Hili linaweza kuwa zao la ujuaji au pia ubinafsi ambalo ni tawi la ukosefu wa uadilifu.

Binadamu lazima uwe na mantiki ya kile unachokisimamia. Shabaha yako iwe kufanikisha hiyo mantiki.

Kutokuwa na mantiki ni sawa na kukosa kusudi. Yaani hujui unataka nini. Kelele nyingi za mkumbo ni kipimo cha maisha kukosa kusudi.

Mathalan, wakati wa uongozi wa Dk John Magufuli, kulikuwa na sauti mbalimbali za kutetea haki za binadamu. Kwamba haki ilikuwa inanyimwa.

Ameingia Rais Samia Suluhu Hassan, amesema haki haipaswi kuwa zawadi. Akakemea watu kusotea haki zao. Mambo yanabadilika.

Waliokuwa wanashikiliwa mahabusu kwa kesi za kubambikiwa, wakaachiwa. Akafanya mabadiliko Takukuru na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka.

Kama wewe ulikuwa unatetea haki za binadamu kwa kusudi la watu kusota kupata haki zao. Kubambikiwa kesi. Unapaswa kuweka tiki kuwa kuna mambo yamefanyiwa kazi.

Ukiendelea kupaza sauti za “a luta continua", bila kuweka tiki kwa yale ambayo mabadiliko chanya yamefanyika, ni harakati bila malengo.

Uhuru wa siasa ni jambo lililopigiwa kelele mno. Kipindi cha Magufuli, shughuli za kisiasa ziliharamishwa. Katiba ilivunjwa. Na wanasiasa wakanywea.

Rais Samia ameunda kikosi kazi. Kichakate maoni ya namna ambavyo shughuli za siasa zinapaswa kuendeshwa.

Najaribu kuelewa lengo kwamba sheria zipo na Katiba inatamka. Hata hivyo, alitokea kiongozi mmoja akakanyaga kila kitu.

Je, Rais atamke tu “ruksa" kama alivyoamua Rais Ali Hassan Mwinyi, au kupitia mchakato mzuri na kuweka msingi ambao hautakuja kubadilishwa kienyeji na mtu mmoja?

Kwa yule ambaye alikuwa anapinga shughuli za kisiasa kukandamizwa, kimantiki na kwa malengo, atatoa ushirikiano ili kujenga mifumo mizuri. Tiki ataweka baada ya mabadiliko kutokea.

Hata hivyo, mwenye malengo mazuri zaidi ataona dalili njema na kuheshimu nia inayooneshwa katika kuelekea suluhu ya jambo lenyewe.

Kutotoa ushirikiano kwa kikosi kazi, na kubaki kunung'unika wakati mlango wa kupokea hoja umefunguliwa, ni dalili ya kupigana vita bila kuwa na kusudi.

Peleka hoja, zisipofanyiwa kazi, utakuwa na ujasiri wa kukosoa dhamira ya kikosi kazi au uadilifu wa wajumbe walioteuliwa. Vinginevyo, baadaye unaweza kulaumu, halafu ukajibiwa “mbona tulikuita hukuja kutuletea hoja zako?”

Tunapaza sauti ili iweje? Tuonekane tunajua sana? Tutambulike kuwa ni wapiganaji? Tupate umaarufu? Au shida yetu ni kuleta mabadiliko?

Mpaza sauti mwenye kusudi la kuleta mabadiliko, ndiye mwenye mantiki. Hivyo, akiona alichokuwa anakipigia kelele kinashughulikiwa au kimepata ufumbuzi, atafurahi. Atajiona mshindi.

Ukiwa na mpaza sauti ambaye anapoona hoja yake inafanyiwa kazi ananuna kwa wivu wa kukosa agenda, huyo hana mantiki.

Taifa limekaa miaka sita bila wafanyakazi wa umma kuongezewa mishahara. Hali imekuwa mbaya. Bei za vitu zinapanda lakini fedha inayoingia ni ileile.

Mei Mosi 2021, Rais Samia alikuwa na mwezi mmoja na siku 11 tu ofisini. Akawaambia wafanyakazi kuwa hali ya uchumi ilikuwa mbaya. Wampe muda. Aliahidi kuweka nyongeza katika bajeti ya 2022.

Mei Mosi 2022, Rais Samia akasema “lile jambo letu mwaka huu lipo". Kwa kiasi gani, akaomba apewe muda angetangaza.

Aliyekuwa anapaza sauti kwa mantiki, angevuta subira, maana Mei Mosi mpaka Julai Mosi ni siku 61 tu. Kama ni mwongo, mbona njia ya mwongo ni fupi?

Kuja na mifano yenye kupima ujazo wa kauli ya Rais Samia “jambo letu lipo" dhidi ya tamko la Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, aliyeongeza asilimia 12 Mei Mosi, au Rais Hussein Mwinyi, aliyepandisha kwa asilimia 15 Zanzibar, haikuwa sawa.

Kisha, Rais Samia akapandisha mshahara kwa asilimia 23.3. Watu wamefurahi. Mpaza sauti mwenye mantiki atajipongeza kwamba kilio kimesikika, kimefanyiwa kazi.

Asiye na mantiki bado atazodoa. Anasema “kwani ni zawadi? Nyongeza ya mshahara ni takwa la kisheria". Huyu anayesema hivi alikuwa hai miaka yote bila nyongeza ya mshahara.

Lazima kujitengeneza kuwa wapaza sauti wenye mantiki. Kama mishahara imeongezwa. Furahi. Ukiweza pongeza. Kisha tazama lingine lenye upungufu, ibua. Tuwe wakosoaji wa kujenga. Sio wabeba mimba za nongwa.

Mafuta yamepanda bei na kupandisha bei za bidhaa nyingi na huduma. Tulipaza sauti kwa mantiki kwamba bei ya mafuta ishuke.

Serikali imetoa Sh100 bilioni ili bei ya mafuta ishuke kuanzia Juni Mosi. Kisha, kuanzia Julai Mosi, bei itashuka kwa Serikali kujibana kwenye matumizi yake ya ndani. Hivyo ndivyo nilimwelewa Rais Samia.

Hapa nilipo nasubiri Juni Mosi, nione tangazo mafuta yatauzwa bei gani. Tatizo kabla Juni haijafika, watu wanauliza mbona bei haushuki. Kwani Juni tayari?

Mpaza sauti mwenye mantiki atamshauri Rais Samia kwamba asiwe anasubiri mpaka wananchi waumie ndio achukue hatua. Mwenye nongwa, atakasirika bei ya mafuta ikishuka, eti anafilisiwa hoja.

Rais Samia anawaambia wanaharakati “yeye ni mama", hivyo hakuna sababu ya kupambana, bali waketi na kuzungumza ili kujenga nchi moja.

Asiye na mantiki ya kile anachokisimamia anajibu “mama yangu yupo nyumbani, wewe sio mama yangu, usitafute huruma hapa". Akili gani hii?

Kanuni ya Abraham Lincoln ni kutaka mtu uwe ngangari unapokutana na ngangari, mpole kwa mpole. Alisema: “Gentle with gentle people, tough with the tough.”

Dk Magufuli alikuwa tough, huyo ndiye ilitakiwa kwenda naye kiugumu-ugumu. Rais Samia ni gentle. Vema kuendana naye.

Shida inakuja hapa; wakati Magufuli alikuwa tough, watu wakawa wapole. Haongezi mishahara na watu walitulia. Watu waliokotwa wakiwa maiti fukwe za Bahari ya Hindi na Mto Ruvu, hakukuwa na maelezo na hakuna aliyemtikisa Magufuli.

Tundu Lissu alipigwa risasi na hakuna kilichofanyika. Hakukuwa na upelelezi, fedha za matibabu alinyimwa ingawa alikuwa mbunge. Mwisho, na ubunge alifukuzwa. Alifanywa nini? Aliachiwa Mungu. Taifa la waomba Mungu.

Ben Saanane, Azory Gwanda, Simon Kanguye. Walipotea. Je, tuna matumaini ya kuwaona tena? Kesi za uhujumu uchumi zilikithiri. Wafanyabiashara walidhulumiwa mpaka mitaji. Tulikuwa tough? Hapana, tulibaki wapole.

Si kwamba Rais Samia asikosolewe. Nchi ‘itaboa’ kama kila mtu atamsifu. Kukosolewa ni afya. Kumkosoa kujengwe na mantiki.

Binafsi napenda kumwelewa mtu kabla sijamkosoa. Utamwelewa kama utajipa nafasi ya kuelewa. Utajenga hoja ze mantiki kwa kuwa ukielewa utajua usahihi ulipo na makosa yake.

Mkosoe kisha mwache afanyie kazi. Ukiona anapuuza, endelea kujenga hoja mpaka ieleweke. Ukiona ukosoaji wako umepokelewa na unafanyiwa kazi, vuta subira au shauri njia bora zaidi za kuliendea jambo.

Tanzania ni nchi yenye Rais na wananchi. Sio Rais na maraisi. Kwamba maraisi mtaani na mitandaoni badala ya kutambua wajibu wa kutoa maoni na kushauri, wanataka kumwongoza Rais.

Kama tuna malengo ya kusaidia nchi, tutashauri kwa kujenga. Tusiwe watu wa nongwa za “kwa nini amekuwa rais". Rais ni mmoja. Tukosoe kwa kujenga. Tuwe imara kutetea masilahi ya nchi. Tusifie ikibidi. Lengo ni nchi isonge mbele.

Credit: Luqman MALOTO
 
TANZANIA NI NCHI YENYE RAIS NA MARAISI?

Kumbe wenye akili mpo humu mnakausha tu siku zote hizi, sio vema. Kwa hali ilivyo elimu km hz zinatakiwa kutolewa mara kwa mara humu.....
 
Ahsante mkuu kwa kutenga muda wako kuandika makala ndefu. Nimesoma nimefika mahala nikahisi kuchoka kabisaa
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom